FaizaFoxy, Habari za asubuhi FaizaFoxy. Utanisamehe Sana kwa kuwa sijaja humu JF kukubaliana na kila jambo ambalo litakupendeza wewe. Kwa upeo wangu huu huu, katika hili, diagnosis yangu ni kuwa, huyu Lilian Mwasha amekosea hiki alichofanya, hakifai. Na kwa upeo wangu huu huu sijalala hadi nikampata na kumwambia hapa umekosea na aondoe hizo video mitandao yake yote. Na kwa huu upeo wangu, nimemwagiza kamishna wa ustawi amwite kwa hatua zaidi na kufika kwenye hiyo shule waliko hao waalimu na watoto kwa hatua zaidi na tamko litolewe la marufuku kuhusu Kila mtu kuingia kwa watoto na kutoa huduma aina hizi na zingine. Na pia hatua zingine zaidi zichukuliwe kwa mujibu wa taratibu za ustawi. Haya, na wewe Sasa kwa kuwa unao upeo mkubwa kabisa, ongezea tufanye nini zaidi.
Ila acha chuki binafsi Ili twende sawa. Nakubariki, ubarikiwe [emoji1666][emoji120][emoji2969]
Sent from my CPH2207 using
JamiiForums mobile app