Waziri Bashe anajisikiaje baada Rais kupiga marufuku chakula kuuzwa nje ya nchi? Ni busara akaachia ngazi

Waziri Bashe anajisikiaje baada Rais kupiga marufuku chakula kuuzwa nje ya nchi? Ni busara akaachia ngazi

Huko Buchosa, mwaka jana wakati msimu wa kulima mpunga umefika bro wangu mmoja alikuwa anakopesha wakulima pesa kwaajili ya kuendeshea kilimo (40000 kwa gunia moja wakivuna), alikuwa anafatwa yeye tena kwa kubebembelezwa ili awakopeshe, kwa mkataba kupitia ofisi za serikali ya kijiji.

Muda wa mavuno umewadia bei ya gunia sokoni ikaanzia 70000 na mpaka sasa imepanda maradufu yeye kazi yake ikawa ni kukusanya magunia tu. Yani katengeneza faida 30000 Tsh hata kabla hajaenda sokoni, halafu kuna raia zinaleta story za mkulima kufanikiwa?

WAKULIMA WENGI HUUZIA MAZAO SHAMBANI, kwahiyo mfanyabiashara ndio mnufaika siku zote.
Inategemea
 
yeye.pamoja.na..mama.yake..wanakula.matapishi.yao kwa.sababu.walijifanya.wanajua.sana.kufungua.nchi.waendelee mbona macho.yanawatoka.sasa
Rais hajazuwia kuuza chakula nje we punguani...kaasa wakulima wasiuze nje Bali waliuzie ghala la taifa na watapata Bei nzuri
 
Shida kwenye hayo maghala Kuna shida nyingi sana, mpaka upate nafasi ya kuuza ni shughuli kweli kweli, unapewa mashariti magumu sana Hadi unashindwa kuuza Kwa Bei ya serikali, nje ya maghala kunakuwa na Jamaa wananunuwa Mazao yanayokataliwa kwenye maghala ya serikali then wao hai wenye tends wanauza ndani. Pia issue ni kuwa serikali haewezi fika Bei eliyo Sokoni muda huu, ingekuwa vizuri serikali ungetoa Bei kubwa zaidi ya Soko la Sasa Eli Kila mkima auzie serikali, umesahau ya wakulima wakorosho yaliyowakuta kipindi kile!! Serikali itoe Bei ya 1000/= Kwa KG uone wakulima watakavyokimbilia kuuzia serikali, Na kazi ya serikali ni kutoa huduma Kwa watu wake, hata wakununua Kwa hiyo Bei 1000/= wao wakaja kuuza Kwa 500/= Kwa watu wake itakuwa imewasadia wananchi wake Kwa kutoa ruzuku Kwa mlaji, inakuwa imemsadia mlaji Kwa kumtolea mzigo wa Bei, kuliko kumkandamiza mkulima
Rais hajazuwia kuuza chakula nje we punguani...kaasa wakulima wasiuze nje Bali waliuzie ghala la taifa na watapata Bei nzuri
 
Shida kwenye hayo maghala Kuna shida nyingi sana, mpaka upate nafasi ya kuuza ni shughuli kweli kweli, unapewa mashariti magumu sana Hadi unashindwa kuuza Kwa Bei ya serikali, nje ya maghala kunakuwa na Jamaa wananunuwa Mazao yanayokataliwa kwenye maghala ya serikali then wao hai wenye tends wanauza ndani. Pia issue ni kuwa serikali haewezi fika Bei eliyo Sokoni muda huu, ingekuwa vizuri serikali ungetoa Bei kubwa zaidi ya Soko la Sasa Eli Kila mkima auzie serikali, umesahau ya wakulima wakorosho yaliyowakuta kipindi kile!! Serikali itoe Bei ya 1000/= Kwa KG uone wakulima watakavyokimbilia kuuzia serikali, Na kazi ya serikali ni kutoa huduma Kwa watu wake, hata wakununua Kwa hiyo Bei 1000/= wao wakaja kuuza Kwa 500/= Kwa watu wake itakuwa imewasadia wananchi wake Kwa kutoa ruzuku Kwa mlaji, inakuwa imemsadia mlaji Kwa kumtolea mzigo wa Bei, kuliko kumkandamiza mkulima
Yaani huwa mnapenda kula hela ya serikali tu, yaani inunue buku ije iuze jero! Kwa Tani laki tano!? Hapo kodi mnakwepa, tozo hamtaki
 
Bashe ni shujaa wa kupigiwa mfano, hukijui kilimo ndiyo maana unaongea hivyo, Mkulima wa Tanzania anahangaika sana kuwalisha wanaostarehe mjini halafu wanataka wapewe bure, ingia shambani ukalime mazao yako uone kama utarudi tena.
Wazo la Bashe ni wazo la kimapinduzi huwezi kulima kama hupati faida, Vivyohivyo huwezi kwenda kazini kama hupati ujira. swala la bei ni sambamba ni gharama za uzalishaji na tija, kilimo chetu kimetelekezwa hivyo gharama zauzalishaji ni kubwa sana na bei za kuuza lazima ziwe juu ilikuleta tija, hivyo basi saizi ya chakula chetu ni hicho kinachotoka njee ambacho gharama zake za uzalishaji zinalingana na soko letu.

