Waziri Mkuu, Majaliwa amuwakilisha Rais Samia kumjulia hali Lowassa

Waziri Mkuu, Majaliwa amuwakilisha Rais Samia kumjulia hali Lowassa

Hii huwa inaudhi sana, tukiwa viongozo tushughulike kwanza na maenwo yetu ya afya, maana huwa ni aibu sana kuona kiongozi wenu anafia nje ya nchi..

Mimi binafsi huwa inaniuma sana! Mfano Nyerere aliwapinga wazungu weeee mwishowe akafia kwao-aibu iliyoje?

Nashauri serikali ibadilishe lile eneo la Dege Kigamboni badala ya kufanyika mambo ya starehe bora iwe Hospital kubwa sana barani Afrika, ya kisasa, yenye kila aina ya Huduma, madaktari kutoka huko India wawepo pale na yaweza kutumika kama Health Tourism.

Waliosomea Cuba mtanielewa hapa!
 
Tuna urafiki na nchi za kijamaa ajabu wakiumwa wako na mabeberu aibu sana
 
Hisia zangu zinanipeleka kusiko kabisa kuhusu huyu mzee.

Anyway Mungu ampe siha njema
 
MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS SAMIA KUMJULIA HALI LOWASSA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa anayeendelea na matibabu Afrika ya Kusini.

Akizungumza na wanafamilia kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia, Waziri Mkuu amewasilisha salaam za pole kutoka kwa Mheshimiwa Rais na kusema Mheshimiwa Rais anafuatilia hali ya Mheshimiwa Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.

Waziri Mkuu ametoa salamu hizo leo (Jumatano, Desemba 28, 2022) jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambako alienda kumjulia hali Mheshimiwa Lowassa.

Kwa upande wake, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wanafamilia na namna ambavyo anafuatilia matibabu ya mpendwa wao.

Naye mtoto mkubwa wa Mheshimiwa Lowassa na Mbunge wa Monduli, Bw. Fredrick Lowassa amewashukuru Watanzania kwa maombi yao ya kumtakia afya njema baba yao.

View attachment 2461149
Lowasa sio wa kumuonea huruma hafai ameumiza wengi, sumu ya mwakyembe haitamuacha Karma is real acha ateseke unyama unyama tu.
 
January ni wa Makamba
Riziwani ni wa Kikwete
Fred ni wa Lowassa
Nape ni wa Moses Nauye
Lusinde na wa Job lusinde
Dr Mwinyi na wa Mzee Ruksa
Unasema ni ubinafsi?

Why ikusumbue kama waligombea na wakapigiwa Kura kama wengine?

Nape Hadi Baba yake kafa bado Yuko secondary...why umletee habari hizo...alimzuia Nani kugombea huko mtama? Masononeko mengine hayanaga hata akili....

Ndoto za watoto wote duniani kufata nyayo za Baba zao...sio wote wanaofanikiwa ....kama swala ni mtoto Tu bila kuangalia uwezo basi Membe angeweka mwanae wa kumzaa na sio kumuachia Nape
 
Inawezekana doctor anayemfuata ana jua historia ya mgojwa wake pia sababu nyingine inaweza kufuata mazingira yakiusalama
Ibireshwe kwa namna gani?hata sasa Muhimbili, KCMC,Bugando..hizo ni hospita nzuri tu na anaweza kutibiwa kiongozi yoyote,kiongozi ni mtu kama watu wengine,ila ni swala la kujiaminisha tu na kiburi cha pesa pia
 
Back
Top Bottom