Waziri gani alimdhulumu Rais mstaafu Mwinyi vifaa vyake vya ujenzi?

Okay, aliyasema 20 years ago. With fresh memory and faculties.

Back then alisemaje, alisema aliona ni uungwana kumuachia mtu mabati na masimenti akutunzie wakati yeye mwenyewe ndio alipanga siku ya kuondoka?
Hivi akili yako ipo sawa?? Huja soma kwamba ali pata msukumumo wa kutakiwa kuondoka ili yeye aingie kwenye hiyo nyumba , Na arudi kwao ZnZ .
Na huja soma baadae muhusika alimpelekea mabati na cement alivyokuwa "white house"
 
Mbona kitabu kinasema Jackson Makwetta?
 
Mzee Mwinyi alivyorudi kivingine na kuwa rais,yule waziri alitetemeka kichiz. Ajabu mzee akamteua tena kwenye baraza lake. Siku ya kuwaapisha mawaziri,akamwambia nimekuteua sijaangalia mambo yako binafsi nimeangalia utendaji wako serikalini. Baada ya siku kadhaa mbele yule waziri akamletea mzee bati roli zima. Mzee akamjibu kama umeamua kurudisha nataka mabati yangu 200 tu na si zaidi. Ikiwezekana kama yatakuwa ni yale yale nitafurahi sana. “kuna la kujifunza hapo”.
 
Nimekuelewa bwashee!
 
Wapunguze bei ya kitabu.. kutoka 70,000 wauze hata 30,000 ili wanunue watu wengi au hawajui Biashara?
 
Kawaida ya watu wenye roho za kimaskini ni kudhulumu kwa kudhani ndio njia nyepesi ya kujikwamua!! Na watu wenye mioyo iliyoridhika huwa hawajali "fukara anayeogopa umaskini" anapowadhulumu bali wao humshukuru Muumba.
 
Kwa maelezo yaliyosomwa na Prof. Mkandara, ni sahihi kusema pasi na shaka wala kumvunjia heshima, kwamba Mh. Rais Mwinyi alikuwa dhaifu kuliko rais wote katika historia ya nchi yetu!
Haswaa, Kuna tofauti ya uungwana na udhaifu uliokithiri...choose uno.
 
Kumbe alilipwa? Asa mnakunja nn?
 
jamaa nasikia kipindi akiwa waziri aliomba gari kwa mkurugenzi kwa ajili ya shughuli za harusi ya mwanae!jamaa akamtolea nje kimadharau.mungu si hadija ndala ndefu mwisho wa siku akawa prezdaa mbona mkurugenzi hakuna rangi aliacha kuona..jamaa alikuwa alikuwa ana kisasi kinoma he never let go untouched..km gabachori manjis gas alivyomwambia wakati ni wazir kwamba mimi hapana ongea na mbwa mi iko ongea na yenye mbwa!!kitu alifanywa hatakaa asahau maisha yake
 
Kwa maelezo yaliyosomwa na Prof. Mkandara, ni sahihi kusema pasi na shaka wala kumvunjia heshima, kwamba Mh. Rais Mwinyi alikuwa dhaifu kuliko rais wote katika historia ya nchi yetu!
Umekuwa mwepesi sana kutoa hukumu kwa vile labda ulikuwa hujazaliwa kipindi hicho. Mzee Mwinyi alipokea nchi hii ikiwa hoiiii bin taaban! Yaani aliachiwa fremu tu ya nchi. Hata ukitaka sabuni ya mawingu ya kufulia ilikuwa lazima upange foleni, kwa waliokuwa vijijini ile mifuko ya kitambaa (kikiitwa Marekani) iliyokuwa ikija na mchele na unga ndiyo mavazi, redio ya mkulima ndiyo ilikuwa ya maana, eti kuwa na televisheni au friji ulikuwa mlanguzi, heeeee!

Umewahi kuisikia 'redio kiroboto' iliyokuwa ikieleza kwa kificho jinsi nchi ilivyokuwa ikipata shida kwa kukosa mahitaji muhimu? Mbali ya kutukanwa na kushambuliwa na Nyerere na wengine hadharani Mzee Mwinyi alikuwa mvumilivu na hakuwahi kumjibu hata siku moja.

Umewahi kusikia vijana waliowahi kuteka nyara ndege ili angalau kujikwamua katika hali ngumu iliyokuwepo? Wale walikuwa desperate yaani (siyo kwamba naona ni vyema). Ilikuwa safari nje ya nchi lazima upate kibali cha Ikulu na Income tax ndiyo upatiwe tiketi.

Mzee Mwinyi hii nchi aliitoa mbali sana ambao nyinyi kwa sasa munaona ni vitu vya kawaida. Yeye kama binaadamu hakuwa mkamilifu na alifanya makosa kadhaa lakini kwa kweli aliyofanya mema ni mengi kuliko hayo mapungufu.

Lakini sisi binaadamu hatuna shukurani hata tukifanyiwa wema vipi bado baya moja litakuwa na nguvu zaidi kuliko yale mengine.
 

Nadhani ni wewe ndiyo kujafanya uchambuzi sahihi na umerukia tu.

Hebu kasome vizuri ile note ya zamani iliyoletwa na mmoja wa members humu. Ameandika kwamba alimeteua kwa vile utendaji wake wa kazi ni mzuri na ile issue ilikuwa ni personal siyo ya kiserikali.
 
Roho ya mwendazake ilijaa kutu za chuki mpk umeme wa pacemaker ukakatika.
Mtu unakuwa na roho mbaya mpaka unatia huruma .yaani wale unao waonea wanakuhurumia wewe duuu!! Hii kali.... Bongo ya ajabu sana.

Kufanya kazi vile usiku na mchana kuuumbe ilikuwa ni roho ya visasi vinamsukuma!!!

Ndo mjifunzie kwa mwenda zake ...uislamu safi sana wadumu hawa watu na ndo Dini ya kweli.
 
Miaka ile ya mwisho mwa uongozi wa Nyerere kuelekea ile ya Mwinyi hapa bongo kulikuwa na umaskini mkubwa sana. Mzee Mwinyi ikabidi akubaliane na masharti ya IMF kama yalivyoletwa.

Ni katika kipindi hicho cha miaka ya 1980 katikati ndio vijana wengi wenye uwezo na elimu waliposafiri kwenda Uingereza, Canada na Marekani. VIjana wenye elimu wakiwa ni watoto wa wazazi wenye nafasi serikalini ndio wakafanya mikakati ya kufanya mitihani ya TOEFL ili wapate nafasi za kujiunga na vyuo vikuu vya huko nje.

Hawa wanaoitwa diaspora wengi wao waliondoka nchini kipindi hicho, hali ya uchumi ilikuwa mbaya tukiwa tumetoka kupigana vita ya Kagera, na hazina ya nchi ikiwa tupu.

Hivyo Mzee Mwinyi ni shujaa mwenye kila aina ya haki ya kuenziwa. Wapo wanaojaribu kumdhihaki lakini alichokifanya kwa kutazama mazingira ya wakati ule ni chema kwa ajili ya Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…