DOKEZO Waziri Gwajima, hii anayofanya Lillian Mwasha kwa watoto siyo sawa

DOKEZO Waziri Gwajima, hii anayofanya Lillian Mwasha kwa watoto siyo sawa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Anawauliza watoto wanaochukiwa na baba zao. Je amewaandaa kisaikolojia? Mbona yaonekankama ni udhalilishaji kwa watoto na wazazi wao. Angalia clip hapa

Mwanaume hata ukosane na mzazi mwenzako hakikisha unalea mtoto/watoto. Nimefurahi Sana hawa watoto wamesema vilio vya mioyo yao. Ninajua fika kuwa hao Baba wameona hizi Sura. Shame on them.
 

Hawa wanaharakati uchwara wana matatizo sana. Sasa hapo amewasaidia hao watoto au amezidi kuwaharibu kisaikolojia?

Lakini ndugu zangu wanaume tuone aibu, tunatungisha mimba, tunapotea na kuwaacha watoto wakiteseka halafu baadae tunawalaumu mama zao eti wanawajaza chuki watoto.
Mkuu kuna wanawake wapumbavu mno hapa duniani. Kuna dada kazaa na kaka yetu akawa analalamika hapati huduma.. sisi kama familia tukamwambia akiwa na shida yoyote asisite kutuambia ili tumsaidie lengo likiwa kutomlisha sumu mtoto. Binafsi nilijitolea sana mwanzoni. Shemeji akaona hapa ni mserereko akaanza kuleta mambo ya kifala mno. Akitaka kitu anasingizia jambo linalohusu mtoto na ubaya ni kwamba hapigi simu yeye bali humpa mtoto aongee. Ile hali ikaendelea nikaamua kumtolea uvivu kumwambia kama kuna shida anieleze mwenyewe bila kumpa mtoto simu. Baada ya kumwambia hivyo akanisusa na kuhamia kwa ndugu yangu mwingine. Hadi ninavyoandika hapa wote tumemblock kwa kuepuka upuuzi aliokuwa akifanya. Bro wangi yule alikuwa sahihi kabisa kukaa nae mbali.
 
Mkuu Dkt. Gwajima D karibu hapa

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
We unesema sawa kabisa. Hii ni kazi ambayo Ustawi wa Jamii wanafanya kila siku----- baba hataki kuleta hela za matumizi.
Lakini sheria ni very tricky unapotaka yule "baba" apime DNA.
Lakini kwa jinsi swali lilivyoulizwa hapa nilidhani anataka watoto wa normal families,siyo watoto wa single parents.
 
MKuu hivi uko siriaz?
1. Yuko hapo kuwatia moyo na kuwajenga.
2. Anawaondolea stress na chuki
Kosa liko wapi?

Nchi mnapenda usiri hata kwenye makosa.
Wewe ni baba uliyekataa mtoto?
Umeshajiuliza maisha watayoishi hao watoto hapo shuleni baada ya huo udhalilishaji? Kwanini asingezungumza nao pembeni bila wenzao kuona/kusikia na bila camera?
Athari za huo ujinga aliofanya ni zaidi ya athari za hao watoto kutelekezwa.
Anyway, wanawake huwatumia watoto kama fimbo, haijalishi baba anawajibika au hawajibiki.
 
Anawauliza watoto wanaochukiwa na baba zao. Je amewaandaa kisaikolojia? Mbona yaonekankama ni udhalilishaji kwa watoto na wazazi wao. Angalia clip hapa

Anawauliza watoto wanaochukiwa na baba zao. Je amewaandaa kisaikolojia? Mbona yaonekankama ni udhalilishaji kwa watoto na wazazi wao. Angalia clip hapa

Huyu ana mtoto wa umri huu kweli na anajua ghulba tunazopitia kuwa descpline hawa teenagers wetu majumbani!!? au anawatoto kweli!!!?

Hiyo shule inayoruhusu huyu kufanyia fields ZAKE kwenye shule hizo Ana uhakika aharibu brand ya hiyo shule!?
Juzi nimetoka kumtembelea binti yangu shule ni form six alinikimbilia nakunirukiakwa furaha akisema dady nilikumisi saana!!

lakini siku walipokuwa wamefungua shule jana yake nilimchapa baada ya kugoma kunyoa nywele huku akiwa tupia maneno ya kejeli mama yake kwa lugha ya kiingera eti mind your business!
Tandika haswa na nikamnyoa nywele na msamaha akaomba japo alisusia maandazi aliyopikiwa japo juzi nilimpelekea akayashambulia vilevile!

Huyu dada asipeleke hizi bulshit za single mothers anazowahoji huko ( majority ni uongo/ fake victims ) zitatuharibia watoto wetu mashuleni, aishie huko huko kwenye media! Aache kabisa asiwageuze watoto wetu kuwa one of her NGO packages

Soon hawa watoto watakuwa enjected kuwachukia wanaume and what next!!? Lesbians start this way!

LET NO ONE SHE IS NEGATIVE TO SPOIL OUR TRADITIONAL WAYS OF LIFE OR MANNERS!
 
FaizaFoxy, Habari za asubuhi FaizaFoxy. Utanisamehe Sana kwa kuwa sijaja humu JF kukubaliana na kila jambo ambalo litakupendeza wewe.

