Wazazi wa mtoto huyu watakesha wanabubujikwa machozi ya furaha na kumuombea maisha marefu Rais Samia

Wazazi wa mtoto huyu watakesha wanabubujikwa machozi ya furaha na kumuombea maisha marefu Rais Samia

Ndugu zangu Watanzania,

Kila nikikaa nikawaza na kufikiria makubwa na mazito anayoyafanya Rais Samia katika Taifa letu kugusa maisha ya watanzania.Nabakia kusema Mama yetu Mpendwa na Rais wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Alizaliwa katika ardhi ya Tanzania kuja kuwafuta watu machozi na kuwarejeshea tabasamu katika mioyo yao.

Mama yetu Daktari Samia ni Mama Mwenye huruma isiyoelezeka wala kupimika katika mzani.Ni mama mwenye moyo wa upendo wa hali ya juu sana,ni Mama mwenye utu na kuguswa na matatizo ya watu.ni Mtumishi wa kweli wa watu ,ni Mama ambaye moyo wake na Maisha yake amejitolea kwa ajili ya kuwatumikia watanzania kwa moyo wake wote.

Embu fikiria ndugu yangu mtanzania, Unafikiri wazazi wa Mtoto huyu ambaye Mama yetu na Rais wetu mpendwa Daktari Mama Samia ameahidi kumhudumia na kumsaidia kupata mguu wa bandia . unafikiri wazazi wa Mtoto huyu wana furaha kiasi gani mioyoni Mwao? Unafikiri ni vipi wanaweza sahau upendo na huruma ya Rais Samia kwa mtoto wao? Ni vipi watalala na wakapata usingizi bila kumuombea maisha marefu Rais Samia?

Unafikiri Mtoto huyu na Mwanafunzi huyu aliyegusa hisia za watu atamsahau vipi Rais Samia? Unafikiri ni furaha kiasi gani atakayokuwa nayo mtoto huyu pindi atakapopatiwa Mguu wa Bandia? Unafikiri anaweza vipi kulisahau jina la Rais Samia moyoni Mwake katika uhai wake wote hapa Duniani ? Unafikiri atawasimulia nini watoto wenzake mpaka wajukuu zake panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu?

Ndugu zangu Watanzania unaweza kuwa na chuki binafsi na Rais Samia .lakini ukweli ni Kuwa Rais Samia ni mtu na nusu,ni kiongozi ambaye tunapaswa kumuombea Maisha marefu na kumuunga mkono kuendelea kutuongoza Watanzania. Ni kiongozi ambaye wapo watu watakuja waje wamkumbuke sana na kumlilia sana kwa mazuri aliyo watetendea atakapomaliza muda wake wa Urais hapo 2030 panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu.

View attachment 3045822

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Amefanya vizuri sana Mama Samia...Hongera Kwake.
 
Mimi ni Rais wa wapi??
Auunafikiri Rais ni kama wewe??
Kwa hiyo unasubiri hadi uwe Rais ndio usaidie watu? Ni wapi katika majukumu ya Rais au katika katiba au sheria yoyote ile inasema Rais analazimika kuwasaidia kupata miguu au mikono bandia wale waliovunjika? Hujuwi kuwa huo ni moyo wa huruma na upendo wa Rais Samia kaka kiongozi na mzazi mwenye uchungu na maisha ya watu?
 
Wewe hujitambui!
Kwa nafasi yangu nawasaidia wengi!
Lakini SSH kwa nafasi yake anapaswa kujikita kusaidia waTanzania wote kwa usawa ule ule. Ni jukumu lake kisera na kisheria kama kiongozi!
Moyo wa huruma kwa mtu mmoja mmoja anayejitokeza kwenye ziara zake tafsiri nyepesi ni kuwa anawatumia kwa manufaa binafsi ya kisiasa!

Na kama unaona Rais wako yupo sawa basi yeye, wewe na wenzako hamjui majukumu ya Rais wa nchi.
Endeleeni!
 
