Waziri Mkuu Majaliwa, pokea makadirio yangu kibanda cha VETA Tabora

Asante

Mie umenifundisha

Fascia board sie twaita Fisha bodi
Murram twaita Molam

Mengine sielewi ila hayo ni somo kwangu
 
Populist........Cheap politics...Huyu Majaliwa hafai kabisa. Hiyo bei ni sawa kabisa kwa mjengo wenye viwango. Kama anataka madarasa ya shule za KATA hiyo nyumba unaweza kuijenga hata kwa laki 3. Ila ikichukuliwa na upepo usimuulize mjengaji.

Tatizoni kwamba, hilo jengo likianguka kwa Mvua kali, ataitwa mhandisi ajieleze. Ni ujinga mtupu.

Ipo hivi ndugu zangu watanzania, nyumba hiyo hiyo unaweza kuijenga kwa milioni 1 mpaka milioni 11- kutokana na kiwango. Kama serikali inataka tujenge nyumba zake kwa kiwango cha KATA, Tutakwisha. Cheap is expensive- ukiuelewa usemi huu utajua kuwa huyu majaliwa ana CHEAP POLITICS..Sitaki hata kumsikia.
 
Eti muweke ndani huyu.. kwa kisa gani. tumerudi nyuma wakati wa mwendazake. Si angesema tu wamhoji kwani huyo engineer atatorokea Kenya au... wakati ana BOQ ya jengo. Aitwe akahojiwe lakini si kumuweka ndani.. Ujinga mtupu..
Tunarudi wakati wa ujima.
 
Kuna BOQ hapo au ujinga wa mtu mwizi!
Hujajenga ndugu yangu, nakuonea huruma. Ushauri: Utapotaka kujenga, usimpe pesa ndugu yako akusimamie mjengo- mtagombana na kumuita mwizi. Kajenge mwenyewe mpaka finishing kwa viwango ndio urudi hapa JF utoe maoni.
 
Hujajenga ndugu yangu, nakuonea huruma. Ushauri: Utapotaka kujenga, usimpe pesa ndugu yako akusimamie mjengo- mtagombana na kumuita mwizi. Kajenge mwenyewe mpaka finishing kwa viwango ndio urudi hapa JF utoe maoni.
Kumbe na wewe ni mpumbavu! Unataka mpaka nikuweke ndani unipakulie ndiyo ujue nina jengo!
 
Hujajenga ndugu yangu, nakuonea huruma. Ushauri: Utapotaka kujenga, usimpe pesa ndugu yako akusimamie mjengo- mtagombana na kumuita mwizi. Kajenge mwenyewe mpaka finishing kwa viwango ndio urudi hapa JF utoe maoni.
Mkuu kuna mijitu mijinga humu mtandaoni, hata unashangaa anajuaje kuwasha mtandao maana vichwani hakuna kitu
 
Kibaya zaidi huyu wanayemzungumzia sio mkandarasi bali ni mwalimu aliyebebeshwa jukumu la kusimamia mradi chini ya mfumo mbovu wa fosi akaunti!

Amandla...
 
Sizungumzii jengo bali jengo la viwango.
Na unapozungumzia viwango vya jengo pia angalia matumizi yake! Viwango vya jengo viendane na viwango vya matumizi!

Kilichotakiwa kujengwa ni kibanda (hut or shelter) na siyo nyumba (house)!
 
Amekiri wapi? Liliulizwa swali katika kadamnasi kuhusu bei ya hicho choo na mtu akasema 40000. Hamna mahali ambapo huyo unayemuita mjenzi amekiri chochote.

Amandla...
Maswali yameulizwa Tena mengi kuhusu choo.
Watu msio na akili za kutosha, mmepewa mahesabu ili mupitie na kusahihishaujenzi wa jengo mnalotaka , mmekalia kuchonga kama hamna akili nzuri!
Lete mkadirio yako, nyumba za kerikali hazijengwi kwa maneno matupu.
Tatizo lako umekurupuka.
Jengo ni jengo liwe ya serikali, la kanisa , la Msikiti , hata nyumba ya kuishi ya mtu binafsi.

Kanuni za ujenzi nizilezile hazibaldiliki isipokua kwa mazingira maaluum.

Hayo mahesabu ni yakwako na hu yo mwenzako sio lazima ni yakubali.
Kama unataka tuboshane kimahesabu leta Bill of quantity ya hicho kibanda.
 
Asante kwa estimate ya gharama za Nyumba ya mlinzi. Kwa kweli bila estimate unaweza kusema ndivyo sivyo.
Lakini ndugu, S.No. 17 kwenye estimate hii umeweka IT4 za mita 3.4 na idadi ni 38 kwa gharama ujenzi ya 65,000. Hii imefanya nirudi kuangalia mkao wa nyumba ya mlinzi.
Naona kama idadi ya bati 38 za mita 3.4 ni nyingi sana. Naomba ufafanuzi maana tunajifunza pia!!.
 
Amekiri wapi? Liliulizwa swali katika kadamnasi kuhusu bei ya hicho choo na mtu akasema 40000. Hamna mahali ambapo huyo unayemuita mjenzi amekiri chochote.

Amandla...
Nikweli swali limeuliukizwa kwenye kadanamnasi jibu jibu limetokewa ni , Asian. Je Asian inauzwa 300,000
? Jamani, hata kama mnamtetea mwana taaluuma mwenzenu sio hivyo . Angesema kaweka European hata kwa 1,000,00tsh ningekubali haraka, lakini kwakukili ni Asian , hiyo ni 40,000 .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…