Shida ni kuwa hata hao wa VETA watakuwa wengi sana, kama hakuna viwqnda twaitegemea China tatizo litaendelea kuwepo
VETA haimaanishi ukaajiriwe viwandani, bali ujiajiri, Fundi gereji, umeme, kutengeneza machine ndogo ndogo, fundi cherehani etc.

Leo magari Ya umeme yakija kutoka China nani atayatengeneza? Ukienda mjini CBE pale badala kuleta mashuka toka Nje vinakuja Vitambaa mafundi wengi wa Charahani wametoboa pale same kwa kariakoo. SIDO Kuna vimachine vidogo vidogo kibao wanatengeneza, Machine za kukoroga, kupasha moto etc
 
Kaongea vzuri, lakin hata asingeongea vijana wanajipambania kivyao vyao na kama vyuo vya VETA wanavijua viliko.

Maana hata vyuo walivyoenda kusoma hakuwaambia yeye bali wienda kimpango wao na struggle za wazaz wao.
Hivyo vijana kuna vitu wanahitaj kuambiwa na serikali ila sio hilo alolisema PM maana hata huko kwenye vijiwe bhangi wanaambiwaga.

Vijana kazen kivyenu vyenu wala msikate tamaa najua waliopanga mfumo wa elimu ndo wanawasimanga leo kwamba ni mfumo wa kijinga and that is the big betrayal.
Be strong msiogope kudharaulika wala kifo. Msiichukie nchi yenu kwasababu yoyote your motherland will never dump at all.

Ila viongoz wakifa msifurah, ila mtaamua mlie au iwe kama sio msiba wa viongoz wenu, kwakuw mnamsiba wenu wakat wote, na huo msiba wenu haukuwagusa wao pia.
 
Tatizo ni kwamba wanaosema hivyo wanakinzana na maleongo yao ya kuwa dona kantri.
Wao waseme hivyo alafu waseme kabisa sera ya nchi ni kuwa wapokeaji wa misaada.

Alafu uliona wapi nchinikaendelea kwa kauli za namna hii bwana. Baadae wazungu wakianza kutunyanyasa tunalalamika wakati tunayataka wenyewe
 
Mkuu mara nyingi toka tupate uhuru tumedanganywa kwa hila.
Nakumbuka viazi hao wakituambia 1960 tukipata uhuru hadi chooni tutawekewa barabara za rami nchi nzima.
Kumbe ni njia ya kumtoa mkoloni mweupe na kuleta mkoloni mweusi.
Kumbe hao tuliowakabidhi nchi walikuwa hawana basic skills za kuongoza hata kijiji.
Ila kwa sasa hatuwezi kuwalaumu wakoloni weupe kwani tuna zaidi ya miaka 50 ya amani.
Tatizo ni nini?
 
Tatizo waafrika wanawaza kwa kutumia matako baadala ya akili
 
Aonyeshe mfano yeye na wategemezupi wake
 
Tutasoma huko VETA bure?
Tatizo pesa mkuu
 
nia ya Mh.Waziri Mkuu ni vijana kujiongeza ili kufikia malengo yao katika maisha, in five years to come hali itakuwa mbaya sana kwa graduate, POVERTY IS THE LACK PRODUCTIVITY, YOU CAN NOT BE PRODUCTIVE IF YOU HAVE NO KNOWLEDGE, WHERE TO FIND KNOWLEDGE ? Ndio huko VETA, BAKITA, SIDO
 
Wanajamvi Heshima kwenu,

Kwako Mh Dr Samia Suluhu Hassan Rais wetu mpendwa.

Nakuandikia kwa heshima na taadhima kuhusu kauli tata, aliyoitoa waziri Mkuu Majaliwa huko Tabora, kuwataka vijana wasomi wa vyuo vikuu kujiunga na vyuo vya VETA Kusomea ufundi wa fani mbalimbali.

Kwa upeo wangu wa kutafakari mambo naona Waziri Mkuu amevuka mstari,kwa kauli aliyoitoa.
Ni kauli

Mosi ya kudharau kada mbalimbali zilizosomewa na vijana chuo KIKUU mpaka kuwataka waziache.

Kada kama uhasibu, uhandisi ,Udaktari, Ujiolojia,ualimu, Procurement kuzitaja chache.

Watu hao juu wametumia muda mwingi,pesa kusoma kidato Cha kwanza mpaka Cha sita, Kisha miaka mitatu mpka minne chuo KIKUU.

Hili ni group kubwa la wanazuoni ambao wapo mtaani hawana ajira,walipokuwa wanasoma walikuwa na malengo yao,

Walijua kabisa VETA zipo, ukweli kuhusu VETA ni kada ya kati ya kawaida iliyokuwa na malengo ya kutoa skills study kwa ajili ya kujiajiri, kwa namna ya pekee watu ambao waliishia darasa la saba zamani, lakini sasa kidato Cha nne, ambao hawakuweza kuendelea na masomo ya juu ili wajiajiri.

Mh Rais mashaka yangu ni kuwa Kuna ombwe kubwa la ajira nchini, safari hii wapiga kura wengi nchini ni vijana, ambao hawana ajira.

Kwa Nini kauli kama hii inatoka kuelekea uchaguzi mkuu?? sio nzuri, itachochea chuki kwa vijana wasio na ajira ambao Bado wana matumaini na serikali Yako.

Kwa namna ilivyo vijana hao wamekuwa underrated, hadhi ya degree za vyuo vikuu ni bure, haina maana, mpaka leo hii vijana hao washauriwe kusomea ufundi🤔🤔🤔

Mwisho Mwishoni natamani Waziri Mkuu ajitafakari, na Mama kama mkuu wa nchi utafakari hii kauli tata, ambayo kwangu mimi kama mtanzania inatosha kwa Waziri Mkuu kukaaa pembeni baada ya Bunge kuvunjwa.

Ni imani yangu ujumbe huu utafika mezani kwako, kwa wewe mwenyewe kusoma, au kupitia wasaidizi wako.

Nandagala One -Mpumalanga South Africa.
 

Attachments

  • IMG-20250312-WA0024.jpg
    68.3 KB · Views: 1
Wala hajamchonganisha, you know soko la ajira window ya degree ni ndogo sana, mlango uliopo ni technicians, most of them wakitokea veta

As ajira hata US huku tulipo, vijana wana opt trade skills (technical skills) kuliko degree, na trend imeanza kukua kwa kasi sana.
Ni mfano mdogo but that the reality
 
Hujasema kitu, hapo wasomi wanatakiwa waamue kwa utashi wao binafsi, sio kutoa general advice, hiyo ni dharau kubwa sana kwa wahitimu wa vyuo vikuu, ni kauli ambayo imetolewa bila tafakuri kubwa!!!
 
Kwakuwa PM naye ni mwalimu, kauli yake ipo ndani ya taaluma yake.... naiheshimu, ila nakubaliana naweza kaitoa wakati usio sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…