DOKEZO Waziri Gwajima, hii anayofanya Lillian Mwasha kwa watoto siyo sawa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mheshimiwa huwa nakupita kimya kimya hapa JF lakini nimeona nawiwa kukupa hongera kwa uwajibikaji wako na kuwa karibu na jamii kwa maswala yanayokuhusu.
Hongera sana mama.
Hbr za asubuhi. Ahsante Sana kwa ufuatiliaji. Usinipite kimya kimya ndugu yangu, nahitaji mawazo ya kila mmoja, ahsante kwa Leo, endelea kufuatilia na kutoa ushirikiano. Jamii yetu ina mambo mengi Sana, huku lile huku jingine jipya. Ila tutafika kwa ushirikiano. Ubarikiwe

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
MKuu hivi uko siriaz?
1. Yuko hapo kuwatia moyo na kuwajenga.
2. Anawaondolea stress na chuki
Kosa liko wapi?

Nchi mnapenda usiri hata kwenye makosa.
Wewe ni baba uliyekataa mtoto?
Hizi huduma hazitolewi kwa staili hii. Ngoja wataalamu wa huduma hizi waandae kipindi halafu ufuatilie utajua. Vipindi lakini vinatolewa ila watanzania ni wengi nadhani wengine hamsikii kwa wakati

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Habari za asubuhi FaizaFoxy. Utanisamehe Sana kwa kuwa sijaja humu JF kukubaliana na kila jambo ambalo litakupendeza wewe. Kwa upeo wangu huu huu, katika hili, diagnosis yangu ni kuwa, huyu Lilian Mwasha amekosea hiki alichofanya, hakifai. Na kwa upeo wangu huu huu sijalala hadi nikampata na kumwambia hapa umekosea na aondoe hizo video mitandao yake yote. Na kwa huu upeo wangu, nimemwagiza kamishna wa ustawi amwite kwa hatua zaidi na kufika kwenye hiyo shule waliko hao waalimu na watoto kwa hatua zaidi na tamko litolewe la marufuku kuhusu Kila mtu kuingia kwa watoto na kutoa huduma aina hizi na zingine. Na pia hatua zingine zaidi zichukuliwe kwa mujibu wa taratibu za ustawi. Haya, na wewe Sasa kwa kuwa unao upeo mkubwa kabisa, ongezea tufanye nini zaidi.

Ila acha chuki binafsi Ili twende sawa. Nakubariki, ubarikiwe [emoji1666][emoji120][emoji2969]

Hongera Dk. kwa hatua hii tukuka. Hakika upo hapo kwa kusudi la Mungu.

Tuko pamoja.
 
Amekosea, huwezi kuona kwa kuwa siyo taaluma yako pengine, lakini hata kama siyo taaluma yako, kwa mawazo ya kawaida kabisa, huwezi kwenda kufanya haya kwa utaratibu ule. Cancelling huwa ni huduma patanishi na hufanyika kwa usiri na kwa utaratibu rasmi na huzingatia pande zote.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Kuna watu humu usipoteze muda wako kuwajibu Mama.

Utachoka bure.
 
Hizi huduma hazitolewi kwa staili hii. Ngoja wataalamu wa huduma hizi waandae kipindi halafu ufuatilie utajua. Vipindi lakini vinatolewa ila watanzania ni wengi nadhani wengine hamsikii kwa wakati

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Mheshimiwa Waziri, nashauri watu kama hawa muwe mnawapa semina, ili wafanye kwa usahihi.

Pili, mheshimiwa Waziri natamani ungetembelea kituo cha watototo flani...nisikitaje jina au utume wataalam wako.

Kuna mtu amewajaza kituoni, anapewa misaada ya waziwazi na wazungu na raia pia lakini jioni yake anapeleka kuuza vyakula kwa maduka makubwa na watoti wana hali mbaya sana.

Nitawasilishaje hili kwako?

