Waziri Mkenda: Ajira ya Chuo Kikuu isiwe kuangalia GPA pekee lazima wapimwe, wafanye na usaili

Kweli kabisa. Yaani hili kundi ndilo lililofeli kabisa wanaokandia. Kuna watu wana akili acha kabisa.
 
Pain killer na Mudawote kwani Profesa Mkenda Kakandia GPA au kuna mtu anaponda GPA. Labda lengo la Profesa liko kwenye kuboresha usaili wa wale wanaobakizwa chuoni kutokana na GPA zao kuwa kubwa. Hapo kuna ubaya gani??
 
Ulichozungumza upo sahii lkn sio kila mwny GPA kubwa ama ufaulu mkubwa anaweza kuwa tutor..
Nmefaulu vzur o level na a level lkn hyo haimanish nna uwezo wa kutransfer knowledge kwa watu wengne...
Transferring knowledge and skills is an art na sio kila mtu anahyo sanaa
 
Humu watu Kuna wajinga tu na Wenye wivu ,wapo hapa kuponda watu wenye gpa zao nzuri ,waliotumia muda wao vzuri chuo kujisomea ....

Jitu lipo hapa kusema lecture wetu wamekariri ,ameshindwa kuelewa kuwa na kumbukumbu ya yale uliyofundishwa ni akili kubwa ...

Mtu mwenye gpa ya 4.7 yupo na uwezo mzuri kuzid Hao wenye 2.0 ila humu ndani mnajipa Moyo na kutoa mifano mfuu ili kuponda gpa [emoji3][emoji3][emoji3]


Wengi wanaoponda humu ,hawajafika chuo ,hata kama wamefika wamefeli vibaya mnoo ,gpa za 2.p Sasa wanajifaliji Kwa kuziponda GPA kubwa [emoji3]wanataka wawe sawa na watu waliotumia muda wao vzuri chuo kujisomea na kufaulu vzuri ...

Kiufupi wewe mwenye 2.0 hitakuja kuitwa hata interview kujua una nin ,wanaitwa wenye 4.7 ...

Humu ndani watu Wana wivu ,uchawi ,roho mbaya ,na husdaa ya hali ya juu dhidi ya watu waliojisomea na kufaulu [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Pure fact.. maisha ya chuo unaezq kutana na lecturer hawez kudeliver content ndig tuu mpk unajiulza huyu kawaje lecturer
 
Mi nadhani pia wangeweka na kigezo cha kusomea ualimu either bachelor ama postgraduate kwa wanaokwnda kufundisha vyuoni
 
Kuna Chuo hapa dar ndio mbishe zake hizi.

Wanachuo wa kike wanaliwa sana gesti na kupewa ghaka/possible qns Ili wafaulu vizuri Pepa.
 
Ahahahahah kama umeniona vile, maana nishawahi kuitwa na. mkuu mmoja wa chuo alikuwa rafiki yangu huku Mkoani, akasema bora uje ufundishe, siuna-GPA ya 3.8 nikamwambia waapi mkuu, nina 3.7 ya SUA.

Ajira ikaishia hapo, na ninao uwezo mkubwa sana wa kufundisha lkn ndo hivyo tena ahahahah
 
Pain killer na Mudawote kwani Profesa Mkenda Kakandia GPA au kuna mtu anaponda GPA. Labda lengo la Profesa liko kwenye kuboresha usaili wa wale wanaobakizwa chuoni kutokana na GPA zao kuwa kubwa. Hapo kuna ubaya gani??
GPA itaendela kuwa kigezo cha kuita watu kwenye usaili na kuajirii Hilo halipingiki ....

Siwezi kuita mjinga mwenye gpa ya 2.0 wakati mezani nina CV ya watu wenye gpa za 4.0 and above et Kwa kujipa Moyo anaweza kuwa na akili ...

Kama ameshindwa kuwa na kumbukumbu za alichokuwa anafundishwa shuleni na kujibu mtihani na kufaulu ataweza nin kazin ..


Harafu fuatili watu wengi wenye gpa za 2.0 ni weupe vichwani kama ilivyo kwenye karatasi ,gpa ya chuo ,matokeo ya form six ,matokeo ya form four havijawahi kudanganya [emoji3][emoji3][emoji3]...

Nioneshe vyetu vyako vyote hivyo nikuambie uwezo wako wa kufikili na kuchambua Mambo ....
 
GPA itaendela kuwa kigezo cha kuita watu kwenye usaili na kuajirii Hilo halipingiki ....
Na hili la GPA kuendelea kuwa kigezo ni jambo siyo la kujadili, ndivyo ilivyo na ndivyo itakavyokuwa na ndivyo Mkenda alivyosema.

Nani kasema waitwe wenye GPA ndogo? Ila kinachosemwa ni kwamba hao wenye hizo GPA kubwa ni LAZIMA wasailiwe kwa KINA.

Hapo Tatizo liko wapi!!??
 
Nioneshe vyetu vyako vyote hivyo nikuambie uwezo wako wa kufikili na kuchambua Mambo ....
Dunia hii itakuwa ngumu sana kama kupima uwezo wa uelewa wa watu itakuwa ni kwa kuoneshana vyeti. Waliogundua hii mifumo ya Kompyuta tunayotumia kuwasiliana walimuonesha nani vyeti!!??
 
Dunia hii itakuwa ngumu sana kama kupima uwezo wa uelewa wa watu itakuwa ni kwa kuoneshana vyeti. Waliogundua hii mifumo ya Kompyuta tunayotumia kuwasiliana walimuonesha nani vyeti!!??
Hao ni ma genius na dunian wapo wachache Sana .....huo sio mfano ..
 
