Wanajamvi Heshima kwenu,
Kwako qMh Dr Samia Suluhu Hassan Rais wetu mpendwa.
Nakuandikia kwa heshima na taadhima kuhusu kauli tata, aliyoitoa waziri Mkuu Majaliwa huko Tabora, kuwataka vijana wasomi wa vyuo vikuu kujiunga na vyuo vya VETA Kusomea ufundi wa fani mbalimbali.
Kwa upeo wangu wa kutafakari mambo naona Waziri Mkuu amevuka mstari,kwa kauli aliyoitoa.
Ni kauli
Mosi ya kudharau kada mbalimbali zilizosomewa na vijana chuo KIKUU mpaka kuwataka waziache.
Kada kama uhasibu, uhandisi ,Udaktari, Ujiolojia,ualimu, Procurement kuzitaja chache.
Watu hao juu wametumia muda mwingi,pesa kusoma kidato Cha kwanza mpaka Cha sita, Kisha miaka mitatu mpka minne chuo KIKUU.
Hili ni group kubwa la wanazuoni ambao wapo mtaani hawana ajira,walipokuwa wanasoma walikuwa na malengo yao,
walijua kabisa VETA zipo, ukweli kuhusu VETA ni kada ya kati ya kawaida iliyokuwa na malengo ya kutoa skills study kwa ajili ya kujiajiri, kwa namna ya pekee watu ambao waliishia darasa la saba zamani, lakini sasa kidato Cha nne, ambao hawakuweza kuendelea na masomo ya juu ili wajiajiri.
Mh Rais mashaka yangu ni kuwa Kuna ombwe kubwa la ajira nchini, safari hii wapiga kura wengi nchini ni vijana, ambao hawana ajira.
Kwa Nini kauli kama hii inatoka kuelekea uchaguzi mkuu?? sio nzuri, itachochea chuki kwa vijana wasio na ajira ambao Bado wana matumaini na serikali Yako.
Kwa namna ilivyo vijana hao wamekuwa underrated, hadhi ya degree za vyuo vikuu ni bure, haina maana, mpaka leo hii vijana hao washauriwe kusomea ufundi🤔🤔🤔
Mwisho Mwishoni natamani Waziri Mkuu ajitafakari, na Mama kama mkuu wa nchi utafakari hii kauli tata, ambayo kwangu mimi kama mtanzania inatosha kwa Waziri Mkuu kukaaa pembeni baada ya Bunge kuvunjwa.
Ni imani yangu ujumbe huu utafika mezani kwako, kwa wewe mwenyewe kusoma, au kupitia wasaidizi wako.
Nandagala One -Mpumalanga South Africa.