Kwa hakika Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan, Mama wa huruma na upendo anastahili pongezi na kuungwa mkono kwa moyo wake wa upendo kwa watu. Kwa hakika Mama ni zaidi ya kiongozi.Ni mama kwelikweli ambaye anajuwa uchungu wa Mwana.
Kwamba amesafiri(V8 200+) kwenda kutoa mguu wa bandia ambao hata wewe ungeweza kununua? shame on you
 
Kweli wewe hujitambui hata kidogo.unauliza Mheshimiwa Rais kasomesha na kuponya wangapi? Kwamba huoni wanafunzi wanaosoma bure mamilioni kwa mamilioni? Huoni wanafunzi kwa maelfu kwa wanaopata mikopo vyuo vikuu? Halafu usivyo na akili unasema ameponya watu.hivi una akili kweli wewe tangia lini Malisa akawa na uwezo wa kuponya? Hata angekuwa daktari hawezi kumponya mtu .kazi ya mtu au daktari ni kumtibu mtu na kazi ya uponyaji ni ya Mungu Mwenyewe na pekee .acha kufuru na ujinga wako hapa.
We ndo bumunda haswaaa, kama syo kodi zetu angesomesha.
Tatizo wewe ni parasite huna unachochangia kwa wanafunzi kusoma
 
Kweli wewe hujitambui hata kidogo.unauliza Mheshimiwa Rais kasomesha na kuponya wangapi? Kwamba huoni wanafunzi wanaosoma bure mamilioni kwa mamilioni? Huoni wanafunzi kwa maelfu kwa wanaopata mikopo vyuo vikuu? Halafu usivyo na akili unasema ameponya watu.hivi una akili kweli wewe tangia lini Malisa akawa na uwezo wa kuponya? Hata angekuwa daktari hawezi kumponya mtu .kazi ya mtu au daktari ni kumtibu mtu na kazi ya uponyaji ni ya Mungu Mwenyewe na pekee .acha kufuru na ujinga wako hapa.
We ni mwehu,hujitambui, poyoyo.
Bila jitihada za Malisa kwa juhudi zake binafsi na si kwa kodi za watanzania, ameweza kosomesha waloshindwa kusomeshwa ma SSH,ingia kwa page yake fb utaona maana kukuambia tu huku kichwa chako ni sawa na pango la nyoka
 
Wajibu wake kivipi? Kwani kuna mahali sheria inamtaka kuwatibu wote waliopata ajali na kuvunjika miguu? Kuna mahali sheria inamtaka kuwanunulia miguu ya bandia au mikono ya Bandia ambao hawana? Huoni hiyo ni huruma na moyo wa upendo alio nao Mheshimiwa Rais
Naanza kuhisi tunashindana na mwehu asiyejua RAIS wa JMT ni nani
 
Hii ni zaidi ya wivu... Ni UPENDELEO wa wazi!
Anyways, unaweza kuweka bayana vigezo vilivyotumika kumpa huyo mtoto hiyo nafasi huku wengine nchi nzima hawajui hatma yao?

Use your brain wisely if at all you have it!
Mbona swali lako halina mantiki ndugu yangu? Kwani katiba na sheria inasema nini mtu akiugua na kupata matatizo kama aliyoyapata huyo mtoto au yule mama aliyesaidiwa pale mji mdogo wa Mlowo kulipiwa matibabu ya mtoto wake au yule mwingine ambaye amepata majereha kutokana na ajali?? Kwanini mnashindwa kupongeza panapostahili kufanya hivyo.kumbuka Mh Rais hawajibika kumtibu kila mtu mwenye ugonjwa hapa nchini.hats Marekani tu kwenyewe hakuna suala la namna hiyo.anachofanya Rais wetu ni huruma na upendo tu alionao Mama yetu kama Mzazi.
 
Najuwaga hunaga akili mdogo wangu ila sikujua kama umefikia huku😀😀😀
Hata kwa posho yako ya UWT ungeweza kununua hauzidi laki 2, hapo hapo kuna RC/RAS/RMO/REO/DC/DAS/DED/Mbunge/DMO/DEO/madiwani wote hao wameshindwa kutoa mguu wa bandia wa laki 2 mpaka Rais aje kuahidi? shame on you
 
Wewe Umenunulia wangapi mpaka sasa?
 
Back
Top Bottom