Hivi karibuni PM ametoa kauli ya ajabu ambayo haitarajiwi kutolewa hata na mjumbe wa nyumba kumi:
Majaliwa anadai kuwa watanzania ambao wamemaliza vyuo vikuu na hawana ajira, wakajiunge na VETA ili wajiajiri! Hiki ni kioja kikubwa!! Yaani mechanical engineer akajiunge VETA ili akawe fundi mchundo. Civil engineer aende VETA ili awe fundi mwashi!! Processing engineer aende VETA ili akawe mhudumu wa hoteli. Accountant aende VETA ili akawe fundi cherahani.
Kwa aina ya viongozi wa namna hii, tutarajie kauli nyingi za kushangaza.
Sitashangaa siku madaktari watakaposema wamekosa ajira, Majaliwa akawaambia waende vijijini wakawe wakunga wa jadi!! Kwa sababu kwa Majaliwa, mgawanyo wa majukumu kwake ni somo ambalo hakuwahi kulielewa.
Yaani kama mtu anataka kuwa fundi mwashi, kwa nini apoteze muda wake wote, akasome high school au diploma, kisha aende mpaka university, wakati angeweza kujifunza kuwa fundi mwashi mara baada ya kumaliza darasa la saba? Kuna sababu gani mtu apoteze muda zaidi ya miaka 10 masomoni halafu aje kuwa bodaboda au fundi mchundo wakati angeweza kuwa kwenye nafasi hizo bila ya kwenda chuo chochote? Mhitimu wa university anaweza kufanya hizo kazi kama sehemu ya kujikimu kwa kuwa Serikali na jamii, wameshindwa kumpa hifadhi stahili kufuatana na uwezo na utaalam wake. Hiyo ndiyo sababu baadhi ya mataifa, huamua kuwapa watu wa namna hii pesa ya kujikimu, kwa sababu siyo kosa lao.
Kule Australia, mtu akiwa anataka kazi, halafu akaikosa, alipojiandikisha kuwa anatafuta kazi lakini hajapata, anaanza kupewa subsistence allowance ya dola600 kwa mwezi. Siku ikipatikana kazi, akataarifiwa, ikatokea yeye akasema haitaki hiyo kazi, ndipo ile subsisitence inafutwa. Yote hiyo ni kwa kutambua kuwa anayetaka kufanya kazi, akashindwa kupata kazi, tatizo ni Serikali na jamii, siyo tatizo lake pekee yake.
Kujiajiri siyo kazi rahisi, ndiyo maana unawakuta akina Majaliwa mpaka leo wanahangaika kuwa wabunge, licha ya ukweli kuwa hawana chochote cha maana wanachoweza kuchangia katika kuleta mabadiliko chanya kwa Taifa.
Viongozi hawa wa iana ya akina Majaliwa, utawasikia kila mara wakisema kuwa Watanzania wengi wamejiajiri, wakati ni uwongo mkubwa, wanasema hivyo ni kwa sababu hawaelewi maana ya ajira. Maana ya ajira ni kuwa na mapato ya uhakika yanayotabirika. Mwendesha boda ambaye mwezi huu anapata laki 3, mwezi ujao anapata zero kwa sababu pikipiki yake imeharibika, mwezi unaofuata anapata laki 1, huyu hajajiajiri wala hana ajira, bali ni mgangaikaji.
Ili ujiajiri unahitaji vitu vitatu vikubwa:
1) mtaji
2) Ujuzi na uzoefu
3) Network.
Akina Majaliwa wana mitaji, wana uzoefu wana networks, lakini wameshindwa kujiajiri, badala yake wamefanya uongozi kuwa ni ajira yao, LAKINI wanawataka wahitimu wa vyuo wajiajiri wakati hawana mitaji, hawana uzoefu isipokuwa ujuzi nadharia, wala hawana networks.
NB. Poleni sana vijana, na ninawahakikishieni vijana wengi, hakuna mwanga wala matumaini chini ya CCM. Kuondoka mahali mlipo ni lazima kuunganisha nguvu kuiondoa CCM ambayo ni kikwazo kikubwa cha kubadilisha mifumo ya utawala na uongozi ili Taifa liongozwe kwa mifumo inayoruhusu ubunifu na utumiaji wa fikra mbadala katika kuliondoa Taifa kutoka kwenye mkwamo mkubwa wa maendeleo halisi. Lakini siku zote tufahamu kuwa ni rahisi sana kumwondoa kiongozi mzuri kuliko kumwondoa kiongozi mbaya. Kiongozi mbaya huwa yupo tayari hata kuua ili aendelee kushikilia madaraka. Kiongozi mbaya huwa ana hofu ya kuondoka kwani siku akiondoka, mabaya yake yatakuwa wazi. Kwetu Tanzania CCM ndiye kiongozi mbaya, na ndiye kizingiti kikubwa cha ustawi wa Taifa.