Mtaani kwetu kila mtu analaani
 
Habari za asubuhi FaizaFoxy. Utanisamehe Sana kwa kuwa sijaja humu JF kukubaliana na kila jambo ambalo litakupendeza wewe. Kwa upeo wangu huu huu, katika hili, diagnosis yangu ni kuwa, huyu Lilian Mwasha amekosea hiki alichofanya, hakifai. Na kwa upeo wangu huu huu sijalala hadi nikampata na kumwambia hapa umekosea na aondoe hizo video mitandao yake yote. Na kwa huu upeo wangu, nimemwagiza kamishna wa ustawi amwite kwa hatua zaidi na kufika kwenye hiyo shule waliko hao waalimu na watoto kwa hatua zaidi na tamko litolewe la marufuku kuhusu Kila mtu kuingia kwa watoto na kutoa huduma aina hizi na zingine. Na pia hatua zingine zaidi zichukuliwe kwa mujibu wa taratibu za ustawi. Haya, na wewe Sasa kwa kuwa unao upeo mkubwa kabisa, ongezea tufanye nini zaidi.

Ila acha chuki binafsi Ili twende sawa. Nakubariki, ubarikiwe [emoji1666][emoji120][emoji2969]

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Naomba umsamehe huyu bibi yetu wa jf, lugha yake huwa imejaa ukakasi sana.
Msamehe mheshimiwa.
 
Naona Sana, najitahidi Sana kushirikiana na jamii kuchukua hatua, hata niwe wapi siachi kuchungulia nini kinaendelea na kusaidia jambo pale ninapoona niongeze nguvu, ila pamoja na kuja hadi humu, wenzako wengine wanaona ni upuzi tu kwa kuwa mara ingine naweza kutofautiana na[emoji28]. Anyway ndiyo uongozi na binadamu ni sisi sisi, Iko siku ya kale yatapita na tazama yatakuwa mapya, tutapumzika na yote, tuendelee kushirikiana.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Mshahara wako unautendea haki.💯💯🙏🙏🙏
 
Kuna watu humu usipoteze muda wako kuwajibu Mama.

Utachoka bure.
Nakubaliana na wewe. Lakini kuna wakati Roho wa Mungu ananiambia niseme nao tu tena kwa hekima na upole Ili labda watapona dhidi ya mzigo wa chuki ambao nadhani wengi wametwishwa kwa kusudi la mwovu au wamejitwisha tu wao wenyewe mzigo ambao hata hawana safari nao. Hivyo, labda itawaponya.

Ila nawasoma kuwa wengine wako kimkakati kabisa na kadri ninavyowatambua nami kweli sasa nitawapotezea Ili waendelee na lao nami na langu. Halafu Baraka za Mungu zitatimia kwa Kila mmoja kwa kadri ya Rehema zake atujuaye wote. [emoji1666] Ubarikiwe. Ahsante Sana.

AMINA.💯👌👌
 
Mheshimiwa Waziri, nashauri watu kama hawa muwe mnawapa semina, ili wafanye kwa usahihi.

Pili, mheshimiwa Waziri natamani ungetembelea kituo cha watototo flani...nisikitaje jina au utume wataalam wako.

Kuna mtu amewajaza kituoni, anapewa misaada ya waziwazi na wazungu na raia pia lakini jioni yake anapeleka kuuza vyakula kwa maduka makubwa na watoti wana hali mbaya sana.

Nitawasilishaje hili kwako?

Mtaani kwetu kila mtu analaani hili, tumemuinya mhusika tumechoka
Tena Hawa wanaohujumu watoto vituoni ndiyo nilitoa na press siku moja tunahitaji taarifa zao. Nitumie sms tafadhali kwenye 0765345777 nijue ni wapi huko wataalamu wakatimize jukumu lao kwa utaratibu stahiki.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Naomba umsamehe huyu bibi yetu wa jf, lugha yake huwa imejaa ukakasi sana.
Msamehe mheshimiwa.
Eti nami akili yangu ikanituma kuwa nijali tu hoja zake kama binadamu mwenzangu nikiamini labda nami naweza kumshauri kama yeye anavyoshauri wengine Ili kama kusudi letu ni moja kwa ustawi wa JMT [emoji1241] yetu, basi twende naye sawa Nadhani Mungu atanijalia karama ya roho wa kutambua uelekeo wake na kisha huenda sasa nikamwacha ajitukuze yeye kwa kusudi lake nami niendelee na langu. Nakubaliana kabisa na ww, maana mara zote akili yangu mm ndogo yake ndiyo super brain [emoji28][emoji28][emoji28]

Back
Top Bottom