Waziri Gwajima afafanua dawa ya asili ya Corona (NIMRCAF), waweza itengeneza mwenyewe nyumbani

Nchi imegeuka kua ya kishirikina, inchi ya wapiga ramli.

Toka lini kachumbari/chachandu ikawa tiba ya magonjwa?

Tufute wizara ya afya maana haina uhumimu, tutymie waganga wa kienyeji na wapiga ramli.
tafuta kitabu kinachoitwa TUREJEE EDENI ujifunze kua matunda na mbogamboga ni dawa kuliko hizo za viwandani au mahospitalini
 
For idiots
huko kwa waja chanjo ya Corona waliyogundua marekani inaua watu hasa

 
We unapayuka tu bila sababu yeyote, components zote za hiyo dawa (Limao, tangawizi, pilipili, kitunguu swaumu) ni vyakula ambavyo havina madhara yeyote unless Kama mtu ana allergy. Kazi ya mchanganyiko wa vyakula hivi ni ku boost kinga ya mwili ili uweze kupambana na maradhi (tiba lishe) Sasa hii inayo inahitaji international accreditation?
 
Asubuhi waziri anatangaza hakuna Corona hapa Tanzania, mchana waziri huyo huyo anazindua dawa ya kutibu Corona huku akiwasisitiza watanzania wainunue kwa wingi ili kuishinda Corona!

Huu ndio uwendawazimu kwa mtu mwenye mtindio wa ubongo.
 
Nini mantiki ya kuitangaza kama dawa ya kutibu Corona?
 
tafuta kitabu kinachoitwa TUREJEE EDENI ujifunze kua matunda na mbogamboga ni dawa kuliko hizo za viwandani au mahospitalini
Unaonaje tukifuta wizara ya afya halafu kila mtu akapewa kitabu cha turejee edeni, kutakua na haja ya kua na wizara ya afya tena ama kutakua na haya ya kua na hospitali? Zote itabidi zifungwe, sio?
 
Mimi nilianza kutengeneza juisi ya matunda ya asili kabisa.

Nachukua Orange, apple, Banana, limau au ndimu nasaga kwa blender na usiweke sukari.

Hii juisi safi sana natural wanywa kila asubuhi.

Hata watoto wawapatia hii, safi sana.

Punguza pombe, achana na sigara na fanya mazoezi na utoke jasho khasa.

Saa nzuri kukimbia ni asubuhi kati ya saa 11 na saa 7 na jioni ni kati ya saa 12 na saa 7 kukiwa kumepoa.

Ila tusisahau kuepuka misongamano isiyo lazima na ikibidi vaa barakoa.

Nawa mikono kwa kutumia maji ya sabuni na osha mikono kwa vitakasa maji.

Watu hawakumwelewa uzuri raisi wetu JPM wanadai amesema hakuna Korona Tanzania.

Lakini hapohapo wanasahau kasema kwamba kuna watu wamekwenda kuchomwa chanjo na wamerudi Tanzania na wameleta ugonjwa.
 
Nchi imegeuka kua ya kishirikina, inchi ya wapiga ramli.

Toka lini kachumbari/chachandu ikawa tiba ya magonjwa?

Tufute wizara ya afya maana haina uhumimu, tutumie waganga wa kienyeji na wapiga ramli.
Hahahahahahahahahahahaa
 
Nimetaja mambo mengine mawili,efficacy na efficiency,hebu nayo yajibu.Mimi napayuka wewe pumbavu kabisa.
 
Wanasanyansi wa kitanzania wa National Institute for Medical Research (NIMR) ndio wamefanya huo utafiti .Huwaamini wanasayansi wetu? Ulitaka wawe wakoloni wazungu waliojaa kichwani kwako ndio wafanye uwaamini?
Weka hapa chapisho la utafiti huo!

Unajisemea tu kama mlevi?
Unajua nini maana ya 'utafiti' hasa unaohusu maswala kama haya?

Mnalipwa kutwa nzima kushinda hapa JF, lakini hata mnapopewa fursa nzuri ya kutoa michango ya maana kuonyesha mazuri yanayofanywa na hao mnaowatetea bado mnabaki mnababaika tu?

Sasa nyinyi faida yenu kwa taifa hili ni nini?
 
Wewe muuwaji, lazima ufunguliwe kesi
 
dose

Kunywa mililita 20 sawa na vijiko vikubwa vya chakula viwili (2) kila baada ya masaa 8.

Kwa ambao tayari ni wagonjwa kunywa hadi utakapo pona

Kwa ambao sio wagonjwa unaweza kutumia kiasi hicho
mara moja au mbili kwa siku kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili.
 
Hii dawa huwa inazinduliwa kila mwaka! Nakumbuka mwaka jana ilizinduliwa tena.
 
Hiyo mbona ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume?yaani Mwamba utasimamia show mwanzo mwisho hadi binti ahisi kunawaka moto
Hahahahaahhahahahahaha yn namsukuru mungu na Mimi kuwepo katika utawala huu Kama mwanasayansi mwenye phd haamini alichokisomea anaamini nyungu
 
Wewe muuwaji, lazima ufunguliwe kesi
Wauaji hawa hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…