Wazazi wazembe wanatoa Elimu kama Urithi, Sheria ya Mirathi inakataa Elimu sio Urithi, Biblia inataka baba kuacha Urithi

Urithi katika agano jipya pia unaonesha uko tofauti, je umesoma hii:m toka kwa Yesu mwenyewe?

‭‭Lk‬ ‭12:13‭-‬15‬ ‭SUV‬‬
[13] Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu. [14] Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu? [15] Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.

Mbona unaleta mstari wa ndugu kuombana urithi.

Mtoa mada anaongelea mzazi yaani baba kumpa mwanae urithi. Wewe mstari wako unaongelea mtu kumuomba ndugu yake urithi.

Uhusiano wa baba na mtoto ni mkubwa ndio maana baba kapewa wajibu wa kuacha urithi mpaka kwa wajukuu zake.

Ndugu hajapewa wajibu kama wa baba kwa mwanae
 
Nimeishi sweden na uk .hakuna mambo ya kurithi ila baba anakupa mtaji unasepa.mfano trump baba yake alikuwa tilionaire lakini alimpa bil 2 tu akaanze maisha .mali unajitafutia mali ya baba yako ni ya yeye kula bata na mama yako na mademu zake

Kama kusingekuwa na urithi basi hata hiyo nchi ya Sweden isingekuwepo na isingekuwa nchi ya ya Wasweden.
Wasweden waleo wamerithi hiyo nchi kutoka kwa Babu na baba zao.

Ukisema hakuna mambo ya urithi unauhakika kwenye sheria na mahakamani za Sweden hakuna mambo ya Urithi?

Kwenye huu dunia kiumbe chochote chenye utashi lazima kurithisha sio tûu maumbile ya mwili bali hata rasilimali.

Maskini ndio wanasemaga hakuna urithi kwa sababu wao hawana vya kurithi, lakini Watu wenye akili kubwa na matajiri huwezi kusikia wakifikiria jambo hilo achilia mbali KUSEMA.

Labda hujui maana ya urithi. Urithi ndio maana halisi ya maisha
 
Na wanakuwa wakali balaa, utasikia nimeuza mali zangu kukosomesha......mentality ya wazazi wa namna hii ni mtihani kwelikweli.

Hayo maneno tunaambiana maskini tu. Urithi ni mali na basic education tu ya kuendesha hizo mali.

Hayo makaratasi mtarithishana huku hamna hela wakati wenzenu wanaachia hadi wajuukuu zao mali. Kusingekua na kina Mo au Azam kama wangekua wanaachiana vyeti tu.
 
Ibrahim alimuachia Isaka, na Isaka akamuachia yakobo.

Hawa jamaa walikuwa ni masuper billionea, ila walirithi maandalizi ya kiakili na mali kutoka kwa Ibra.

Mababa wa Imani wanatakiwa kuiga hii
 
Kama kusingekuwa na urithi basi hata hiyo nchi ya Sweden isingekuwepo na isingekuwa nchi ya ya Wasweden.
Wasweden waleo wamerithi hiyo nchi kutoka kwa Babu na baba zao.

Ukisema hakuna mambo ya urithi unauhakika kwenye sheria na mahakamani za Sweden hakuna mambo ya Urithi?

Kwenye huu dunia kiumbe chochote chenye utashi lazima kurithisha sio tûu maumbile ya mwili bali hata rasilimali.

Maskini ndio wanasemaga hakuna urithi kwa sababu wao hawana vya kurithi, lakini Watu wenye akili kubwa na matajiri huwezi kusikia wakifikiria jambo hilo achilia mbali KUSEMA.

Labda hujui maana ya urithi. Urithi ndio maana halisi ya maisha
Mkuu mm nimezaa na msweden baba yake ana hadi viwanda huyu dada nliishi nae maisha ya kawaida na nimuajiriwa kampun ingine sio ya babake .na wasweden mali huwa wanadonate asilimia kubwa hawawapi watoto.akiwa na shida wanamkopesha .
 
