Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatakiwa kuwajibika kwa kudanganya Taifa lililokuwa na taharuki kubwa

Waziri Mkuu wa Tanzania aliwadanganya Watanzania tena akiwa msikitini kuwa Rais ni mzima na anaendelea na kazi. Alifikia hadi kuwashutumu waliokuwa wanahoji alipo rais kuwa wao sio wazalendo hadi kufikia kutoa kauli za kashfa kuwa walikuwa wanataka Rais akazurure kariakoo.

Wakati makamu wa rais (Rais Mtarajiwa) anatoa taarifa za msiba aliweka wazi kuwa rais alikuwa amelazwa hospital mara mbili. Hivyo kwa kauli za makamu wa rais ni udhihirisho kuwa Waziri Mkuu alidanganya taifa.

Atoke hadharani aombe msamaha.

 
Kwa kweli Majaliwa pale hakutumia hekima ya kiongozi kama yeye.
Anafikiri afya ya kiongozi wa juu ni mali ya serikali, amelewa madaraka hakumbuki kuwa kiongozi yeyote ni sisi wananchi tumewaweka pale na wanawajibika kwetu.
 
Likivunjwa Baraza la mawaziri nae akae pembeni
 
Inatakiwa wote walioshiriki kuua democrasia waondolewe wakachunge ng'ombe vijijini mwao..
 
Waziri mkuu anatakiwa ajiuzulu kwa kulidanganya Taifa kwamba rais yupo ofisini na anachapa kazi, Kumbe uongo, Angesema rais ni mgonjwa wananchi wangeweza kumuombea hata akapata nguvu tena. sasa wananchi hata wangemuombea huko aliko wasingweza kuwekeza katika kumuombea kumuepusha na hatari za roho na mwili kwa sababu waziri mkuu kasema akiwa msikitini kwamba rais ni mzima wa afya. waziri mkuu ajiuzulu katika hili.
 
Katiba ingekuwa fair enough tungemtoa kwa maandamano
 
Kwa kweli Majaliwa pale hakutumia hekima ya kiongozi kama yeye.
Anafikiri afya ya kiongozi wa juu ni mali ya serikali, amelewa madaraka hakumbuki kuwa kiongozi yeyote ni sisi wananchi tumewaweka pale na wanawajibika kwetu.
Hawa walishajimilikisha nchi
 
Ingependeza sana iwapo ataondoshwa kwenye hiyo nafasi na kuwekwa mtu mwingine! Uongo, unafiki, uonevu, ukabila, ubinafsi, nk vifikie mwisho sasa.

Wanafanya aibu na wanaviburi vya madaraka

Wanajisahau sana kwamba sisi raia ndio mabosi wao.

Hawatujali
Hawafuati katiba
Hawatii viapo vyao.

Kwanini hawawajibishani? Ukweli wanatufedhehesha sana watanzania popote duniani tunaonekana useless na Vilaza zaidi kuliko mwanadamu yoyote ulimwenguni.
 
Raisi alilazwa tar 6 akatoka tar 7. Akazidiwa tar 14 mpaka tar 17 alipofariki. Majaliwa alisema hayo tar ngapi? Timeline inaweza kumuokoa, kama alisema baada check up ya tar 7 na kabla ya tar 14 alikua sahihi.
 
Raisi alilazwa tar 6 akatoka tar 7. Akazidiwa tar 14 mpaka tar 17 alipofariki. Majaliwa alisema hayo tar ngapi? Timeline inaweza kumuokoa, kama alisema baada check up ya tar 7 na kabla ya tar 14 alikua sahihi.
Ugonjwa wa moyo sio kama malaria hasa kwa mtu mzito kama rais wa nchi, huo ni uongo ...kwamba rais mpaka analazwa maana hiyo ni serious issue haiwezekan kabisa akalazwa Leo eti kesho aruhusiwe never, wametudanganya tena

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
Naamini kama ingewekwa wazi kuwa Rais anaumwa na akaombewa Mungu angesikia maombi yetu na kumponya. Mbona Lissu tulimwombea na akapona?

Wale waliosema Rais mzima na anaendelea kuchapa kazi hawa ndo wauaji/wachawi. Hebu fikiria una jirani yako ana mume anaumwa. Unamuuliza mr.funiko simuoni siku hizi yupo ok. Anakwambia mzima kabisa anachapa kazi.

Wakati wewe unaona kabisa kuwa kuna jambo linaendelea ndani.na mr.funiko si mzima. Kumbe ungeambiwa ugonjwa ungeweza shauri kuwa labda apige nyungu au awe anakula tangawizi na kunywa juice ya limalo kila wakati. Angepona.

Mficha Maradhi mauti humuumbua. Anapokuja fariki Mr. Funiko unadhani mshtakiwa wa kwanza ni nani? Ni yule aliyesema Mzee mzima na anapika mzigo kama kawa...unataka atoke aende wapi?akabebe zege ndo uamini?

Huyu mke ndo atakuwa mchawi kamuua mumewe ili ajipatie mali. Ndo maana hakutaka apone.

Wito wangu. Serikali kamata wote waliotoa habari za Uzushi kuwa Rais mzima kabisa hana tatizo.kamateni hawa muwatie ndani. Hawa ndo wamesababisha Rais Afariki..amekosa maombi yetu.

Mbona Lissu aliombewa na akapona?
 
Haya mambo yamekuwa kinyume sana.

Lisu tulikatazwa kumuombea ili afe ila tuliomba na hakufa.

Huyu tulihoji alipo na hali yake ikoje ili tumuombee, tukaonekana wabaya, mwisho wake ndio ikawa mwisho wa Awamu ya 5.

Waliotuninyima haki ya kujua Afya ya Rais wawajibishwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…