Waziri gani alimdhulumu Rais mstaafu Mwinyi vifaa vyake vya ujenzi?

kuna mambo mengi sana Mzee mwinyi ameyaandika katika kitabu chake. ni vyema ukapata nakala yako ukajisomea kwa undani zaidi.
Lkn kwa mujibu wa muhtasari ulio somwa na Prof. Mkandala ni kwamba Mzee Riuksa ktk safari yake ya maisha ya uongozi amekumbana na changamoto nyingi sana tena panda kichwa, mfano;

1. changamoto za kibaguzi kuhusu dini yake, kuhu asili yake.

2. changamoto za kiuchumi, baada ya kupokea kijiti kutoka kwa Hayati mwalimu JK alikuta hali ya kiuchumi ni mbaya sana isiyo elezeka, alifanya jitihada za kuifungua nchi na mambo yakaanza kuwa mazuri lkn aliaanza kupigwa fitina kali kuwa amekumbatia ubeberu badala ya ujamaa , n.k,
alipata changamoto ya uchochezi wa kidini ambao ulisimamiwa na kuenezwa na Rev.Mtikila ambaye kwa maksudi na chuki alieneza chuki za kidini ambayo ilimpa taabu sana mzee Ruksa kuendesha nchi.

ilichochewa Migomo ya wanafunzi na maandamano n.k n.k

Alifanyiwa figisu na fitina mpaka aliamua kujiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani n.k.

alipigwa fitina na Jungu mpaka akashindwa kuwa mwenyekiti wa CCM taifa.
n.k nk.

Kama mambo haya bado yapo ni bora tuyaache mara moja kwani haya tija kwa taifa letu. lkn pia ni vyema viongozi wetu wakafahamu ni wapi walikosea mpaka hali hii ikakomaa, inaonekana kuna tatizo mahala, nalo linafaa lirekebishwe ili kunusuru umoja wa taifa letu.
 

Umesoma kitabu chake chote? Wapi alisema alibaguliwa dini yake?
 
Ni mzanzibari hivi. Jina limenitoka
Late Major General Abdalah Natepe
Hassan Nassoro Moyo
Alikuwa Lowassa. Nadhani na yeye atakuja kujibu akitoa kitabu chake mwaka mmoja kabla hjasafiri!
Au ni Ameir?
Hassan nasoro Moyo.
Ahsante sana bwashee!
Alikuwa Hassan Nasoro Moyo
Jackson M Makweta
 
Abdalah Said Natepe, tena Mzanzibari mwenzie!!!

Sent from my itel A32F using JamiiForums mobile app
 
Amemtaja aliedhulumu ni Jackaon Makweta daaa ni dhambi na aibu kubwa baada miaka mingi udhalimu unajulikana pia alimwambia nenda zako Zbar huko....kama dharau na ubaguzi....Mzee ameandika kitabu chake
 
Mbona hayo yalishawahi kuandikwa humu kitambo! Pia kama unasema yalipata kutu kwanini baada ya mwinyi kuwa raisi alimpelekea vile vitu? Kumbuka jamaa alimnyima mwinyi akimwambia ni mali ya serikali
 
Kuna mdau kaandika mahali mambo fulani nimeyakopi kama yalivyo hapo chini.