Kwa upeo wangu huu huu, katika hili, diagnosis yangu ni kuwa, huyu Lilian Mwasha amekosea hiki alichofanya, hakifai. Na kwa upeo wangu huu huu sijalala hadi nikampata na kumwambia hapa umekosea na aondoe hizo video mitandao yake yote.

Na kwa huu upeo wangu, nimemwagiza kamishna wa ustawi amwite kwa hatua zaidi na kufika kwenye hiyo shule waliko hao waalimu na watoto kwa hatua zaidi na tamko litolewe la marufuku kuhusu Kila mtu kuingia kwa watoto na kutoa huduma aina hizi na zingine.

Na pia hatua zingine zaidi zichukuliwe kwa mujibu wa taratibu za ustawi. Haya, na wewe Sasa kwa kuwa unao upeo mkubwa kabisa, ongezea tufanye nini zaidi.

Ila acha chuki binafsi Ili twende sawa. Nakubariki, ubarikiwe [emoji1666][emoji120][emoji2969]
 
Aseeeee
Shukrani mheshimiwa.
Kumbe mnaona.
Naona Sana, najitahidi Sana kushirikiana na jamii kuchukua hatua, hata niwe wapi siachi kuchungulia nini kinaendelea na kusaidia jambo pale ninapoona niongeze nguvu, ila pamoja na kuja hadi humu, wenzako wengine wanaona ni upuzi tu kwa kuwa mara ingine naweza kutofautiana nao [emoji28]. Anyway ndiyo uongozi na binadamu ni sisi sisi, Iko siku ya kale yatapita na tazama yatakuwa mapya, tutapumzika na yote, tuendelee kushirikiana.



Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Dkt. Gwajima D karibu hapa

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Ahsante Sana, pamoja na kuwa Niko safari mbali Sana na masaa yanatofautiana, Mungu alinipa Rehema za kuona. Kwa kweli hili jambo halina afya kabisaaa.

Pamoja na uchovu na usiku wote huo: nilihakikisha katika hatua za awali Nampata mhusika na kumwambia hili jambo ni baya, halifai na ni kinyume na sheria ya mtoto na huduma za ustawi. Aache mara moja. Aidha, nimeelekeza ofisi yangu washughulikie kwa stahiki zote zinazohusika na asitokee mwingine kufanya mambo haya hayafai.

Ahsante Sana.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Sioni alichokosea
Ifike wakati wababa wawajibike na malezi
Hao wasichana wanahitaji upendo na malezi ya baba zao
Amekosea, huwezi kuona kwa kuwa siyo taaluma yako pengine, lakini hata kama siyo taaluma yako, kwa mawazo ya kawaida kabisa, huwezi kwenda kufanya haya kwa utaratibu ule. Cancelling huwa ni huduma patanishi na hufanyika kwa usiri na kwa utaratibu rasmi na huzingatia pande zote.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kigezo kipi anatumia kuhakiki hiyo 'chuki' ikiwa ni mtoto ndio kaulizwa bila ya mzazi husika kuwepo??

Kuwaita mbele ya wenzao ni kuweka suluhisho lolote la kuleta huo upendo?? Kama dhamira ni kumkabili/wajibisha mzazi husika, je anaathirika/wajibishwa vipi ikiwa hayupo hapo??

Kwa sehemu kama shule hudhani anatengenezea hao waliojitokeza mbele mazingira ya kuonewa 'bullying' na wenzao kwa kufanyiwa dhihaka ya kutokupendwa na wazazi wao?
Uko sahihi kabisa, hapa ni kuongezea tatizo. Hatua zitachukuliwa na za awali mimi nimechukua tayari

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Ndio nani huko dasilama?

Nafikiri si sawa, kuna namna nzuri ya kuwatambua na kuwasaidia lakini sio hii.
Uko sahihi, baada ya kugundua kuna shida hii, hapa Kila kitu kingeenda kwa utaratibu rasmi wa itifaki za huduma za ustawi na kwa usiri na kutafuta ufumbuzi kwa kushirikiana na pande zote yaani wazazi na watoto.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Hizi harakati za wakina dada na wakina mama sidhani kama zitawaacha salama wakina dada na wakina mama wajao.
Hili kakosea, hatua zitachukuliwa na wengine wasifuate huu utaratibu. Yako baadhi ya matatizo ikiwemo haya ya migogoro ya watoto na familia inabidi jamii wawape wataalamu wa ustawi wa jamii Ili waendelee kitaalamu.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Mh ikiwezekana ni maombi yetu tafadhali hawa wanaharakati katika engo yoyote wasiwe wanapewa nafasi ya kuzungumza na watoto huko shuleni bila wataamu na miongozo sahihi dhidi ya hayo mazungumzo.

Urahisi wa kujenga kizazi kijacho katika mtazamo hasi katika mambo mengi ni mkubwa mno.

Mtu mwenye maumivu na machungu na majeraha hata kuwa na jema la kuijengea jamii kwa mtazamo ulio kinyume na yalio moyoni mwake. Kuna msemo usemao kinywa cha mtu hunena yaliyo moyoni mwake.

Wakati huu mlio na dhamana ya kusimamia ustawi wa jamii yetu tunaomba mjaliwe hekima ya kusikia kinywa kinachonena majeraha yaliyo jaa moyoni ili mkinyamazishe.
Uko sahihi, kuingia shuleni kusema na watoto kuna sehemu utaratibu unakosewa. Ngoja tuwekane sawa, siyo Kila mtu anatakiwa kuwa msemaji na watoto huko shuleni

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom