Waziri Mkuu Majaliwa: Hatutadharau ushauri, maoni na maeneo yenye hofu kuhusu makataba wa bandari

Waziri Mkuu Majaliwa: Hatutadharau ushauri, maoni na maeneo yenye hofu kuhusu makataba wa bandari

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
MAJALIWA: HATUTADHARAU USHAURI, MAONI NA MANENO YENYE HOFU KUHUSU BANDARI
---

Majaliwa.jpg
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania kwamba Serikali haitodharau maoni na ushauri wanaoutoa kuhusu maeneo yenye hofu kwenye mradi wa uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Majaliwa amewataka pia Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali pamoja na wawakilishi wao ndani ya Bunge kwani Serikali imejidhatiti kuhakikisha bandari inakuwa na ufanisi unaoendana na mahitaji ya sasa na kwa kuzingatia manufaa ya kijiografia ya Nchi yetu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumanne, Juni 20, 2023 katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 40 ya chuo cha International Evangelism Centre kilichoko Sakila jijini Arusha ambapo amesema bandari haijauzwa, bali Serikali inataka kubadilisha Muwekezaji ili iweze kuendeshwa kwa ufanisi na tija zaidi.

Majaliwa amesema wakati wa kuingia mikataba utakapofika Wataalamu wa uchumi nchini wataishauri Serikali kuhusu muda wa uendeshaji wa uwekezaji huo, hivyo amewataka Wananchi waendelee kuwa na subra.
 
The good news, to relieve all this gloom, is that a democracy is inherently self-correcting. Here, the people are sovereign. Inept political leaders can be replaced. Destructive policies can be changed. Disastrous mistakes can be reversed.
 
Hii ni taarifa nzuri sana. Uongozi wa watu maana yake ni kuwatumikia. Ili uwatumikie wakati flani na mahala mahala unao wajibu wa lazima wa kuwasikiliza. Kwa hali ya sasa Tanzania ni vema zikakafanyika juhudi za kuwasikiliza moja kwa moja unao waongoza kuliko kuwasikiliza kupitia wa wakilishi wao.

Baada ya kusema/kuandika hayo ziko tuhuma hawa Dp World walifukuzwa huko Yemen miaka ya nyuma kwa sababu ya mizigo kupungua sana kwenye bandari waliyokuwa wanaiendesha. Hapa vita ikatajwa ni kisababisho.

Hivyo Kwa nini wasiwe ndio walikuwa sababu ya kuchochea hiyo vita? Kwa nini isiaminiwe kuwa walikuwa wanafaidika na biashara za silaha na kutumia bandari hiyo ya Yemen kujitajirisha kupitia vita vya mnyewe kwa mnyewe. Kwa nini Tanzania isiwe na hofu kushirikiana nao?
 
Endel
Endeleeni tu kuendekeza huo ujinga money kama utawafikisha popote

Ukweli ni ukweli, na utabakia kuwa hivyo Dunia ya leo yoyote anayetaka kufanikiwa kiuchumi ni lazima afwate christian western economic system, hata Wachina waliacha Budhism na kufwata western leo hii ni Super power, Japan alifwata western christian economic system, hata Emirates na Gulf States zote waliacha Arabic culture na kufwata western christian economic system na ndio maana leo hii wamefanikiwa, hivyo hata sisi ili tufanikiwe hakuna njia nyingine isipokuwa western christian economic system, huo ni ukweli!
 
Back
Top Bottom