Kijana akifikisha miaka 18 baba yake alikuwa anampa shamba, mifugo na malazi. Kisha anamuozesha.

Kweli kabisa jadi zilijali wazazi kutoa ajira kupitia urithi, ila sasa wazazi wameitupia serikali jukumu hili la msingi kuwa familia itoe urithi na ndani yake itapatikana kujitegemea kwa kujiajiri.

Vijana tunaacha mikorosho, minazi, mitumbwi, nyavu, mifugo vijijini kukimbilia kuwa bodaboda na machinga.

Pengine siyo lawama zote tuwabebeshe wazazi wetu, inawezekana hatutambui urithi mkubwa wa ardhi, mifugo, ngalawa n.k inayoweza kutufanya hakuna haja kukimbilia mijini.

Mjini tuwaachie wale ambao tayari wamewekeza, sisi ambao wazazi wetu ambao hawajawekeza mijini tubaki shamba kuendeleza urithi vijijini.
 
Ni sawasawa.
Ndio nakuuliza Sweden hakuna sheria za mirathi?

muongo huyo. sweden familia tajiri ni Wallenberg family, hiyo familia wamepata utajiri kwa kurithishana vizazi na vizazi

kwa miaka zaidi ya 200 hiyo familia ndio familia tajiri kuliko zote sweden. toka mwaka 1700s huko mpaka leo vizazi vyao vinaendeleza utajiri kwa kurithisishana. Generation ya tano ndiyo inayosimamia mali mwaka huu
 
Mkuu mm nimezaa na msweden baba yake ana hadi viwanda huyu dada nliishi nae maisha ya kawaida na nimuajiriwa kampun ingine sio ya babake .na wasweden mali huwa wanadonate asilimia kubwa hawawapi watoto.akiwa na shida wanamkopesha .

mkuu toka miaka ya 1700s mpaka leo familia tajiri sweden ni Wallenberg family. utajiri wameupata kwa kurithisishana vizazi na vizazi vya hiyo familia. aliyetafuta mali Per Hansson Wallenberg alishakufa toka mwaka 1741 yaani miaka 300 iliyopita . ila mpaka leo vitukuu vyake ndio wanaendeleza utajiri huo
 
View attachment 2897775

tunaanza na mistari ya biblia

Mithali 13:2 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi​

Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na
Bwan
a”

NIMEGUNDUA WAZAZI WA ZAMANI WASIOENDA SHULE WANA AKILI KULIKO WAZAZI WA KISASA.

Elimu ya Mzungu imezalisha wazazi wajinga kuliko wazee ambao hawajapata hiyo elimu.

Wazee wa zamani hawakuwa na elimu ila walikuwa na akili sana. Walikuwa wanaandaa ajira za watoto wao.

Walijua mahitaji ya msingi ya binadamu ni nini chakula, Mavazi na malazi.

Baba ilikuwa wajibu wake kuhakikisha kizazi chake kinapata uhakika wa chakula, mavazi na maradhi kwa wakati.

Kijana akifikisha miaka 18 baba yake alikuwa anampa shamba, mifugo na malazi. Kisha anamuozesha.

Hapo maana yake ajira ameshampatia mwanae kwenye hilo shamba na mifugo

Wazazi wa siku hizi mtoto wa miaka 25 hapewi chochote kwa kisingizio amepewa elimu. Na elimu ndio urithi.

Ukweli elimu sio urithi. Hakuna sheria ya mirathi inayotambua elimu kama urithi.

Wazazi wa zama hizi Wanajifanya wanapenda dini ila mafundisho ya dini kuhusu urithi wanayakataa. Biblia inasema Nyumba na mali mtu atapewa na baba yake. Hakuna walipo sema elimu ndio urithi

Wazazi wengi siku hizi wanatumia asilimia kubwa ya vipato vyao kusomesha watoto wao, ila wanasahau wajibu wao wa kidini hasa Wakristo kuwarithisha mali hao watoto wao.