Mmmh!
Ukikosa ku-peruse ukurasa wako wa mtandao kwa saa 12 tu,unakuwa umeachwa nyuma masafa.
Sikuwapo hewani kwa saa 36 hv,usiku huu napitia group hili,nayaokoteza mengi.
Hili la Mhe.J.M.Makwetta,limenigusa.
Asante kwa analysis hii ndg yetu.
Nami niseme tu,nilimfahamu Jackson (Mungu airehemu roho yake) enzi anasoma sekondari A level-1960s,nikiwa nasoma Lupembe Primary School.
Aliwahi kuwa anakuja kutufundisha darasani kwa wakubwa wetu madarasa ya V,VI&VII,anapokuwa likizo.
Lakini kwangu na kwetu wa familia za Aron B.Swalle,Mzee Francis M.Hongoli Lupembe,Mzee Godfrey M.Hongoli Lupembe - Jackson alikuwaga mgeni wetu mara nyingi.
Alikuwa akija kuonana na wazee wale mara kadhaa,hasa akiwa masomoni Chuo kikuu na alipoanza kufundisha IDM Mzumbe.
Ikumbukwe,Jackson alikuwa shemeji yake Mzee Francis kwa Shangazi Munyawvolofu,hivyo automatically kuwa ndg wa akina Hongoli na uzao wao.
Lkn pia,Jackson alikuwa rafiki,wa kiwango tofauti cha ukaribu na wasomi wa mwanzo wa Kanikelele akina:August P.Mpolo,Metusala S.Sasami,John A.B.Swalle (Nyalusi).
The man was humble ambaye alikuja kuwa model wangu.
Jamani,niliwahi kudokeza huko nyuma kuwa,
KWA CHOCHOTE KITAKACHOSEMWA JUU YA HISTORIA YA LUPEMBE aka KWAVISU,JOHN AaRON MHAVILE aka MUNYILEMBULA aka Baba Joyce,na
JACKSON M.MAKWETTA aka Munyamtwango, ni wabunge wa kupigiwa mfano.
One can write volumes kuwahusu wanasiasa hao.
Time will tell.Tuombe Mungu.
Mhavile alijenga uchumi na misingi ya elimu kwa kujenga misingi ya ushirika (akiwa ameazimwa na wazee akina Mbanga,purposely kwa kazi hiyo,maana alikuwa msomi wa Std.X)
Lupembe Farmers' Cooperative Union,kika-boost kilimo cha Pareto,Kahawa na Chai.
I can humbly argue here kwamba TURNING POINT YA MAENDELEO YA KWAVISU,NI PARETO,KAHAWA,NA CHAI.
Baadae Chai,ilileta HYBRID 614,i.e.In stand to be corrected,zao lililotutoa kutoka kutegemea wvuledzi,mayao na sweda kwa chakula,kuwa A FOOD SECURED LUPEMBE.
Jackson alikuja kuanzia alipokuwa ameishia Mhavile.
Akipokea kijiti toka kwa Mwl.Sapali,Jackson alianza na ELIMU.
Aliiga approach ya wenzetu wa Kilimanjaro kwa kuunganisha nguvu za wananchi na kwa kutumia NDDT,tukaanza kujenga sekondari kwenye kila tarafa.
Ikumbukwe kuwa,ni Makwetta,aliyemwambukiza J.J.Mungai,wazo la sekondari za jamii nae akajiongeza kwa kujenga shule za kata kwa kupitia MET kule Mufindi.
Mchokozi hapa,nitofautiane na hoja na:4.
Pamoja kwamba Jackson Makwetta alimfundisha Anne Semamba Makinda kule IDM,
Njia ya Anne kiutumishi hasa ktk siasa,haikumtemea Jackson.
Jackson hakuwa mwanasiasa in the real meaning of it.
Jackson was purely academic,professional and pragmatic technocratic.
Aliingia ktk ulingo wa siasa,just by virtue kwamba mfumo wetu wa utawala unatulazimisha tutumie ulingo wa siasa kufikia malengo ya kuingia kwenye timu za kuongoza wengine.
Ikumbukwe,Anne aliingia ktk siasa,akiwa kiongozi wa kitaifa wa TYL,tangu akiwa chuoni IDM Mzumbe.
Na waliingia bungeni pamoja na Jackson mwaka 1975,Anne akiwa anatokea TYL.
i.e.kwa msiofahamu TYL ni TANU YOUTH LEAGUE,sawa kwa mbaali na UV-CcM.
Wkt Jackson hakuwa kuwa kwenye top-clique ya Chama,Anne ameogelea humo tangu akiwa kinda mwali.
Anne ni mjumbe wa NEC-CcM, hata kabla ya Mzee Mkapa (RiP) na Dr.Kikwete.
Hata Mzee Rukhsa nadhani.
Nakumbuka kwenye uchaguzi mkuu wa chama 1982 tukiwa pale Diamond Jubilee,BwM aliangukia pua kuingia NEC,Anne na JK walipeta kupitia UVCcM.
Halikadhalika kwenye MM wa kihistoria wa CcM kule Kizota 1987,Mzee Mkapa aliambulia patupu ktk kinyang'anyiro kuwa m-NEC,Anne aliibuka kidedea.
JK (akigombea kwa mara ya kwanza kupitia Kapu Kuu) aliibuka mshindi wa tatu,nyuma ya Kingunge na Nnauye Moses - vinara wa propaganda hao.
Miaka yote ya utumishi wake Jackson M.Makwetta,hakuwahi kutafuta durectly nafasi ya uongozi ktk chama.
Ninakaribia kuhitisha kuisoma Biography ya Mzee Rukhsa.
Waliomshauri aingize hiyo sintofahamu yake kwa Jackson,wamebughi.
Sawa,ameandika hilo ili kuonesha kuwa yeye si mtu wa visasi.
Ila wewe binafsi jiulize na kujijibu ktk moyo na roho yako,
NAFSI YAKO HAINA ELEMENT ZA KISASI KABISAAAAAA?
Kama ni HAPANA,hizo elements chache ulizo nazo,(i.e.jambo ambalo si dhambi maana umelipokea kwa uumbaji) HUWA UNAZITUMIAJE NA KWA NANI?
Ni bahati mbaya,Jackson hawezi kuinuka amjibu Mzee Rukhsa,naamini hata angeweza,the best he could have done Jackson niliyemfahamu,angemnyamazia.
Zaidi zaidi hata Mzee Rukhsa na waliomsaidia kuiandaa bio yake wasingeliingiza kumbukumbu hiyo kabisa.
In short,Mzee Rukhsa alilipiza kisasi kwa Jackson.
Again,TIME WILL TELL.
Ndugu zangu,kwa tuliomfahamu Marehemu Jackson M.Makwetta,hicho tunasoma kwenye bio ya Mzee Rukhsa kumhusu,HAKITUSHANGAZI.
Jackson was PURELY HUMBLE,FIRM N A FACTUAL TRUTH-TELLER.
Jackson alikuwa muwazi na asiyepindisha wala kukawiza jambo.Ndio kisa akawa kipenzi cha mabosi wake kuanzia:Sokoine 1977,Msuya,Salimu,Warioba,Malecela na Msuya tena.
Unapaswa uwe ulimfahamu ama kwa kufanya naye kazi au hata kwa kusimuliwa tu na waliokuwa naye karibu,ndio unielewe nisemacho.
Historia ya Mzee Mwinyi kuingia ikulu,ilijaa makandokando,hata kama hayalingani,kama tuliyoshuhudia kwa safari za wengine pia.
Asituaminishe kuwa alipita njia nyoofu na nyororo.
Yapo mengi under-cover ya kutosha volumes zingine hata tano usawa wa bio hii.