Kwakuruhusu tu watu wauze njee Mashamba mengi mnoo yamefunguliwa kwenye kilimo cha mahindi msimu huo unaopita, jambo ambalo lingeongeza uzalishaji hasa ukizingatia watu wenye mitaji mikubwa wameingia shambani jambo ambalo ni nzuri, uwekezaji kama huu ukiendelea kufanyika gharama zitapungua na tija itaongezeka, wakulima wakubwa wanakuja na teknologia ambazo hupunguza gharama kwa mkulima wa kawaida.

Hukuna namna tutakifungua kilimo bila soko la njee, hili la ndani ni la kuwanyonya wakulima. Penginepo serikali ikubali kumfidia mkulima ili tija iongezeke.
Halafu mtu mwendawazimu mmoja analalamika wakenya kuja kununua shambani! Halafu huyo huyo mtu anataka mkulima auze soko la ndani linalo involve madalali kwa asilimia 90 halafu analalamika tena anasema wanaofaidika ni madalali na sio mkulim, hizi ni akili?

Mkulima sio taahira, auze anapoona panampa tija, period!
 
Hivi mkulima akiuza Gunia lake la Mahindi Tshs 85000/ Hadi Tshs 90,009/ Sio Faida hiyo Kwa mkulima? Umesikia kuwa serikali itanunuwa Mahindi kupitia NFRA na CPB jee unajuwa hao Bei zao huwa ni kiasi Gani Kwa Gunia? Hao NFRA na CPB wakununua Bei kubwa sana itakuwa ni 50,000/ Kwa Gunia hapo Bado usumbufu wa kuamvuwa moisture ni 15, Mahindi machafu, , Wanaopewa tends ni matajiri wao wananuwa then ndio wanapeleka NFRA ila mkulima hawezi uza direct Kwa serikali mfano angalia pale Njia panda ya kapele mkoa wa Songwe wilaya ya momba ama Engusero Kwa wilaya KITETO ndio utajuwa kuwa mkulima anapata mateso
Halafu mtu anakwambia mfumo wa soko huria haumnufaishi mkulima!
 
Tuwache Demand na Supply viamue Bei ya Mazao yetu, kama mahitaji yetu ya Chakula makubwa kuliko uzalishaji basi tuongeze uzalishaji Kwa kuongeza mazingira Rafiki Kwa mkulima Eli aweze kuzalisha Kwa wengi,
 
Kuna wakulima wengi Kwa Hali ya mazao mwaka huu wanaokwenda kukata mitaji kama hawatapata SoMo la uhakika litakaliwasadia kurudisha gharama zao za kilimo , wamelima Kwa gharama kubwa Hali ya mavuno wanakataa mitaji mfano mwengine Kuna Bwana Moja Anaitwa Abdi pale pori namba moja amelima zaidi ya ekari 500 Kwa gharama zaidi ya Milioni 100, unazani Kwa hali ya mwaka huu anaweza kurudisha gharama zake kama hatopata Bei nzuri. Mwingine Tyson anayelimia Ngabolo ametumia zaidi ya Milioni 35, na Mahindi hawezi kuzidi Gunia 400 unafikiria anahitaji apate Bei gani Eli awezi kurudisha gharama zake?
Mfano mwingine Kuna Bwana Mwengi Anaitwa Abdilahi yeye ametumia zaidi 35milioni kwenye mashamba take huko lekumashi , unadhani nayeye ni rahisi kurudisha gharama zake?
Watu ni wajinga sana humu ukikaa na kuangalia wanachoandika, gharama ya kulima mpaka kuivisha si ndogo, ni gharama kubwa ukizingatia inflation kwenye bidhaa za mbolea, mbegu, viwatilifu /dawa , posho za wafanyakazi na mafuta ya diesel Kwa ajili ya matrekta kwa ajili ya kulimia hata dawa za kuhifadhia, gharama za kuchambua + kupack na kusafirisha hicho chakula,
Watu hawajui wanachoandika humu, mtu anaandika upotoro mpaka wewe unaona aibu, watu waende tu hapo singida na manyara waone wakulima wanavyoumizwa na maamuzi ya kijinga kama haya
 
Mwaka Jana Bei ya Alizeti elifika 90,000/= ghafla serikali ikaruhusu Wenye viwanda vya Mafuta waengizi Malighafi za kuzalishia Mafuta ya kula, Bei ikadondoka Hadi kufikia Tshs 60,000/= Kwa Sasa Hii Alizeti ya mwaka huu ikiwa tayari itauzwa Kwa Bei ya chini ya 50,000/= mkulima aliyetumia gharama kubwa Kulima Kwa kuangalia Bei ya Soko la mwaka Jana, Mwaka huu2023 ameumizwa vibaya sana, Unapoongelea Wakulima lazima ujue changamoto zao, na jinsi wanavyoumia huko mashambani na kukuta Mazao Yao Bei zipo chini
 
Waziri Bashe anatakiwa aweke nguvu kufufua na kuimarisha vyama vya ushirika, hapo wakulima wa chini watafaidika, na ataweza kuwa na control na mfumuko wa bei.
Vyama vya ushirika hivi vilivyoua kilimo cha mazao ya biashara yote nchi hii na kunemesha matumbo ya viongozi wa hivyo vyama? Hivi huwa mnajua mnachoandika au?
 
