Hii huwa inaudhi sana, tukiwa viongozo tushughulike kwanza na maenwo yetu ya afya, maana huwa ni aibu sana kuona kiongozi wenu anafia nje ya nchi..
Mimi binafsi huwa inaniuma sana! Mfano Nyerere aliwapinga wazungu weeee mwishowe akafia kwao-aibu iliyoje?
Nashauri serikali ibadilishe lile eneo la Dege Kigamboni badala ya kufanyika mambo ya starehe bora iwe Hospital kubwa sana barani Afrika, ya kisasa, yenye kila aina ya Huduma, madaktari kutoka huko India wawepo pale na yaweza kutumika kama Health Tourism.
Waliosomea Cuba mtanielewa hapa!