Surfice by saying,HISTORIA NI ZANA MUHIMU KWA KILA MWENYE NIA NA MALENGO THABITI YA KULETA MAENDELEO ENDELEVU YAKE NA YA JAMII YAKE.
To me JACKSON M.MAKWETTA STANDS TO BE ONE AMONGST MY BEST MODELS.

MUNGU AIREHEMU ROHO YA MPENDWA JMM.

Ahsanteni sana.

Credit kwa Gideon Swale (Kiwopambuli
 
Mbona hayo yalishawahi kuandikwa humu kitambo! Pia kama unasema yalipata kutu kwanini baada ya mwinyi kuwa raisi alimpelekea vile vitu? Kumbuka jamaa alimnyima mwinyi akimwambia ni mali ya serikali
Alimnyima vitu vyake kivipiii ??

Waziri mpya hakuwepo hapo nyumbani siku Mwinyi anaondoka.

Kwa nini Mwinyi hakuondoka na nguo zake na watoto wake na mabati yake na masimenti yake ?

Na Mwinyi hakufukuzwa kazi, hakuondoka ghafla, alipanga siku ya kujiuzulu, na alijua mapema kwamba anaondoka nyumba ya serikali.

Muungwana huwezi kuacha mazaga zaga yako kwenye nyumba ya mtu! Ndo maana wanasema "mwenye chake muungwana." Hasumbui wengine kumtunzia mazaga zaga yake kwa sababu ana kwake.
.
 
Haya mambo yanajulikana zaidi ya miongo miwili iliyopita, hivyo kumbukumbu unayotaka kusema haipo sasa ilikuwepo.
 
Jackson kama ulivyoeleza ni kweli alileta maendeleo huko kwenu na unaweza kusema alikuwa kiongozi mzuri pure technocrat na sio mwana siasa , lakini hili suala la yeye kutaka nyumba kwa haraka na kuchukua hivyo vifaa linafahamika zaidi ya miaka 20 iliyopita
 
Haya mambo yanajulikana zaidi ya miongo miwili iliyopita, hivyo kumbukumbu unayotaka kusema haipo sasa ilikuwepo.
Okay, aliyasema 20 years ago. With fresh memory and faculties.

Back then alisemaje, alisema aliona ni uungwana kumuachia mtu mabati na masimenti akutunzie wakati yeye mwenyewe ndio alipanga siku ya kuondoka?
 

Asee umedadavua vyema
 
..but this is petty.

..hivi kulikuwa na haja ya kuandika haya kwenye kitabu chake?
It is not petty. Anataka wanasiasa vijana wajifunze kujishusha na kutolipiza visasi.

Kumbuka kuwa alipokuwa rais alikuwa anamuapisha huyo huyo aliyemfanyia unyama akiwa amesimama mbele yake akiahidi utii kwa rais.

Ni lazima huyo aliyefanya ubaya alikuwa na unyonge mwingi wakati wa kiapo na wakati wa kupokea maagizo.

Wanasiasa wengi wa afrika hawana uwezo wa kujishusha, wanajawa na kile kiburi cha elimu kinachochanganyika na ushauri mbovu wa wapambe wanaoshauri ubaya ufanyike ili waendelee kuutunza ukaribu wao na bosi wa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…