Waziri Bashe anajisikiaje baada Rais kupiga marufuku chakula kuuzwa nje ya nchi? Ni busara akaachia ngazi

Inategemea
 
yeye.pamoja.na..mama.yake..wanakula.matapishi.yao kwa.sababu.walijifanya.wanajua.sana.kufungua.nchi.waendelee mbona macho.yanawatoka.sasa
Rais hajazuwia kuuza chakula nje we punguani...kaasa wakulima wasiuze nje Bali waliuzie ghala la taifa na watapata Bei nzuri
 
Shida kwenye hayo maghala Kuna shida nyingi sana, mpaka upate nafasi ya kuuza ni shughuli kweli kweli, unapewa mashariti magumu sana Hadi unashindwa kuuza Kwa Bei ya serikali, nje ya maghala kunakuwa na Jamaa wananunuwa Mazao yanayokataliwa kwenye maghala ya serikali then wao hai wenye tends wanauza ndani. Pia issue ni kuwa serikali haewezi fika Bei eliyo Sokoni muda huu, ingekuwa vizuri serikali ungetoa Bei kubwa zaidi ya Soko la Sasa Eli Kila mkima auzie serikali, umesahau ya wakulima wakorosho yaliyowakuta kipindi kile!! Serikali itoe Bei ya 1000/= Kwa KG uone wakulima watakavyokimbilia kuuzia serikali, Na kazi ya serikali ni kutoa huduma Kwa watu wake, hata wakununua Kwa hiyo Bei 1000/= wao wakaja kuuza Kwa 500/= Kwa watu wake itakuwa imewasadia wananchi wake Kwa kutoa ruzuku Kwa mlaji, inakuwa imemsadia mlaji Kwa kumtolea mzigo wa Bei, kuliko kumkandamiza mkulima
Rais hajazuwia kuuza chakula nje we punguani...kaasa wakulima wasiuze nje Bali waliuzie ghala la taifa na watapata Bei nzuri
 
Yaani huwa mnapenda kula hela ya serikali tu, yaani inunue buku ije iuze jero! Kwa Tani laki tano!? Hapo kodi mnakwepa, tozo hamtaki
 
Halafu mtu mwendawazimu mmoja analalamika wakenya kuja kununua shambani! Halafu huyo huyo mtu anataka mkulima auze soko la ndani linalo involve madalali kwa asilimia 90 halafu analalamika tena anasema wanaofaidika ni madalali na sio mkulim, hizi ni akili?

Mkulima sio taahira, auze anapoona panampa tija, period!
 
Halafu mtu anakwambia mfumo wa soko huria haumnufaishi mkulima!
 
Tuwache Demand na Supply viamue Bei ya Mazao yetu, kama mahitaji yetu ya Chakula makubwa kuliko uzalishaji basi tuongeze uzalishaji Kwa kuongeza mazingira Rafiki Kwa mkulima Eli aweze kuzalisha Kwa wengi,
 
Watu ni wajinga sana humu ukikaa na kuangalia wanachoandika, gharama ya kulima mpaka kuivisha si ndogo, ni gharama kubwa ukizingatia inflation kwenye bidhaa za mbolea, mbegu, viwatilifu /dawa , posho za wafanyakazi na mafuta ya diesel Kwa ajili ya matrekta kwa ajili ya kulimia hata dawa za kuhifadhia, gharama za kuchambua + kupack na kusafirisha hicho chakula,
Watu hawajui wanachoandika humu, mtu anaandika upotoro mpaka wewe unaona aibu, watu waende tu hapo singida na manyara waone wakulima wanavyoumizwa na maamuzi ya kijinga kama haya
 
Mwaka Jana Bei ya Alizeti elifika 90,000/= ghafla serikali ikaruhusu Wenye viwanda vya Mafuta waengizi Malighafi za kuzalishia Mafuta ya kula, Bei ikadondoka Hadi kufikia Tshs 60,000/= Kwa Sasa Hii Alizeti ya mwaka huu ikiwa tayari itauzwa Kwa Bei ya chini ya 50,000/= mkulima aliyetumia gharama kubwa Kulima Kwa kuangalia Bei ya Soko la mwaka Jana, Mwaka huu2023 ameumizwa vibaya sana, Unapoongelea Wakulima lazima ujue changamoto zao, na jinsi wanavyoumia huko mashambani na kukuta Mazao Yao Bei zipo chini
 
Waziri Bashe anatakiwa aweke nguvu kufufua na kuimarisha vyama vya ushirika, hapo wakulima wa chini watafaidika, na ataweza kuwa na control na mfumuko wa bei.
Vyama vya ushirika hivi vilivyoua kilimo cha mazao ya biashara yote nchi hii na kunemesha matumbo ya viongozi wa hivyo vyama? Hivi huwa mnajua mnachoandika au?
 
Kitu nilichokuja kugundua Watu wengi ni empty Sana kwenye hii field ya kilimo na hata basic idea Tu ya jinsi uchumi wa kilimo unavyofanyika nchi hii. Ndio maana wanaandika ujinga humu.
 
Vyama vya ushirika hivi vilivyoua kilimo cha mazao ya biashara yote nchi hii na kunemesha matumbo ya viongozi wa hivyo vyama ? ,hivi huwa mnajua mnachoandika au ?
Naelewa Mkuu, mfumo wa ufanyaji kazi wa vyama vya ushirika una manufaa, ukiboreshwa na kusimamiwa ulete faida. Viongozi wengi kuanzia ngazi za juu wanajaza matumbo yao. Au tuuze nchi kwa Dp watuendeshee?
 
Unaposema serikali itanunuwa Tani laki tano, Wilaya Moja tu ya KITETO inatarajiwa kuvuna Tani 174000 za Alizeti Kwa msimu huu, Mahindi zaidi ya Tani laki mbili, Bado mkoa wa Songwe, Rukwa, Songea, Mbeya , Iringa, Njombe, Wilaya Kondoa, Kongwa, Mpwawa, Tabora. Jee serikali ukimaliza kununua hizo Tani laki Tano zake, Hizo Tani Milioni Kaza zinzobaki zitauzwa wapi? Ukifunga mipaka?
 
Kujiuzulu sio utaratib wa CCM!! Labda alazimishwe lkn personally never ever ever ever ever!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…