Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeongea mkuu graduates wanaona kwenda veta ni dharau.Ni wapumbavu na wajijinga, mna mentality ya kipuuzi kwani kwenda kusoma VETA kutapunguza utukufu wa degree? Kuna watumishi wa umma wameajiriwa na bado wana vijiwe/ofisi zao mitaani za ufundi, ni double standard. Acheni ujinga nendeni VETA mkasome ufundi nchi ipige hatua kimaendeleo, skilled labour, the future of Tanzania
Mkuu mimi nina busara nyingi Sana kuliko kasimu.Hamna mjinga wa hivo. Nina uhakika asilimia 100. Labda wewe na hatuwezi kukupa nafadi kama hiyo. Labda uwe kiongozi wa familia yako, uwaambie wanao wakajiuze.
Namshukuru Mungu kuna watu nawaongoza wenye familia wanaoKwahyo sasahv wew ni tajir?!
Kura ipi unaiongelea hapa?Wanajamvi Heshima kwenu,
Kwako Mh Dr Samia Suluhu Hassan Rais wetu mpendwa.
Nakuandikia kwa heshima na taadhima kuhusu kauli tata, aliyoitoa waziri Mkuu Majaliwa huko Tabora, kuwataka vijana wasomi wa vyuo vikuu kujiunga na vyuo vya VETA Kusomea ufundi wa fani mbalimbali.
Kwa upeo wangu wa kutafakari mambo naona Waziri Mkuu amevuka mstari,kwa kauli aliyoitoa.
Ni kauli
Mosi ya kudharau kada mbalimbali zilizosomewa na vijana chuo KIKUU mpaka kuwataka waziache.
Kada kama uhasibu, uhandisi ,Udaktari, Ujiolojia,ualimu, Procurement kuzitaja chache.
Watu hao juu wametumia muda mwingi,pesa kusoma kidato Cha kwanza mpaka Cha sita, Kisha miaka mitatu mpka minne chuo KIKUU.
Hili ni group kubwa la wanazuoni ambao wapo mtaani hawana ajira,walipokuwa wanasoma walikuwa na malengo yao,
Walijua kabisa VETA zipo, ukweli kuhusu VETA ni kada ya kati ya kawaida iliyokuwa na malengo ya kutoa skills study kwa ajili ya kujiajiri, kwa namna ya pekee watu ambao waliishia darasa la saba zamani, lakini sasa kidato Cha nne, ambao hawakuweza kuendelea na masomo ya juu ili wajiajiri.
Mh Rais mashaka yangu ni kuwa Kuna ombwe kubwa la ajira nchini, safari hii wapiga kura wengi nchini ni vijana, ambao hawana ajira.
Kwa Nini kauli kama hii inatoka kuelekea uchaguzi mkuu?? sio nzuri, itachochea chuki kwa vijana wasio na ajira ambao Bado wana matumaini na serikali Yako.
Kwa namna ilivyo vijana hao wamekuwa underrated, hadhi ya degree za vyuo vikuu ni bure, haina maana, mpaka leo hii vijana hao washauriwe kusomea ufundi🤔🤔🤔
Mwisho Mwishoni natamani Waziri Mkuu ajitafakari, na Mama kama mkuu wa nchi utafakari hii kauli tata, ambayo kwangu mimi kama mtanzania inatosha kwa Waziri Mkuu kukaaa pembeni baada ya Bunge kuvunjwa.
Ni imani yangu ujumbe huu utafika mezani kwako, kwa wewe mwenyewe kusoma, au kupitia wasaidizi wako.
Nandagala One -Mpumalanga
South Africa
Ufundi selemala hadi veta?Sio degree. Niambie ujasiriamali unaoweza anza na degree kidogokidogo fresh from school na ni kiasi gani?
Hapa tuiweke vizuri hii issue ya veta. Mimi naona imekaa vzuri..
Veta 2 yrs. Mtu nimekaa home 8 fck years. Kwanini nisidake issue za useremala hvi, niulete kitaa, hata kwa kusimamia
Kwani ukiwa na degree huwezi kujiajiri?Waende kujifunza ujenzi,ufugqji,kilimo na ushonaji ili wajiajiri mbona mi sioni shida katika mtizamo huo
Kwa mfano mwenye degree ya Electrical Engineering kutoka pale CoET -UDSM, kwani hawezi kufanya wiring mpaka aende VETA? Labda kauli ya PM ililenga baadhi ya kozi za degree..!Mbona ni kauli yenye kujenga, sema watu kutaka makubwa, na ni kwakuwa hiki ni kipindi cha uchaguzi basi kila kauli itajadiliwa... Simple kama unaoana umesoma na bado degree haijaweza kukutoa ulipo...
