Waziri Mkuu Majaliwa: Hatutadharau ushauri, maoni na maeneo yenye hofu kuhusu makataba wa bandari

Huo mkataba magufuli asingethubutu kuingia kichwa kichwa
 
Mkataba ungekuwa unasema hivyo kama anavyosema waziri mkuu Kassim Majaliwa tusingelalamika.

Sasa hivi ufafanuzi unatolewa mwingine na mkataba unasema mengine, sisi watanzania hatutasikiliza chochote ambacho hakipo kwenye mkataba ,yatakuwa ni matumizi mabaya ya masikio yetu.
Hata chifu Mangungo wa Msovera alipewa maelezo mazuri sana

Kuna gunduzi nyingi sasa hivi kama magari ya kutumia umeme, gesi na mwarabu anategemea mafuta kwa hiyo walishaona mbali sana ndiyo maana ya mikataba ya milele.

Next generation biashara ya mafuta inaweza kuja kuwa ya kawaida sana lzm waandae pa kukimbilia
Waziri MKuu kaongea kwa uzoefu wa kazi wa miaka sita hapo bandarini. Huyu ni sehemu ya uongozi wa JPM tena mtu muhimu sana anayajua mengi kuliko wewe uliyekuja na fitina na pengine umeshavuta pesa ya hawa mafisadi wa bandarini.
 
Wewe ndo huelewi unachokiandika au hujamuekewa mleta mada.Iko hivi waziri mkuu kaongea maneno mazuri..tunataka hayo maneno mazuri yawe kwenye mkataba..sio jukwaani..mbona kitu kiko clear kabisa hiki...
 
Viongozi wetu wanajiongelea tu kama vile hawaishi nchi hii.
 
Wewe ndo huelewi unachokiandika au hujamuekewa mleta mada.Iko hivi waziri mkuu kaongea maneno mazuri..tunataka hayo maneno mazuri yawe kwenye mkataba..sio jukwaani..mbona kitu kiko clear kabisa hiki...
Mkataba kuuelewa pia inahitaji utulivu. Mkataba Mama ni kwa ajili ya kupelekwa na kupokelewa bungeni.

Mikataba ya kiutendaji ya kibiashara ndio yenye uwazi wa mijadala kati ya wawekezaji na wadau wanaokwenda kufanya nao biashara.

Kumbuka kuwa hao DPW itawabidi wasajiliwe na BRELA hivyo watalazimika kuyatii matakwa ya wafanyabiashara wetu.

Watu wengi wanausoma mkataba uliokwenda bungeni na kuuogopa wakidhani ndio utakaokuwa ukitumiwa katika shughuli za kibiashara za kila siku.
 
Mkuu kwa hiyo unataka kusema huo mkataba uliopelekwa bungeni hauna maana/impact/ influence kwa mkataba wa kibiashara utakaosiniwa??Mkataba uliopelekwa bungeni ni wa kuruhusu majadiliano ya kuelekea mkataba mwingine- then fine...lkn kwenye huu mkataba wa kuruhusu mazungumzo tayari pande mbili zimeishatoa matwaka yao ambayo pia ndo kama preliminary kwa ajili ya huo mkataba wa kibiashara unaousema wewe?

Sitaki kuamini kuwa serikali ilisubmit bungeni andiko lisilo na maana yoyote au uhisiano na mkataba utakaoandikwa...
 
Kilichopelekwa bungeni ni agreement to agree kitu kama MOU ni wa jumla. Hii mikataba inayokwenda kuandikwa kati ya wawekezaji na wafanyabiashara wazalendo ndio ya muhimu kwani ikitokea kutokuelewana kibiashara kati ya pande hizo mbili ule uliopelekwa bungeni automatically unakuwa hauna kazi tena.

Mfano mkataba wa kibiashara kuhusu masuala ya TEHAMA umesainiwa kati ya DPW na wazalendo, pakatokea sintofahamu kati ya pande hizo na wakaamua kusitisha biashara, maana yake na ule uliopelekwa bungeni unakuwa hauna kazi tena.
 
Cha kwanza ndugu Waziri Mkuu, Hakuna mkataba wa maisha hapa Duniani isipokuwa ndoa zetu za kikristo tu. kwa hiyo futeni hicho kipengele kwanza ndipo turudi kwenye makabrasha kwa vipengele vingine kama tukikorofishana na hawa jamaa basi kesi iende kimataifa SA badala ya Kisutu.
 
