Dawa ni kuomba poo mambo yaishe na heshima iwepo kwa mkubwa na mdogo.
 
CCM hawaelewi washike wapi au waachie wapi..

Wamejifanya kuachia mikutano ili kuionyesha dunia kuna demokrasia matokeo yake CHADEMA nondo wanazopiga kwenye mikutano ni za moto sana, kiasi kwamba upepo unabadilika na watu wanaonekana kuelewa sana. CCM uvumilivu umewashinda na wamerudi tena kuanza kutumia mabavu.

Wakipiga marufuku mikutano ndio kama hivyo wanazidi kujichafua kwa uminyaji wa demokrasia, wakisimama ni mshale na wakikaa ni mshale.

Siku ya kufa nyani miti huteleza, by the way sina chama lakini huo ndio ukweli. asipo Polisi CCM hawana uwezo kupambana na CHADEMA.
 
Huu ujinga wanatufanyia makusudi wakijua ni kinyume cha sheria, na kwasababu hatutawafanya chochote.

Hapo zitaanza zile safari za kwenda mahakamani kupinga hiyo amri, mpaka hukumu ije kutoka ni miaka miwili.

Hivi hii michezo tutaendelea kuvumilia tukichezewa mpaka lini?!
 
CCM hawawezi kucheza mziki wa chadema hata simu moja, Leo waziri wao wameamua kutoa la rohoni wakaona waweke mpira kwapani wasepe nao. HATA SIKU MOJA UONGO HAUKAI SEHEMU UKWELI UMESIMAMA
CCM ina dhamana na inawajibika katika kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo waTanzania wote na sio kucheza muziki kama vyama vingine vya siasa visivyo na agenda.

acha upotoshaji useless jukwaani gentleman πŸ’
 
CCM ina dhamana na inawajibika katika kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo waTanzania wote na sio kucheza muziki kama vyama vingine vya siasa visivyo na agenda.

acha upotoshaji useless jukwaani gentleman πŸ’
CCM na wafuasi wake hawakupaswa kuwa zama hizi bali walipaswa kuwa stone age
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…