Waziri Mkuu Majaliwa: Hatutadharau ushauri, maoni na maeneo yenye hofu kuhusu makataba wa bandari

Waziri Mkuu Majaliwa: Hatutadharau ushauri, maoni na maeneo yenye hofu kuhusu makataba wa bandari

Screenshot_20230620-213327.jpg
 
Nimemsikiliza PM katoa sababu zinazofanya bandari isiwe na ufanisi. Kama hizo sababu ndio zimewafanya waingie mkataba wa aina hii. Basi na ijulikane hawa viongozi wetu wamechoka kutoa uongozi na wanaiona kazi ya uongozi kama ni karaha flani hivi kwao inayo wazuia kutanua na kula kwa mrija vile ambavyo wamesha jilimbikizia. Ufunuo wa Yohana 3:17

Mh Rais katika hotuba yake kaweka wazi makando kando ya Mamlaka ya Bandari hasa yale ya mifumo yake ya kiutendaji na yaliyo katika mkataba wa ujenzi wa meli 5.

Hii ni hatua kubwa ya kupambana na wabadhirifu wa mali ya umma kwa kuweka wazi matendo yao na moja ya nyenzo muhimu katika vita hii na aungwe mkono katika jitihada zake hizi mpya.
 
Karibia Tanzania tunaolewa na nchi za kiarabu
 
Western christian values zip ambazo ni Bora wewe,uchoko nao ni values??Qatar ameendesha world cup ya mfano kuwahi kutokea na kagomea christian values za kuadvertise ushoga waz waz,hayo kawaambia kwenu kwimba huko labda watakuelewa

Sasa Football world Cup ni Islamic au Arabic au Budhist? Football yenyewe mnayoishangilia ni mzao wa Christianity western, au unafikiri Football na sheria zake imeanzia Katar?
 
MAJALIWA: HATUTADHARAU USHAURI, MAONI NA MANENO YENYE HOFU KUHUSU BANDARI
===

Waziri Mkuu Majaliwa Leo akiwa anatoa elimu kuhusu bandari wakati wa kuhutubia waumini wakikristo katika sherehe ya miaka 40 ya kanisa la Internalional Evangelist Church, Amehimiza kuwasikiliza wananchi na umuhimu wa ushauri, maoni, na maeneo yenye hofu kuhusu bandari.
Kwa hili, Majaliwa ndiye kiongozi pekee aliyedhihirisha kuwa na akili timamu.
 
Kauli hii aliyotoa Waziri mkuu ambaye ndiye mtendaji mkuu na kiongozi wa shughuli za serikali bungeni imewadhihirisha wote wapiga debe, wanaotukana wanao hoji ubovu wa mkataba na hata wabunge waliopitisha azimio 100% kuwa ni watu wa hovyo na serikali imegundua kuwa lazima isikilize maoni ya hawa wanaopinga mkataba na kuboresha yaliyo muhimu.

Chawa na wapambe tena wengine wakiwa wasomi WAME AIBIKA.

9db5de04a6c74d4ab28fedf024324c5f_354827700_1299982727577428_6806552756679842962_n.jpg
 
MAJALIWA: HATUTADHARAU USHAURI, MAONI NA MANENO YENYE HOFU KUHUSU BANDARI
---

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania kwamba Serikali haitodharau maoni na ushauri wanaoutoa kuhusu maeneo yenye hofu kwenye mradi wa uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Majaliwa amewataka pia Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali pamoja na wawakilishi wao ndani ya Bunge kwani Serikali imejidhatiti kuhakikisha bandari inakuwa na ufanisi unaoendana na mahitaji ya sasa na kwa kuzingatia manufaa ya kijiografia ya Nchi yetu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumanne, Juni 20, 2023 katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 40 ya chuo cha International Evangelism Centre kilichoko Sakila jijini Arusha ambapo amesema bandari haijauzwa, bali Serikali inataka kubadilisha Muwekezaji ili iweze kuendeshwa kwa ufanisi na tija zaidi.

Majaliwa amesema wakati wa kuingia mikataba utakapofika Wataalamu wa uchumi nchini wataishauri Serikali kuhusu muda wa uendeshaji wa uwekezaji huo, hivyo amewataka Wananchi waendelee kuwa na subra.
Sipingi nia ya Serikali kubadilisha mwekezaji, ila napinga mkataba kati ya JMT na Dubai unaoipa DPW mamlaka ya bandari kuliko TPA na nchi kwa ujumla.

Huo mkataba wa IGA utupiliwe mbali na DPW iingie ubia na TPA au ipitie TIC kama wawekezaji wengine kwa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo. Mkataba wa IGA hata ukirekebishwa bado unakosa uhalali kwani Serikali tayari ina chombo (TPA), kilichoundwa kisheria na kupewa mamlaka ya kuendesha na kuendeleza bandari kinachoweza kuingia ubia na mwekezaji yeyote mwenye sifa
 
Hawampendi Majaliwa lkn ndiyo mtu pekee sober kwenye hiyo serikali yenu, halafu Majaliwa ana western Christian values, yuko vizuri basi tu!
Nusu ya mstari inaeleweka; nusu iliyobaki ni kama imeandikwa na mtu tofauti kabisa wa ile iliyoandikwa mwanzo!
Hicho ndicho kiasi cha kuchanganyikiwa baadhi ya waTanzania walichofikia wakati huu!

Inatisha sana.
 
Sipingi nia ya Serikali kubadilisha mwekezaji, ila napinga mkataba kati ya JMT na Dubai unaoipa DPW mamlaka ya bandari kuliko TPA na nchi kwa ujumla.

Huo mkataba wa IGA utupiliwe mbali na DPW iingie ubia na TPA au ipitie TIC kama wawekezaji wengine kwa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo. Mkataba wa IGA hata ukirekebishwa bado unakosa uhalali kwani Serikali tayari ina chombo (TPA), kilichoundwa kisheria na kupewa mamlaka ya kuendesha na kuendeleza bandari kinachoweza kuingia ubia na mwekezaji yeyote mwenye sifa
Nia ya IGA tayari imekwishaonesha ni nia ovu. Sioni ni kwa namna gani inaweza kurekebishwa ionekane kuwa yenye nia njema.

Hii IGA itupiliwe mbali moja kwa moja.
 
Magufuli yuko ofisni anachapa kazi na anawasalimia sana, kumbe yuko mortuary, why believe this man?
Ulitaka aseme magu kafariki ghafla bila wananchi kuandaliwa kisaikolojia , uongozi ni hekima sio kuropoka ovyo
 
Endelea kumwamini tu Matajario sijui majaliwa! Huyu jamaa ni wa kumpuuza. Tangu atuambie kuwa jiwe yupo na afya tele na anachapa kazi, sitakaa nimwamini tena matarajio
ACHA upuuzi ww ,Yule alikuwa mkuu wa nxhi huwezi kutangaza kifo chake ghafla TU , lazima uandae mazingira ambayo hayataleta tafaruku
 
Back
Top Bottom