Wazazi wengi wa Kitanzania hawana mali za kuwarithisha watoto wao zaidi ya Simba na Yanga

Wazazi wengi wa Kitanzania hawana mali za kuwarithisha watoto wao zaidi ya Simba na Yanga

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari zenu!
Mada inajieleza.
Wazazi wengi bongo hawana cha kuwarithisha watoto wao zaidi ya Simba au Yanga.
Jitahidi ufanye chini juu uache urithi wa kueleweka.
Screenshot_20241019-150219.jpg
 
Hata wewe watoto wako watakuwa wanakushangaa Kwa kusema kwanini baba akuwekeza katika biashara mbali mbali akaamua kuridhika na mshahara wa serikali tu
 
Jamii ya watanzania inaongoza katika ujinga na kua na akili finyu katika ukanda wa Africa mashariki.
Mimi hoja hii naiunga mkono asilimia mia..! naongezea Afrika mashariki na kati, hata gazeti la mwananchi limewahi chapisha habari ukurasa wa mbele kbs inayothibitisha ujinga wa wananchi wa taifa hili ukilinganisha na mataifa mengi ya afrika. HILO GAZETI LILIPOSTIWA HUMU JF
 
Unakuta familia nzima baba mama na watoto wanawajua mpaka makocha wa viungo na daktari wa timu.. ukiuliza asili ya babu wa babu yao hawajui walitoka wapi ?
😀😀😀
 
Unajua kwanini Afrika kuna curroption na watu kufuja pesa na uroho na uzandiki ? Mawazo kama yako yaani mtu anaiba ili mpaka vitukuu vije kutafuna wakati cha muhimu kuwarithisha watoto wako ni Elimu ya kuweza kupambana na Mazingira...,

Hilo la kuhakikisha majority wanatoka kwenye Tabaka la Have Nots ni watunga Sera ambao tunawalipa wameshindwa kuhakikisha mtu anapata Ujira wa kuweza kupata basic needs na akizeeka retirement plan.... Na hata hao CCM hio ndio ilikuwa Misingi yao.....

"CHAMA CHETU KINASEMA - mtu mwenye Afya ambaye tumeshindwa kumpa njia halali ya kujipatia riziki yake...., Nawaomba ardhi - hakuna ardhi; hamnipi ardhi, Mnasema "Ardhi hakuna". Naomba kazi ya kibarua basi, Nipeni basi ya kibarua, "Hamnipi kazi ya kibarua. Mimi niko tayari kabisa kufanya kazi au ya kulima au ya kibarua chochote nipeni. Hamnipi Chama Chetu kinasema MTANILISHA".
 
Back
Top Bottom