Piga kozi za veta kuna mawili aidha ujiajiri ama uajiriwe kwa level ya chini... Sababu huku level ya chini possibility ya kupata ajira ni kubwa kuliko level ya juu
We unahisi ukisoma kozi ya ufundi umeme, huwezi pata hata kazi ya kupiga wiring kwenye majengo?
au kozi ya kuchomelea, huwezi pata fursa ya kutengeneza mageti?
Kuwa na Kazi au kukaa bila kuwa na Kazi which is better ???!!Ukimaliza degree unajisajili PSRS hapo huwezi tena kuajirika kwa astashahada au stashahada labda kwa mchina ukalipwe laki mbili na nusu.
Mfumo wa PSRS hauwezi kumuajiri mtu kwa low entry level huku profile yake iko juu. Au wewe utakubali ukimaliza elimu ya degree ya miaka 3 au 4 usijisajili PSRS badala yake usubiri umalize kozi ya miaka 2 au 3 ya VETA ndipo ujisajili kwa level ya chini?
Yaani umalize degree na uisahau kabisa
Of course !Kwa mfano mwenye degree ya Electrical Engineering kutoka pale CoET -UDSM kwani hawezi kufanya wiring mpaka aende VETA? Labda kauli ya PM ililenga baadhi ya kozi za degree..!
Madai yao wameshushwa hazi.Tanzania tuna watu wapumbavu sana......
Kwani kuna ubaya gani ukajiongezea ujuzi na maarifa kama unapata nafasi hiyo....
Kwanini ukae nyumbani ukizunguka na bahasha ilihali kuna uwezekano wa kupiga kashoti kozi na kupata ajira mahali......
Tanzania kadri watu wanavyosoma ndio wanazidi kuwa wajinga.......
hizi ndizo moja ya akili tulizonazo kama taifa. Kwakweli inasikitisha sana. Embu tujitahidi kuwa tunafikiri kwa kina kabla ya kuropoka.Mbona ni kauli yenye kujenga, sema watu kutaka makubwa, na ni kwakuwa hiki ni kipindi cha uchaguzi basi kila kauli itajadiliwa... Simple kama unaoana umesoma na bado degree haijaweza kukutoa ulipo...
Piga kozi za veta kuna mawili aidha ujiajiri ama uajiriwe kwa level ya chini... Sababu huku level ya chini possibility ya kupata ajira ni kubwa kuliko level ya juu
We unahisi ukisoma kozi ya ufundi umeme, huwezi pata hata kazi ya kupiga wiring kwenye majengo?
au kozi ya kuchomelea, huwezi pata fursa ya kutengeneza mageti?
Wewe unadegree ya udaktari utajiajiri vipi? Labda familia yako ikujengee hospitali au maabara na vifaa vyake. Course zingine ni ngumu sana kujiajiri kama vile uhasibu, uinjinia na sheria labda uuze duka au ufanye shughuli zingine ambazo hazihusiani na hizo kozi.Kwani ukiwa na degree huwezi kujiajiri?
Habari!
Elimu ya VETA tunaweza kuiita elimu ya kati. Wakufuzi wake ni wahitimu wa elimu za juu. Wapo pia wakufuzi wenye elimu ya kati, nawafahamu.
Bahati mbaya kauli ya Majaliwa haijawataja hao wenye degree anataka waenda VETA ni degree za fani gani, na je, nini hatma ya elimu yao ya degree.
Huko VETA wakasome kozi za mda gani? Kwa lengo gani? Nani atagharamia ada na mahitaji mengine na nini hatma ya elimu yao ya VETA ikiwa hatma ya degree zao haijapatikana?
Mh. Samia usiogope gharama ya kuvunja bunge kwa kumtimua huyo Mh. Majaliwa.
Majaliwa ni jirani yangu huko Lindi ila kwenye mambo ya kitaifa Mimi sina jirani. Timua kabisa ili kuwepo na funzo kwa viongozi wengine waache kuongea kwa misisimko.
NJE YA MADA
Kama kuna mtoto wa Kiongozi mteule wa Rais anasoma VETA mje mnipige ngumi 4 za puani niko hapa TAZARA Dar es salaam nawasubiri.
Achana na watoto wa vichochoroni, nazungumzia mtoto aliyekulia nyumba za bure za viongozi.
Kura ipi unayoifahamu wewe???Kura ipi unaiongelea hapa?