DOKEZO Waziri Gwajima, hii anayofanya Lillian Mwasha kwa watoto siyo sawa

DOKEZO Waziri Gwajima, hii anayofanya Lillian Mwasha kwa watoto siyo sawa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Watoto waliotoka mbele wana maumivu makubwa sana mioyoni! Kila mzazi wa kiume au wa kike ebu akae kwenye nafasi yake. Tunawapata hawa watoto kwa mapenzi yetu lakini mapenzi yakinyauka tunawapa watoto huzuni kubwa sana
 
Sioni alichokosea
Ifike wakati wababa wawajibike na malezi
Hao wasichana wanahitaji upendo na malezi ya baba zao
Kwa kigezo kipi anatumia kuhakiki hiyo 'chuki' ikiwa ni mtoto ndio kaulizwa bila ya mzazi husika kuwepo?

Kuwaita mbele ya wenzao ni kuweka suluhisho lolote la kuleta huo upendo? Kama dhamira ni kumkabili/wajibisha mzazi husika, je anaathirika/wajibishwa vipi ikiwa hayupo hapo?

Kwa sehemu kama shule hudhani anatengenezea hao waliojitokeza mbele mazingira ya kuonewa 'bullying' na wenzao kwa kufanyiwa dhihaka ya kutokupendwa na wazazi wao?
 
Hili ni lifeminist tu linajikuta linamshirikisha Mungu kwenye mambo ya kipumbavu, mara nyingi au mara zote baba kukataa kuhudumia mtoto hapo ujue chanzo ni mama sema madingi hatunaga time ya kuzungumzia yanayotusibu tunakausha na Mungu ndo muamuzi.

Feminist huyu ni wa kupuuzwa hayo maombi yenyewe ukiyaangalia kwa jicho la tatu ni ya mchongo, maombi kashayafanyia rehearsal kayakariri mpuuzi mmoja wa kupuuzwa.
 
Kwa kigezo kipi anatumia kuhakiki hiyo 'chuki' ikiwa ni mtoto ndio kaulizwa bila ya mzazi husika kuwepo??

Kuwaita mbele ya wenzao ni kuweka suluhisho lolote la kuleta huo upendo?? Kama dhamira ni kumkabili mzazi husika, je anaathirika vipi ikiwa hayupo hapo??

Kwa sehemu kama shule hudhani anatengenezea hao waliojitokeza mbele mazingira ya kuonewa 'bullying' na wenzao kwa kufanyiwa dhihaka ya kutokupendwa na wazazi wao?

Kigezo cha kukataa mimba, kuweka condition love
Moja kwa moja ni kwamba hawapendiwi
Ulitaka athibitisheje?
Hakuna nguvu kubwa kama hiyo aliyowapa kumtumainia Mungu wao
Na bd kawambia anataka kukutana nao likizo
Unajua anataka kufanya nini
 
Back
Top Bottom