Waziri Mkuu Majaliwa: Wenye degree kasomeni ufundi VETA mjiajiri
Kuambiwa mkasome VETA na degree zenu ndio povu liwatoke namna hii?
Screenshot_20250314-075844.jpg
 
Toka magetoni ,acha akili mgando . Mimi ni CPA, mwajiriwa wa serikali ,pia nimejiajiri(consultant )lakini ni mtaalamu wa rangi na napenda rangi kuliko uhasibu na nilisoma veta.Nakumbuka mmoja ya walimu wangu BUSARA aliniambia unachokifanya nje ya mshahara ndio utajiri ,veta imenisaidia .
Kwa akili yako unataka kusema Tanzania waliosomea fani mbali mbali wanazo ajira?au wamejiajiri?
Kama nchi tufike wakati tuwe Sirius na maisha ya watu tuwe na mipango mirefu kwa maendeleo ya watu wetu.
Bado tunao vijana wengi wmemaliza veta nao hawana mitaji hawana kazi za kujipatia kipato.
 
Kassim Majaliwa kiufupi umeshajipotezea heshima na heshima uliyobaki nayo ni ndogo Sana.

Nakushauri Ujifunze kukaa Kimya hakuna faida utaipata baada ya kuwa mropokaji.
Watu wengi tunaona kuhusu VETA ni kitu kibaya lakini kuna nchi kama China wenzetu ni kawaida sana mtu mmoja kujua vitu viwili au vitatu.Degree ni elimu lakini maendeleo ni kitu kingine.Wapo watu walishafanya hivyo kitambo na wanafurahia kufanya waliyojifunza veta
 
Mbona ni kauli yenye kujenga, sema watu kutaka makubwa, na ni kwakuwa hiki ni kipindi cha uchaguzi basi kila kauli itajadiliwa... Simple kama unaoana umesoma na bado degree haijaweza kukutoa ulipo...

Piga kozi za veta kuna mawili aidha ujiajiri ama uajiriwe kwa level ya chini... Sababu huku level ya chini possibility ya kupata ajira ni kubwa kuliko level ya juu

We unahisi ukisoma kozi ya ufundi umeme, huwezi pata hata kazi ya kupiga wiring kwenye majengo?

au kozi ya kuchomelea, huwezi pata fursa ya kutengeneza mageti?
Inamaanisha Tanzania haijafikia kiwango cha kuhudumiwa na watu wenye Degree?

Inahitaji watu wa VETA tu?
 
Habari!
Elimu ya VETA tunaweza kuiita elimu ya kati. Wakufuzi wake ni wahitimu wa elimu za juu. Wapo pia wakufuzi wenye elimu ya kati, nawafahamu.
Bahati mbaya kauli ya Majaliwa haijawataja hao wenye degree anataka waenda VETA ni degree za fani gani, na je, nini hatma ya elimu yao ya degree.
Huko VETA wakasome kozi za mda gani? Kwa lengo gani? Nani atagharamia ada na mahitaji mengine na nini hatma ya elimu yao ya VETA ikiwa hatma ya degree zao haijapatikana?
Mh. Samia usiogope gharama ya kuvunja bunge kwa kumtimua huyo Mh. Majaliwa.
Majaliwa ni jirani yangu huko Lindi ila kwenye mambo ya kitaifa Mimi sina jirani. Timua kabisa ili kuwepo na funzo kwa viongozi wengine waache kuongea kwa misisimko.

NJE YA MADA
Kama kuna mtoto wa Kiongozi mteule wa Rais anasoma VETA mje mnipige ngumi 4 za puani niko hapa TAZARA Dar es salaam nawasubiri.
Achana na watoto wa vichochoroni, nazungumzia mtoto aliyekulia nyumba za bure za viongozi.
Huenda Majaliwa anaona mbali kuliko wanaopinga tuwaze nje ya box.Fikiria miaka kumi mbele itakuwaje.Kuna ubaya gani mtu akiwa na degree sociology,law,engineering kujua utengenezaji au usindikaji wa matunda?
 
Tanzania tuna watu wapumbavu sana......

Kwani kuna ubaya gani ukajiongezea ujuzi na maarifa kama unapata nafasi hiyo....

Kwanini ukae nyumbani ukizunguka na bahasha ilihali kuna uwezekano wa kupiga kashoti kozi na kupata ajira mahali......

Tanzania kadri watu wanavyosoma ndio wanazidi kuwa wajinga.......
 
Tanzania tuna watu wapumbavu sana......

Kwani kuna ubaya gani ukajiongezea ujuzi na maarifa kama unapata nafasi hiyo....

Kwanini ukae nyumbani ukizunguka na bahasha ilihali kuna uwezekano wa kupiga kashoti kozi na kupata ajira mahali......

Tanzania kadri watu wanavyosoma ndio wanazidi kuwa wajinga.......
We mpumbavu Sana na hauna akili kuna uhakika wa ajira baada ya kutoka VETA ?.
 
Ni wapumbavu na wajijinga, mna mentality ya kipuuzi kwani kwenda kusoma VETA kutapunguza utukufu wa degree? Kuna watumishi wa umma wameajiriwa na bado wana vijiwe/ofisi zao mitaani za ufundi, ni double standard. Acheni ujinga nendeni VETA mkasome ufundi nchi ipige hatua kimaendeleo, skilled labour, the future of Tanzania
 
Yaani nyie mlitaka waziri mkuu awapetty petty mlitaka awaambie "serikali itaongeza ajira" na endapo angefanya hivyo tungeona nyuzi zinasema "waziri mkuu ni muongo na mnafiki".

Basi wenye degree waendelee kuzungusha bahasha mitaani hadi akili ziwakae sawa.
 
Back
Top Bottom