DOKEZO Waziri Gwajima, hii anayofanya Lillian Mwasha kwa watoto siyo sawa

DOKEZO Waziri Gwajima, hii anayofanya Lillian Mwasha kwa watoto siyo sawa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hawa wanaoitwa wanaharakati ni watu wa hatari kwa sbb wengi wao ni wale wenye majeraha ya kushindwa kwenye ndoa zao (Hawajapona)

Hapo hao mabinti walitakiwa kupewa tiba, kwa siri na mshauri nasaha na sio mbele za umati wa wenzao. Hapo tatizo jingine la kuto jiamini limeanza. Muda wote ukiona wenzio wamekaa unaona wanakuongelea wewe.

Kuna watu wanabeba laana mbaya kwa kulaumu baba zao bila kujua ya upande wa pili. kuna nyakati mwanaume anaona andoke kuepusha majera, ulemavu na kupoteza maisha kwa wenza wao.
 
Anawauliza watoto wanaochukiwa na baba zao. Je amewaandaa kisaikolojia? Mbona yaonekankama ni udhalilishaji kwa watoto na wazazi wao. Angalia clip hapa

Hbr za usiku, hongera kwa majukumu. Naifungua haifunguki kwangu. Naomba mwenye nayo nitumieni kwenye 0765345777 hiyo video nione tafadhali ndiyo nijue nini tufanye. Ubarikiwe.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Sioni alichokosea
Ifike wakati wababa wawajibike na malezi
Hao wasichana wanahitaji upendo na malezi ya baba zao
Kila huduma ina mwongozo wake na hizi huduma za ustawi nazo ni taaluma. Nia njema isipoenda na itifaki yake, inaweza kugeuka changamoto halafu tena tukaja kuulizana maswali.

Tujengane tu vizuri Ili umoja wetu uwe na tija nzuri kabisa
 
Kwa kigezo kipi anatumia kuhakiki hiyo 'chuki' ikiwa ni mtoto ndio kaulizwa bila ya mzazi husika kuwepo??

Kuwaita mbele ya wenzao ni kuweka suluhisho lolote la kuleta huo upendo?? Kama dhamira ni kumkabili mzazi husika, je anaathirika vipi ikiwa hayupo hapo??

Kwa sehemu kama shule hudhani anatengenezea hao waliojitokeza mbele mazingira ya kuonewa 'bullying' na wenzao kwa kufanyiwa dhihaka ya kutokupendwa na wazazi wao?
Uko sahihi, Na hapa ndiyo ambapo changamoto itaibukia.

Nimempa mtaalamu wa huduma za ustawi wa jamii atuongoze Ili twende salama. Nia njema iende sahihi ili tufanikiwe
 
Kila huduma ina mwongozo wake na hizi huduma za ustawi nazo ni taaluma. Nia njema isipoenda na itifaki yake, inaweza kugeuka changamoto halafu tena tukaja kuulizana maswali. Tujengane tu vzr Ili umoja wetu uwe na tija nzuri kabisa

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Aseeeee
Shukrani mheshimiwa.
Kumbe mnaona.
 
Ni kitu kizuri kumfariji na kumtia moyo mtu, ila hapo si mahali sahihi. Kwa muktadha wa shuleni, wanafunzi wenzio wakijua matatizo yako wanaweza kuyatumia against you mambo yakazidi kuwa magumu kwa mhusika.

Nilipokuwa binti mdogo nilikua namuona Lilian kama mtu mwenye akili sana sababu anajua kuongea/present, baada ya akili zangu kukomaa nimekuja kugundua Lilian ni mpumbavu mmoja mwenye “Audacity” na guts za kudisplay upumbavu hadharani, sorry not sorry.