Nakukatalia pamoja kuwa mi sijui sana mambo ya chuo maana nilipita tu huko nikachukua ki degree changu. Huu ujinga ndiyo mmekaririshwa kila kitu kikiharibika mnasingizia serikali. Chuoni kila mtu anapaswa kupambana, wala siyo rushwa ni uongo.
Ninachokueleza ni kwamba graduates, matokeo yao ya makaratasi hayafanani na kilichomo kichwani, Nawapokea sana, nawapa nafasi sana, field wanaziomba sana, kujitolea na ajira wanaomba hivyo nakutana nao mara nyingi tu na wakati mwingine yule ambaye kwenye makaratasi wala haonekani mwenye elimu kubwa na diploma ya vyuo visivyo rasmi anafanya vizuri tu kuzidi vijana wa IAA, Mzumbe, UD, UDOM SAUT n.k.

Mfano wa swali jepesi katika field ya biashara ambalo mwanachuo yoyote esp mwenye GPA kubwa hakupaswa kushindwa kulijibu: Ni nyaraka zipi zinatumika kufanya miamala baina ya raia wawili walio nchi tofauti wakati wanafanya biashara?

Hii ni international trade, Mtu ana BBA na GPA fiirst class lakini anajibu mpaka unaona huruma, wakati mwingine unadhani ni panic unamwambia relax, kunywa maji unampigisha hadithi nyingine ili asiumie kisha ukishaona karudi normal unaruhusu panel iendelee ila still wengi wanashindwa na hapo swali limeulizwa kwa kiswahili.

BOSS NAKUELEZA, TUNA TATIZO LINALOPASWA KUFANYIWA KAZI. TUNAPOELEKEA IKITOKEA PAKAWA NA UHURU WA KUAJIRI BAINA YA EA VIJANA WETU WATAUMIA SANA.
 
Acha wivu, boss. Hivi boss unazungumzia graduates wepi wa UD, au UDOM au SUA. Maana karibia viongozi wote Tanzania ni graduates wa hivyo vyuo.
 
Wangetumia hizi nguvu kuangalia AJIRA za MAJESHI yetu

Wanaaajiri majinga kisa JKT... Kigezo cha kipuuzi na Tutaendelea kuwa na JESHI la kipuuzi.
 
Hivi mkuu umesoma kweli? Au wewe ndio miongoni mwa yale masifuri tuko nayo katika hii nchi?

Ni bahati mbaya sana na sijui kama unajua, uhusiano unaojaribu kuutengeneza kati ya matokeo ya mtu ya darasa la saba hadi kidato cha sita na GPA ya chuo ni uhusiano mfu na haupo.

Aya yako ya kwanza ndio kitu anacholia nacho Waziri, kuwa na GPA kubwa kutoka katika chuo chochote kile Tanzania isiwe kigezo pekee cha mtu kuajiriwa kuwa mkufunzi chuoni.

Waziri yupo sahihi, watu wasipate ajira moja kwa moja baada ya kuwa na GPA kubwa, wapimwe kwanza. Kufundisha Chuo kikuu ni kazi inayohitaji mtu mwenye uelewa mpana sana na kudadavua mambo.

Wapo watu wenye GPA kubwa na walizipata kihalali kabisa kwa kukariri notes za darasani na kuyaotea maswali, hawa hawawezi kuwa wakufunzi kwasababu nje ya hiyo mitihani waliyofaulu hamna kitu kingine.

Lakini pia kuna waliopata hizo GPA kubwa kwa njia za kona kona kama kuwa karibu na wakufunzi, hawa pia kuwapa ajira moja kwa moja ni tatizo.

Vyuoni wapo wakufunzi ambao wanaingia kufundisha lakini anaishia kusoma notes, na hata akiulizwa swali na mwanafunzi anashindwa kujibu kwasababu alikariri na uwezo wake ni mdogo.

Andiko langu haliondoi ukweli kwamba wenye GPA ndogo ni VILAZA tu.
 
Acha wivu, boss
Boss, sipo hata kwenye nafasi ya kushindana na yoyote kielimu katika kuchangia uchumi wa hii nchi.

Nilipata nafasi ya ajira nikafanya sehemu yangu na kumaliza na sasa nipo katika nafasi ya kuwezesha wengine wapate ajira. GPA sio suala langu tena maana wakati wangu ulishapita ila Natoa maoni kulingana na kile ninachokiona, kusema kuwa ni wivu hakutabadili uhalisia wa ninachokiona.
 
Hao ni ma genius na dunian wapo wachache Sana .....huo sio mfano ..
Huwezi jua labda na Tanzania tunao "Genius"" wengi tu.

Turudi kwenye mada. Unajua kwamba zamani usomi ulipimwa kwa uwezo binafsi wa mtu kujenga hoja na si vyeti!? na Vyuo walivyosoma hao unaowaita "Genius" vilikuwa havitumii mifumo kama hii inayotumika sasa?

Mimi naona mbali na GPA ni lazima usomi wa mtu upimwe kwa vitendo baada ya kufaulu nadharia/vitendo vya chuoni. Nchi zilizoendelea hutaka sana kujua baada ya kufaulu mitihani wewe binafsi unaweza kuongeza nini kwenye jamii na siyo kusema una GPA kubwa ama ndogo!!?

Wavumbuzi wengi hawakumbukwi kwa GPA bali kwa vumbuzi zao. Leo hii Mark Zuckerberg ama Bill Gates wanakumbukwa kwa uvumbuzi wao na si kwa GPA zao. Bado nasisitiza kwamba kigezo cha GPA kuwa kubwa ndiyo uajiriwe kuwa mhadhiri hakijatolewa na Profesa Mkenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…