Ninachokueleza ni kwamba graduates, matokeo yao ya makaratasi hayafanani na kilichomo kichwani, Nawapokea sana, nawapa nafasi sana, field wanaziomba sana, kujitolea na ajira wanaomba hivyo nakutana nao mara nyingi tu na wakati mwingine yule ambaye kwenye makaratasi wala haonekani mwenye elimu kubwa na diploma ya vyuo visivyo rasmi anafanya vizuri tu kuzidi vijana wa IAA, Mzumbe, UD, UDOM SAUT n.k.
Mfano wa swali jepesi katika field ya biashara ambalo mwanachuo yoyote esp mwenye GPA kubwa hakupaswa kushindwa kulijibu: Ni nyaraka zipi zinatumika kufanya miamala baina ya raia wawili walio nchi tofauti wakati wanafanya biashara?
Hii ni international trade, Mtu ana BBA na GPA fiirst class lakini anajibu mpaka unaona huruma, wakati mwingine unadhani ni panic unamwambia relax, kunywa maji unampigisha hadithi nyingine ili asiumie kisha ukishaona karudi normal unaruhusu panel iendelee ila still wengi wanashindwa na hapo swali limeulizwa kwa kiswahili.
BOSS NAKUELEZA, TUNA TATIZO LINALOPASWA KUFANYIWA KAZI. TUNAPOELEKEA IKITOKEA PAKAWA NA UHURU WA KUAJIRI BAINA YA EA VIJANA WETU WATAUMIA SANA.