Watoto wengi wamesoma, wamemaliza vyuo vikuu ila hawajapata ajira. Wanashinda wanazurura tu na kulala nyumbani kutwa nzima. Sababu baba hana rasilimali za kumpa mtaji. Ama baba amefariki hajamuachia urithi wa mali, sababu kuu ameshapewa urithi wa elimu.

Elimu ni basic need kama kumpa mtoto chakula, Hivi unaweza wapa watoto chakula ati ndio useme Urithi,
Elimu ni basic need Kwa mtu inayomsaidia kutumia Rasilimali. Mzazi unapaswa uache Urithi WA rasilimali ambazo mtoto atazitumia kuendesha maisha yake baada ya kupewa elimu. Elimu bila Rasilimali ni Sawa na mdomo pasipo Meno.

Baba yake Mo dewji kamsomesha Mo dewji IST na chuo kikuu kikubwa duniani.. ila bado akaja kumpa urithi wa mali yaani kampuni ya Mohammed Enterprises

Tatizo la Ajira linaletwa na Wazazi wahuni.

Hujamrithisha mtoto Mali ataachaje kukosa Ajira?

Maisha ni yaleyale Ila binadamu ndio wanajifanya yaonekane yamebadilika

Kwa maoni yako je elimu ni urithi wa kuwekewa nguvu kuliko urithi wa mali ?
Umeongea jambo la msingi sana lakini kwa jinsi ulivyofikisha ni kama upo kanisani vile! au labda tupo kwenye jamii ambayo the only relevant reference ni biblia. Makosa kama haya huwa yanaashiria mgando wa fikra za mtu kwa sample yake ndogo aliyoisoma na sio jamii nzima kiujumla. Kwa mtazamo wangu tafiti yako inaongelea jamii moja tu ya waswahili tena wanaoamini biblia.

In reality tatizo lililopo ni la kijamii ya kiafrika zaidi na wala haihusiani na mafundisho ya dini flani! wenzetu waarabu na wahindi ni mabingwa katika nyanja hiyo ya urithi wa mali na biashara za familia. Weka mafundisho ya dini yako pembeni na tambua tatizo tulilonalo ni utumwa wa fikra za kimagharibi, wamevunja fikra zetu na wametufanya tufikirie vile wanavyotaka wao.
 
ndo wale wazazi unakuta kwenye harusi wanaitwa waseme zawadi waliomuandalia kijana/binti yao....unakuta kanaletwa kajifuko unaweza sema labda ni burungutu la ela...unaona mtu anatoa biblia alafu anachukua MIC ''Mimi kama baba napenda kumpa mwanangu zawadi ya biblia'' KAMALIZA 😁

Wazee wana uhuni mwingi sana
 
Mleta uzi ana hoja ila hajatulia tu.

Ni kweli elimu sio urithi na kamwe haitawahi kuwa urithi.

Urithi ni nini?, urithi ni mali anayoacha marehemu aliyopewa mpendwa wake aliye hai.

Sasa elimu mfano wewe una elimu.ya chuo kikuu (elimu ya vyeti) ni namna gani utairithisha hiyo elimu yako kwa wanao?, yaani mwanao aje atumie vyeti vyako marehemu baba yake.

Maarifa na ujuzi navyo sio urithi bali huwa ni zawadi tu mtu anaamua kutoa kwa kizazi chake kwa kukipa maarifa au ujuzi alionao. Na huu ujuzi na maarifa hutolewa mtu akiwa hai sababu huutoa yeye mwenyewe. Zaidi ya hapo labda aandike kitabu.

Urithi ni matokeo ya mali za mtu baada ya huyo mtu kufariki. Hivyo elimu haiwezi kamwe kuwa urithi.