Kilichopelekwa bungeni ni agreement to agree kitu kama MOU ni wa jumla. Hii mikataba inayokwenda kuandikwa kati ya wawekezaji na wafanyabiashara wazalendo ndio ya muhimu kwani ikitokea kutokuelewana kibiashara kati ya pande hizo mbili ule uliopelekwa bungeni automatically unakuwa hauna kazi tena.

Mfano mkataba wa kibiashara kuhusu masuala ya TEHAMA umesainiwa kati ya DPW na wazalendo, pakatokea sintofahamu kati ya pande hizo na wakaamua kusitisha biashara, maana yake na ule uliopelekwa bungeni unakuwa hauna kazi tena.
Unanichanganya ujue??? Sasa kwenye hiyo MOU kwann waseme hakuna kujitoa kwa sababu yeyote??
Kwann mahakama za tanzania zisiwe na nguvu juu ya changamoto zitakazojitokeza??
Nieleweshe kwamba vimewekwa kwa maana gani katika uo ujumla unaousemea??
 
Unajichanganya mwenyewe mkuu jayaron. Hawawezi kuongelea kujitoa kwenye mkataba uliokwenda bungeni kwani zipo biashara nyingi za ubia kati ya mwekezaji na wazalendo.

Mambo ya mahakama kuwa na nguvu ungewasiliana na taasisi hizo ujue kwanini.

Sio mara ya kwanza kwa mikataba kuja katika namna huu ulivyokuja.
 
MAJALIWA: HATUTADHARAU USHAURI, MAONI NA MANENO YENYE HOFU KUHUSU BANDARI
---

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania kwamba Serikali haitodharau maoni na ushauri wanaoutoa kuhusu maeneo yenye hofu kwenye mradi wa uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Majaliwa amewataka pia Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali pamoja na wawakilishi wao ndani ya Bunge kwani Serikali imejidhatiti kuhakikisha bandari inakuwa na ufanisi unaoendana na mahitaji ya sasa na kwa kuzingatia manufaa ya kijiografia ya Nchi yetu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumanne, Juni 20, 2023 katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 40 ya chuo cha International Evangelism Centre kilichoko Sakila jijini Arusha ambapo amesema bandari haijauzwa, bali Serikali inataka kubadilisha Muwekezaji ili iweze kuendeshwa kwa ufanisi na tija zaidi.

Majaliwa amesema wakati wa kuingia mikataba utakapofika Wataalamu wa uchumi nchini wataishauri Serikali kuhusu muda wa uendeshaji wa uwekezaji huo, hivyo amewataka Wananchi waendelee kuwa na subra.
Huyo muongo wa Taifa msimwamini, hata kipindi cha magufuli akiwa kwenye coma alijitokeza na kusema tunataka tumuone kariakoo au magomeni huyo naye mpuuzeni ni jitu la hovyo kabisa ila Mungu amelichelewesha kulishughulikia.
 
Unajichanganya mwenyewe mkuu jayaron. Hawawezi kuongelea kujitoa kwenye mkataba uliokwenda bungeni kwani zipo biashara nyingi za ubia kati ya mwekezaji na wazalendo.

Mambo ya mahakama kuwa na nguvu ungewasiliana na taasisi hizo ujue kwanini.

Sio mara ya kwanza kwa mikataba kuja katika namna huu ulivyokuja.
makuwadi na madalali ya matapeli warabu tuyapinge kwa nguvu zetu zote.
 
Hebu nipe mfano wa mikataba ya aina tuliyokua nayo nchini?
 
makuwadi na madalali ya matapeli warabu tuyapinge kwa nguvu zetu zote.
Utapeli ni uelewa wako binafsi kuwa mdogo kiasi cha kuhisi unaibiwa.

Tatizo la uelewa mzima kuwa mdogo ndio ukuwadi wenyewe huo unaouongelea.

Rwanda na DRC wameshaini mikataba ya kibiashara, hapa bongo tunadanganywa na siasa za waarabu, siasa za kuibiwa mali zetu.

Wenye haki ya kuona wanaibiwa ni DRC nchi tajiri sana yenye kila aina ya madini huko ardhini.
 
Back
Top Bottom