Unazani wakulima wamevuna kiasi Gani Kwa ekari Kwa kilimo Cha nchii maeneo ya KITETO? Watu wanalima ekari 500 Bado wanadhindwa kupata Gunia hara 800 ukigawa hapo nisawa Gunia ngapi Kwa ekari? Unaweza kukuta hata Mama yako hajawahi Kulima halafu unaleta ukenge humu jukwaani, Uliza watu waliolima maeneo ya Hemba Hemba, ngomai, makawa, matongolo, mkoka, chetego, magungu, Lugine, Kirashi, maliti, mbande, mbiri, pori namba moja, londoni, lekyimashi, Ngabolo, Matui, Engusero, osteti, seringine, njoro, nailelo, msada, chekanao, kiperesa, mrijo, Zajirwa, kazi ngumu, irela, langitomoni, njia panda, twanga, wizamtima, isiza.Tembelea hayo maeneo uone watu wanavyopata kwenye ekari Moja ya mahindi! Acha kywa kiazi tumia akili jaribu kufanya utafiti.
Kitu nilichokuja kugundua Watu wengi ni empty Sana kwenye hii field ya kilimo na hata basic idea Tu ya jinsi uchumi wa kilimo unavyofanyika nchi hii. Ndio maana wanaandika ujinga humu.
 
Vyama vya ushirika hivi vilivyoua kilimo cha mazao ya biashara yote nchi hii na kunemesha matumbo ya viongozi wa hivyo vyama ? ,hivi huwa mnajua mnachoandika au ?
Naelewa Mkuu, mfumo wa ufanyaji kazi wa vyama vya ushirika una manufaa, ukiboreshwa na kusimamiwa ulete faida. Viongozi wengi kuanzia ngazi za juu wanajaza matumbo yao. Au tuuze nchi kwa Dp watuendeshee?
 
Unaposema serikali itanunuwa Tani laki tano, Wilaya Moja tu ya KITETO inatarajiwa kuvuna Tani 174000 za Alizeti Kwa msimu huu, Mahindi zaidi ya Tani laki mbili, Bado mkoa wa Songwe, Rukwa, Songea, Mbeya , Iringa, Njombe, Wilaya Kondoa, Kongwa, Mpwawa, Tabora. Jee serikali ukimaliza kununua hizo Tani laki Tano zake, Hizo Tani Milioni Kaza zinzobaki zitauzwa wapi? Ukifunga mipaka?
 
Waziri wa kilimo mwaka jana alikomalia kuuza chakula nje ya nchi. Kitendo hicho kililalamikiwa sana kusababisha bei ya vyakula nchini kupanda zaidi ya maradufu, lakini waziri huyu alikomalia jambo hilo akitoa sababu eti anawatajirisha wakulima, wakati ukweli ni kuwa alikuwa akiwatajirisha wafanya biashara wenzake (middle men) na makangomba.

Alisikika akiapa kuwa katika utawala wake kamwe hatakubali kuzuia wakulima kuuza chakula nje ya nchi. Alisema piga ua hatakubali kwenye kipindi chake cha uwaziri. Tulishuhudia raia wa nchi za nje wakienea kwenye vijiji vyetu wakinunua mchele, mahindi, maharage na kadhalika hadi yaliyokuwa bado yako shambani.

Tulishuhudia maelfu ya ma semi trela yaliyosheneni vyakula kila siku yakipeleka chakula hicho nchini Kenya hadi Somalia. Bei ya vyakula huko Kenya ikawa nafuu sana ukilinganisha na huku kwetu ambako ambako bei zilipaa kwa zaidi ya 150%. Watanzania walio wengi wakawa hawa uwezo wa kupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku.

Ikafika wakati nchi yetu ikawa na upungufu mkubwa wa chakula hadi ikabidi ianze kununua chakula kutoka nchi zingine hususani Zambia kwa kutumia akiba yetu ya pesa za kigeni (USD) na kusababisha uhaba mkubwa wa pesa hizo huko BoT hadi sasa. Hivyo wafanyabiashara wa bidhaa zingine zinazotoka nje ya nchi wakawa wanakosa pesa (USD) za kuagizia bidhaa hizo.

Baada ya agizo hilo la leo kutoka kwa Rais Samia kupiga marufuku uuzaji vyakula nje ya nchi, huyu waziri wa kilimo anapaswa kujitathmini na kuachia ngazi kama alivyotuapia katika utawala wake.




Kujiuzulu sio utaratib wa CCM!! Labda alazimishwe lkn personally never ever ever ever ever!!!
 
Back
Top Bottom