Ndio maana mtu hawezi kuandika wosia eti amemrithisha mtoto wake elimu yake ya udaktari 😂😂 kitakuwa ni kituko na huo wosia unaweza ukapuuzwa wote.

Naungana na mtoa mada, elimu sio urithi.
 
View attachment 2897775

tunaanza na mistari ya biblia

Mithali 13:2 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi​

Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na
Bwan
a”

NIMEGUNDUA WAZAZI WA ZAMANI WASIOENDA SHULE WANA AKILI KULIKO WAZAZI WA KISASA.

Elimu ya Mzungu imezalisha wazazi wajinga kuliko wazee ambao hawajapata hiyo elimu.

Wazee wa zamani hawakuwa na elimu ila walikuwa na akili sana. Walikuwa wanaandaa ajira za watoto wao.

Walijua mahitaji ya msingi ya binadamu ni nini chakula, Mavazi na malazi.

Baba ilikuwa wajibu wake kuhakikisha kizazi chake kinapata uhakika wa chakula, mavazi na maradhi kwa wakati.

Kijana akifikisha miaka 18 baba yake alikuwa anampa shamba, mifugo na malazi. Kisha anamuozesha.

Hapo maana yake ajira ameshampatia mwanae kwenye hilo shamba na mifugo

Wazazi wa siku hizi mtoto wa miaka 25 hapewi chochote kwa kisingizio amepewa elimu. Na elimu ndio urithi.

Ukweli elimu sio urithi. Hakuna sheria ya mirathi inayotambua elimu kama urithi.

Wazazi wa zama hizi Wanajifanya wanapenda dini ila mafundisho ya dini kuhusu urithi wanayakataa. Biblia inasema Nyumba na mali mtu atapewa na baba yake. Hakuna walipo sema elimu ndio urithi

Wazazi wengi siku hizi wanatumia asilimia kubwa ya vipato vyao kusomesha watoto wao, ila wanasahau wajibu wao wa kidini hasa Wakristo kuwarithisha mali hao watoto wao.

Watoto wengi wamesoma, wamemaliza vyuo vikuu ila hawajapata ajira. Wanashinda wanazurura tu na kulala nyumbani kutwa nzima. Sababu baba hana rasilimali za kumpa mtaji. Ama baba amefariki hajamuachia urithi wa mali, sababu kuu ameshapewa urithi wa elimu.

Elimu ni basic need kama kumpa mtoto chakula, Hivi unaweza wapa watoto chakula ati ndio useme Urithi,
Elimu ni basic need Kwa mtu inayomsaidia kutumia Rasilimali. Mzazi unapaswa uache Urithi WA rasilimali ambazo mtoto atazitumia kuendesha maisha yake baada ya kupewa elimu. Elimu bila Rasilimali ni Sawa na mdomo pasipo Meno.

Baba yake Mo dewji kamsomesha Mo dewji IST na chuo kikuu kikubwa duniani.. ila bado akaja kumpa urithi wa mali yaani kampuni ya Mohammed Enterprises

Tatizo la Ajira linaletwa na Wazazi wahuni.

Hujamrithisha mtoto Mali ataachaje kukosa Ajira?

Maisha ni yaleyale Ila binadamu ndio wanajifanya yaonekane yamebadilika

Kwa maoni yako je elimu ni urithi wa kuwekewa nguvu kuliko urithi wa mali ?
Tafuta chako, acha kutegemea urithi wewe.

Kuangalia sana mali za urithi ni ishara ya ujinga na uzembe, na ndiyo mwanzo wa kuua wazazi ili urithi mali.

Mzazi akiyetafuta chake kivyake hana obligation ya kujupa urithi, hata akiamua kugawa mali yake yote kanisani, msikitini au kwa yatima ninsawa, hiyo no mali yake, si yako.

Usiikodolee macho ukilazimisha upewe urithi.

Tafuta yako na wewe.
 
We ni mpagani huwezi kumuelewa mleta mada

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom