Waziri Mkuu Majaliwa: Wenye degree kasomeni ufundi VETA mjiajiri
Mheshimiwa angempeleka mwanae kama mfano pale VETA labda ingefikilisha ila kwa mkurupuko huo sure saa100, have to do smthing about it!
 
Ni wapumbavu na wajijinga, mna mentality ya kipuuzi kwani kwenda kusoma VETA kutapunguza utukufu wa degree? Kuna watumishi wa umma wameajiriwa na bado wana vijiwe/ofisi zao mitaani za ufundi, ni double standard. Acheni ujinga nendeni VETA mkasome ufundi nchi ipige hatua kimaendeleo, skilled labour, the future of Tanzania
Umeongea mkuu graduates wanaona kwenda veta ni dharau.
 
Hamna mjinga wa hivo. Nina uhakika asilimia 100. Labda wewe na hatuwezi kukupa nafadi kama hiyo. Labda uwe kiongozi wa familia yako, uwaambie wanao wakajiuze.
Mkuu mimi nina busara nyingi Sana kuliko kasimu.
Kasimu nilianze kumhofia tangu alipotuambia rais Magufuli Yuko timamu kiafya na anawasalimia.

Ukiniwekea kasimu mganga na kasimu majaliwa nachagua kasimu mganga.
 
Wanajamvi Heshima kwenu,

Kwako Mh Dr Samia Suluhu Hassan Rais wetu mpendwa.

Nakuandikia kwa heshima na taadhima kuhusu kauli tata, aliyoitoa waziri Mkuu Majaliwa huko Tabora, kuwataka vijana wasomi wa vyuo vikuu kujiunga na vyuo vya VETA Kusomea ufundi wa fani mbalimbali.

Kwa upeo wangu wa kutafakari mambo naona Waziri Mkuu amevuka mstari,kwa kauli aliyoitoa.
Ni kauli

Mosi ya kudharau kada mbalimbali zilizosomewa na vijana chuo KIKUU mpaka kuwataka waziache.

Kada kama uhasibu, uhandisi ,Udaktari, Ujiolojia,ualimu, Procurement kuzitaja chache.

Watu hao juu wametumia muda mwingi,pesa kusoma kidato Cha kwanza mpaka Cha sita, Kisha miaka mitatu mpka minne chuo KIKUU.

Hili ni group kubwa la wanazuoni ambao wapo mtaani hawana ajira,walipokuwa wanasoma walikuwa na malengo yao,

Walijua kabisa VETA zipo, ukweli kuhusu VETA ni kada ya kati ya kawaida iliyokuwa na malengo ya kutoa skills study kwa ajili ya kujiajiri, kwa namna ya pekee watu ambao waliishia darasa la saba zamani, lakini sasa kidato Cha nne, ambao hawakuweza kuendelea na masomo ya juu ili wajiajiri.

Mh Rais mashaka yangu ni kuwa Kuna ombwe kubwa la ajira nchini, safari hii wapiga kura wengi nchini ni vijana, ambao hawana ajira.

Kwa Nini kauli kama hii inatoka kuelekea uchaguzi mkuu?? sio nzuri, itachochea chuki kwa vijana wasio na ajira ambao Bado wana matumaini na serikali Yako.

Kwa namna ilivyo vijana hao wamekuwa underrated, hadhi ya degree za vyuo vikuu ni bure, haina maana, mpaka leo hii vijana hao washauriwe kusomea ufundi🤔🤔🤔

Mwisho Mwishoni natamani Waziri Mkuu ajitafakari, na Mama kama mkuu wa nchi utafakari hii kauli tata, ambayo kwangu mimi kama mtanzania inatosha kwa Waziri Mkuu kukaaa pembeni baada ya Bunge kuvunjwa.

Ni imani yangu ujumbe huu utafika mezani kwako, kwa wewe mwenyewe kusoma, au kupitia wasaidizi wako.

Nandagala One -Mpumalanga
South Africa
Kura ipi unaiongelea hapa?
 
Waende kujifunza ujenzi,ufugqji,kilimo na ushonaji ili wajiajiri mbona mi sioni shida katika mtizamo huo
 
Sio degree. Niambie ujasiriamali unaoweza anza na degree kidogokidogo fresh from school na ni kiasi gani?
Hapa tuiweke vizuri hii issue ya veta. Mimi naona imekaa vzuri..
Veta 2 yrs. Mtu nimekaa home 8 fck years. Kwanini nisidake issue za useremala hvi, niulete kitaa, hata kwa kusimamia
Ufundi selemala hadi veta?

Mpaka namaliza degree nilikuwa naweza kutengeneza ferniture mbali mbali bila hata kwenda veta
 
Mbona ni kauli yenye kujenga, sema watu kutaka makubwa, na ni kwakuwa hiki ni kipindi cha uchaguzi basi kila kauli itajadiliwa... Simple kama unaoana umesoma na bado degree haijaweza kukutoa ulipo...

