Waziri Mahiga: Serikali ya Uturuki imetuambia wamiliki wa shule za Feza ni magaidi

Mkuu taratibu
Maana navyojua Mimi mafunzo ya ugaidi ni kutumia silaha kama milipuko.
Na hao wanafunzi raia wa kitanzania walikuwa wanafundishwa ili wakafanyie wapi uo ugaidi?

Na hayo maeneo nikimaanisha eneo la kujifunzia uo ugaidi yalikuwa na wapi mpaka usalama wetu wa taifa miaka yote isigundue?

Hivi hiyo kauli yao hawaoni kuwa wanatudhalilisha kuwa nchi yetu ni ya hovyo watoto wanafundishwa ugaidi bila serekari kujua?

Kweli siasa ni mchezo mchafu
 

OMG! Too many broken links; please help us see what you see!
 
Wenzetu wapo juu sana katika intelijensia
Rudi nyuma kufuatilia mgogoro wa jimbo la wakurdi wanaitaka kujitenga na uturuki
 
Nilishitushwa sana na coups attempt aftermath. Kamatakamata ambayo ilitokea na bado inaendelea kutokea sijawahi kuishuhudia popote pale duniani ambapo yamepata kufanyika mapinduzi! Takribani watumishi 50,.000 wamepoteza ajira kwa kigezo cha ku-support mapinduzi huku miongoni mwao wakiwemo majaji, walimu na maaskari! Saa chache zilizopita President Erdogan hati ya kukamatwa mchezaji wa zamani wa Galatasaray. Yaani Erdogan amekuwa too paranoid... ni kama amepata sababu za kunyamazisha wote anaohisi ni threat kwa utawala wake. Na hapa ilipofikia, ni kama anajiweka katika mazingira magumu zaidi ya kuongoza Uturuki to the point nafikia kuamini huu mwaka huenda asiumalize salama kabla jaribio lingine halijafanyika... na sidhani endapo hilo litakuwa jaribio but successful coups d'état! Sasa ikiwa hunting imeshavuka mipaka hadi Afrika sasa sijui ni nani atapona huko!
 
Na ndio maana uchunguzi wa kina lazima ufanyike ili kufikia ukweli
 

La msingi ni kupata ushahidi wa kutosha. Kama balozi wao amesema anahusika na ugaidi, inahusika na imamu fethullah aliyeko Marekani, imeshiriki katika jaribio la mapinduzi uturuki, serikali ya Tanzania inakanusha kwa sababu hawa watu inawachunga masaa 24 kwa ukaribu, inamiliki mawasiliano na mahusiano yao yote, inascan nyendo zao majumbani mwao na kila kitu wanafanya?

Siyo busara kukanusha jambo bila research. Wanatakiwa kushirikiana na serikali ya uturuki ili ku establish misingi ya tuhuma hiyo kabla hawajaeda hatua za kukanusha ama kukubali.

Baada ya kuestablish facts, waombe kujua Turkey inahitaji nini na serikali hapo ipime kama ombi hilo linatekelezeka ama kuna namna nyingine.

Watu wanachanganya Feza kama shule na umililki wa shule. Anayetuhumiwa kwa ugaidi ni umiliki wa shule siyo shule.

Shule zinaweza kufuata kila suala zuri la elimu kama vile gaidi anavyoweza kuwa na biashara nzuri ya kuoka na kusambaza keki zisizo na sumu. Lakini bado nia yake na matumzi ya mapato yake yakawa kufanikisha uovu mahala fulani duniani.

Tunasoma kila siku magaidi wanahusika na mauaji ya tembo wetu, biashara za madini yetu, mafuta n.k. Kuwa na mmiliki wa shule nzuri inayofanya vizuri siyo taswira ya dhamira na mipango yake.

Serikali iwe makini na hili lsuala kwa maslahi ya taifa letu. Magaidi wanapata resources kwa njia nyingi sana zikiwemo biashara halali na haramu.
 
Kutakatisha fedha natafakari
 
Kwahiyo watoto wa wakubwa wanaopiga buku pale wanapata darasa la ugaidi shuleni?
 
Duh! Jamaa umenikumbusha ada elekezi
 
Kutakatisha fedha natafakari

Zinaweza kuwa zinaenda kwa mfumo wa kawaida kabisa bila hata utakatishaji lakini zimelengwa kufanikisha ugaidi.

Wakisema wanatuma fedh akwenda kwa yule Fetullah aliyeko marekani, kwa jambo sahihi kabisa na la wazi, nani ataquestion? Fetullah anapochannel hizo fedha kutoka amerika, Tz inasimamiaje kwamba haziendi kufanikisha ugaidi?

Serikali ichunguze.
 
shule za FEZA zinaendeshwa na wafanyabiashara wa kitanzania na waturuki wachache

Nani wamiliki? Umesema tu waendeshaji. Hao Waturuki nani anawajua nyendo zao zote? Uturuki wamefahamu vipi kuna feza school tz yenye waturuki?

Uchunguzi ufanyike tu ili watu wasionewe wala kuumizwa kwa jinsi isivyo halali.
 
Waturuki wenyewe wanasema FEZA ni magaidi alafu nyie wabongo mnaleta ubishi..... Povu jingi..... Subirini muone
Hata Mandela, Samora, Mugabe na wakombozi wengine waliwahi kuitwa magaidi. Imekuwa ni fashen kwa kila anayepinga status quo anaitwa gaidi! ili kulinda maslahi kikundi.
NADHANI Feza inaingizwa mkumboni kutokana na rekodi yake njema katika kutoa elimu bora nchini, jambo haliwapendezi baadhi ya wafafidhina waliokwishazoea kuona shule za madhehebu Fulani tu zikiongoza katika utoaji wa elimu bora! Ni tafakuri binafsi tu ambayo haitakuwa na nguvu km serikali itayapuuza madai hayo pandikizi!
 
Taarifa zimepelekwa kwa hao jamaa kua huku tanzania kuna shule ya upande fulani imeanza kufaulisha sana tufanyeje ili tuiue tubaki na shule zetu?kwa vile nchi yetu ni ya upande fulani basi wakatoa ushirikiano haraka sana.
Labda nijuzwe kidogo nimeona Makanisa yakimiliki shule na taasisi za kibiashara lakini bado sijaona Misikiti inayofanya hivyo bali nimeona misikiti ndani ya taasisi fulani.So hata Feza umiliki wake sidhani kama umeasisiwa kidini
 
Kiongozi nadhani hujaelewa issue nikwamba hizi Shule zinamilikiwa na Jamaa alietaka kupindua Serikali....nakwenye Mapinduzi inatumika Pesa..Kwahiyo inasemakana chanzo cha pesa zinazoSupport huo ugaidi zinapatikana miongoni mwa hizo Shule sasa wanataumia ile ukitaka kumuua NYOKA mkate KICHWA kabisa
 
Unamaanisha Waturuki wazushi
It's obvious as mentioned by the Turkey government some of the teachers impart secretly dangerous doctrine to our sons and daughters hence let our able government led by Dr Magufuli as President take heed, take appropriate action at the right time after thorough investigation, we should remember the sayings of the retired president Jakaya Kikwete,"akili za kuambiwa changanya na za kwako"!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…