Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepiga marufuku tabia ya waganga katika hospitali za serikali kuwaandikia wagonjwa dawa na kuwaelekeza kununua dawa hizo katika maduka ya dawa ya watu binafsi wakati Serikali imetoa dawa za kutosha kwenye zahati,vituo vya afya na hospitali za Wilaya.
Ametoa marufuku hiyo Machi 25,2025 wakati akihutubia wananchi wa Usangi Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi aliyoifanya mkoani humo, ambapo ameeleza kuwa Serikali hutoa kiasi cha shilingi milioni 65 kila mwezi kwaajili ya kununua dawa katika Zahanati, vituo vya afya na hospitali ya Wilaya ya Mwanga hivyo hatarajii kusikia dawa zinakosekana na kupatikana katika maduka ya watu binafsi.
"Milioni 65 zinazotelewa na Serikali ili kununua dawa katika zahanati na vituo vya afya na zinatosha kwa kila mwezi kwa miezi mitatu mitatu ili wananchi watibiwe, hivyo dawa zipatikane" Majaliwa
Aidha amemtaka Mganga Mkuu wa Wilaya kuacha kununua dawa ambazo kwa asili ya mazingira yao hakuna magonjwa hayo badala yake wanunue madawa ambayo mara nyingi magonjwa yake hujitokeza kwa utafiti waliofanya na siyo kuelekeza wananchi kununua dawa kwa watu binafsi.
"Tunataka kila mtu apate huduma za afya katika maeneo yake bila kujali hali yake na tumeshatoa magari matatu ya wagonjwa yaliyoombwa na mbunge wenu Joseph Tadayo ili kubeba wagonjwa na kuwapeleka katika hospitali ya wilaya pamoja na gari moja la uratibu wa afya" Majaliwa.
Aidha ameitaka halmashauri hiyo kuanza kujenga zahanati kwa kutumia mapato yao ya ndani kutokana na miradi yote kupata fedha kutoka Serikali kuu hivyo ni wakati wao wa kujenga zahanati kwa Wananchi na kufanya tathimini ya umbali wa vijiji na wapi waanze napo.
"Tunajua tuna upungufu wa watumishi na Rais Samia ametoa vibali vya ajira watumishi sekta ya afya ili kuongeza idadi ya waliopo na huduma za afya ziweze kuendelea na hivyo waganga wa sekta ya afya wataongezwa katika wilaya hii baada ya kutembelea waganga 156 kupangwa katika wilaya hii" Majaliwa
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mwanga Joseph Tadayo ameishukuru Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za maendeleo ikiwa ni pamoja na nia ya kukamilisha mahitaji yote muhimu ya maendeleo katika jimbo hilo ikiwemo sekta ya elimu, afya na miundombinu ya barabara.