Wazee wenye hekima ndani ya CC ya CCM. Msirudie kupitisha Mgombea Mwenye kaliba ya Magufuli

Wazee wenye hekima ndani ya CC ya CCM. Msirudie kupitisha Mgombea Mwenye kaliba ya Magufuli

Najua ni namna gani Rais na mwenyekiti wa CCM alivyo na nguvu kwa hapa nchini katika kipindi cha kupitisha jina la mgombea wa chama chake.

Kwa mazingira hayo, wenye nguvu na maamuzi makubwa ndani ya chama cha mapinduzi ni Mwenyekiti na Rais wa Tanzania mama Samia, Lakini pia huwezi kumkosa kikwete na Mangula kwa wakati huu.

Chondechonde, Makosa mliyofanya mwaka 2015 kwa kumleta magufuli yalikuwa ni zaidi ya mateso kwa taifa, na kama mungu asingeingilia kati taifa lingekuwa kwenye mateso kwa MDA mrefu sana, isingekuwa rahisi kuponyoka kwa ule mfumo ambao kwao ulishaanza kuonekana ndio utendaji wa kutukuka.

Kilichokuwa kinafanyika awamu ya tano kilikuwa hakina tofauti na kilichokuwa kinafanyika Rwanda na kupelekea genocide, It was just the matter of time, tulikuwa tayari tumechukua uelekeo kuelekea kwenye tatizo lenyewe.

Viongozi waliopewa nyadhifa kutuongoza walitufanya tuishi kama tumbili ndani ya nchi yetu, unaamka asubuhi unasali kwa dini zote ili usiingie kwenye mikono yao ukapotezwa.

Chondechonde mama msije mkajisahau mkaturudisha huko tena. nashauri hata Waziri Mkuu,Majaliwa akimaliza mda wake muacheni akalime huko lindi, ndio mazao ya mwendazake hayo.

Tupeni watu wenye hofu ya mungu na kuona kila mtanzania anastahili kufurahia maisha akiwa ndani ya nchi yake.
Kwa sasa watu hawana pesa lakini wana amani na furaha tele. MUNGU NA ASHUKURIWE.

Mungu kamtwaa Magufuli kwa sababu maalum, aliona jinsi watanzania walivyoteseka.
Ww hujitambui 👆!
 
Tuombe kuwe na katiba mpya ile aliyoandaa warioba naamini itasaidia Sana kuanzua katika vyama vya siasa,uchaguzi na hata ndani ya utawala
 
Tulipata Rais wa hovyo sana. Kaharibu sana hii nchi. Kaharibu hata mifumo ya uendeshaji serikali.....hakuna sheria au kanuni. Ni matamko tu na ubabe wa madaraka. Alishindwa kujenga taasisi imara ya urais. Ikabakia kila kitu kinategemea yeye kaamkaje. Akisema piga risasi, unapigwa tu.

No wonder hata aliyekuwa makamo wake sasa (akiwa Rais) analazimika kunafanya marekebisho makubwa sana kurudisha nchi kwenye mstari na ustaarabu wa utawala bora, wa sheria na haki.

Katika hali ya kawaida, usingetegemea mabadiliko makubwa hivi kama nchi ingalikuwa imeendeshwa kitaasisi na si kwa matakwa ya mtu mmoja very abuseful na mwenye miguvu iliyopitiliza ya kikatiba na kisheria

Ukweli mtupu
 
Mabadiliko makubwa yapi mkuu? Kama watendaji wakuu wote wa serikali ni wale wale walio kuwa awamu ya 5, makamanda ni wale wale. Tafakali msemo wako kuwa mama kafanya Mabadiliko makubwa. Ukitoa couch lako la kukalia kulia ukaliweka kushoto mwa chumba chako si Mabadiliko makubwa.
 
Mabadiliko makubwa yapi mkuu? Kama watendaji wakuu wrote wa serikali ni wale wale walio kuwa awamu ya 5, makamanda ni wale wale. Tafakali msemo wako kuwa mama kafanya Mabadiliko makubwa. Ukitoa couch lako la kukalia kulia ukaliweka kushoto mwa chum a chako si Mabadiliko makubwa.
Kwangu mimi kubwa kabisa ni UHURU. Watanzania tumekuwa huru zaidi baada ya neema ya Mungu ya tarehe 17.03.2021. Mama "karuhusu" na kukaribisha kukosolewa. Hakuna kesi za uchochezi tena na hata japa JF utaona (kama upo makini) watu Wapo huru zaidi. Hatuogopi tena kesi za uchochezi zisizo na kichwa wala miguu.

Mama "anafungua" nchi pia. Jiulize ilifungwa?...na ilifungwa na nani?

Kama huoni mabadiliko yaliyofanyika na yanayofanyika au huoni kama ni makubwa ("fundamental regime change") naheshimu mtizamo wako.

After all, "Samia ni Magufuli na Magufuli ni Samia"..... wacha kazi iendelee!
 
Back
Top Bottom