Bottom line: wanaume jitahidini kuwa kwenye maisha ya watoto mnaoshiriki kuwaleta duniani baada ya ile starehe, hakuna maumivu mabaya kama maumivu ya kukataliwa, ninyi tu mkikataliwa kwenye kutongoza mnakuwa na vinyongo wakati mwingine inakuwa vita kabisa, sembuse mtu aliyekataliwa na aliyemleta duniani? SMH! 🤦🏻‍♀️
 
Imefunguka, nimempa kamishna wa ustawi wa jamii afanyie kazi. Ahsanteni sana kwa ushirikiano.
Mh ikiwezekana ni maombi yetu tafadhali hawa wanaharakati katika engo yoyote wasiwe wanapewa nafasi ya kuzungumza na watoto huko shuleni bila wataamu na miongozo sahihi dhidi ya hayo mazungumzo.

Urahisi wa kujenga kizazi kijacho katika mtazamo hasi katika mambo mengi ni mkubwa mno.

Mtu mwenye maumivu na machungu na majeraha hata kuwa na jema la kuijengea jamii kwa mtazamo ulio kinyume na yalio moyoni mwake. Kuna msemo usemao kinywa cha mtu hunena yaliyo moyoni mwake.

Wakati huu mlio na dhamana ya kusimamia ustawi wa jamii yetu tunaomba mjaliwe hekima ya kusikia kinywa kinachonena majeraha yaliyo jaa moyoni ili mkinyamazishe.
 
Ni kitu kizuri kumfariji na kumtia moyo mtu, ila hapo si mahali sahihi. Kwa muktadha wa shuleni, wanafunzi wenzio wakijua matatizo yako wanaweza kuyatumia against you mambo yakazidi kuwa magumu kwa mhusika.

Nilipokuwa binti mdogo nilikua namuona Lilian kama mtu mwenye akili sana sababu anajua kuongea/present, baada ya akili zangu kukomaa nimekuja kugundua Lilian ni mpumbavu mmoja mwenye “Audacity” na guts za kudisplay upumbavu hadharani, sorry not sorry.

Bottom line: wanaume jitahidini kuwa kwenye maisha ya watoto mnaoshiriki kuwaleta duniani baada ya ile starehe, hakuna maumivu mabaya kama maumivu ya kukataliwa, ninyi tu mkikataliwa kwenye kutongoza mnakuwa na vinyongo wakati mwingine inakuwa vita kabisa, sembuse mtu aliyekataliwa na aliyemleta duniani? SMH! 🤦🏻‍♀️
Its all about Wanaume?
Playing Gender card wont help hapa......
Kwa kuwa umesema kuhusu wanaume nitasema kuhusu wanawake.
Ili yasitokee hayo.
1. Mwanamke asikubali kubeba mimba ya mtu asiye eleweka.
2. Mwanamke asi " tegeshe" ipatikane mimba ili kulazimisha kuwa pamoja ( ndoa) hasa kama anajua mwanaume aliyenaye ana mipango mingine.
3. If mahusiano yalikufa , mtoto asilishwe "sumu" juu ya baba ake, baba ake apewe " access" ya mwanawe, pia mtoto asitumike kama ndio chanzo cha kupiga hela in a name of " Child support".
Vitu ni vingi aseee, ila kusema hili ni jambo la wanaume pekee aseee hii ni issue.
Na haitosaidia chochote.
 

Hawa wanaharakati uchwara wana matatizo sana. Sasa hapo amewasaidia hao watoto au amezidi kuwaharibu kisaikolojia?

Lakini ndugu zangu wanaume tuone aibu, tunatungisha mimba, tunapotea na kuwaacha watoto wakiteseka halafu baadae tunawalaumu mama zao eti wanawajaza chuki watoto.
 
Hili ni lifeminist tu linajikuta linamshirikisha Mungu kwenye mambo ya kipumbavu, mara nyingi au mara zote baba kukataa kuhudumia mtoto hapo ujue chanzo ni mama sema madingi hatunaga time ya kuzungumzia yanayotusibu tunakausha na Mungu ndo muamuzi.

Feminist huyu ni wa kupuuzwa hayo maombi yenyewe ukiyaangalia kwa jicho la tatu ni ya mchongo, maombi kashayafanyia rehearsal kayakariri mpuuzi mmoja wa kupuuzwa.
Una uhakika kuwa una jicho la tatu mkuu???
 
Back
Top Bottom