Piga kozi za veta kuna mawili aidha ujiajiri ama uajiriwe kwa level ya chini... Sababu huku level ya chini possibility ya kupata ajira ni kubwa kuliko level ya juu

We unahisi ukisoma kozi ya ufundi umeme, huwezi pata hata kazi ya kupiga wiring kwenye majengo?

au kozi ya kuchomelea, huwezi pata fursa ya kutengeneza mageti?
Kwa mfano mwenye degree ya Electrical Engineering kutoka pale CoET -UDSM, kwani hawezi kufanya wiring mpaka aende VETA? Labda kauli ya PM ililenga baadhi ya kozi za degree..!
 
Ukimaliza degree unajisajili PSRS hapo huwezi tena kuajirika kwa astashahada au stashahada labda kwa mchina ukalipwe laki mbili na nusu.
Mfumo wa PSRS hauwezi kumuajiri mtu kwa low entry level huku profile yake iko juu. Au wewe utakubali ukimaliza elimu ya degree ya miaka 3 au 4 usijisajili PSRS badala yake usubiri umalize kozi ya miaka 2 au 3 ya VETA ndipo ujisajili kwa level ya chini?
Yaani umalize degree na uisahau kabisa
Kuwa na Kazi au kukaa bila kuwa na Kazi which is better ???!!

Wanasemaga Eti Something is better than Nothing 😳 !
 
Tanzania tuna watu wapumbavu sana......

Kwani kuna ubaya gani ukajiongezea ujuzi na maarifa kama unapata nafasi hiyo....

Kwanini ukae nyumbani ukizunguka na bahasha ilihali kuna uwezekano wa kupiga kashoti kozi na kupata ajira mahali......

Tanzania kadri watu wanavyosoma ndio wanazidi kuwa wajinga.......
Madai yao wameshushwa hazi.
 
Mbona ni kauli yenye kujenga, sema watu kutaka makubwa, na ni kwakuwa hiki ni kipindi cha uchaguzi basi kila kauli itajadiliwa... Simple kama unaoana umesoma na bado degree haijaweza kukutoa ulipo...

Piga kozi za veta kuna mawili aidha ujiajiri ama uajiriwe kwa level ya chini... Sababu huku level ya chini possibility ya kupata ajira ni kubwa kuliko level ya juu

We unahisi ukisoma kozi ya ufundi umeme, huwezi pata hata kazi ya kupiga wiring kwenye majengo?

au kozi ya kuchomelea, huwezi pata fursa ya kutengeneza mageti?
hizi ndizo moja ya akili tulizonazo kama taifa. Kwakweli inasikitisha sana. Embu tujitahidi kuwa tunafikiri kwa kina kabla ya kuropoka.
 
Veta ni kupoteza tu muda kama mtu anataka kujiajiri kupitia ufundi stadi ni bora akaingia kujifunza mtaani veta labda ufuate cheti ili uajiriwe ambapo pia hamna ajira
 
Ila watanzania yawezekana likawa toleo la mwisho wa binadamu
PM hajamlazimisha mtu yeyote ameshauri kama unaona digrii haikusaidii nenda VETA
Sasa yupi bora kati ya kiongozi anayeshauri wenye digrii tujiajiri na anayesema twende veta
 
Ile kauli imenifikirisha Mengi! Na naona inatoa Mwanga kwa wananchi kuwa na wasiwasi juu ya uwezo wa viongozi wetu kushughulikia changamoto zao.

Mimi naamini kuwaza/ kufikiri kwangu huku nitakaoeleza nimekosea kuwaza, na si sahihi ninavyowaza, kwa hiyo mawazo yangu ya puuzwe kwa namna yoyote Ile!!!

Nilichofikiria kwa muda ni :
1. Ama Waziri Mkuu, as a person na si cheo chake, anakebehi elimu inayotolewa na vyuo vikuu ama hajui umuhimu wa Uwepo wa vyuo vikuu jambo ambalo siamini!

2. Ama serikali Haina mkakati wa wapi wahitimu wa vyuo vikuu wanatakiwa kuwa baada ya kupata shahada zao, mbali na serikali hiyo hiyo kuhimiza udahili wa wanafunzi huko vyuo vikuu.

3. Ama Lengo la serikali kuwepo kwa vyuo vikuu lilishabadilika na Sasa pale ni sehemu ya kutengeneza wadaiwa wa madeni kama chanzo cha mapato! (Mikopo ya Elimu ya juu)!!!

Ninarudia, Mimi naamini kuwaza kwangu huku nimekosea kuwaza, na si sahihi ninavyowaza, kwa hiyo mawazo yangu ya puuzwe kwa namna yoyote Ile!!!
 
Acha mdogo wangu apambane na Mangi shop

Nikikumbuka akaniambia sitaki kusikia kusoma inatosha sasa ni make money

Mm nipo tuu, ndo kwanza namwambia sijala ntumie hafu tatu hapo!

Ghafla imethibitishwa
 
Habari!
Elimu ya VETA tunaweza kuiita elimu ya kati. Wakufuzi wake ni wahitimu wa elimu za juu. Wapo pia wakufuzi wenye elimu ya kati, nawafahamu.
Bahati mbaya kauli ya Majaliwa haijawataja hao wenye degree anataka waenda VETA ni degree za fani gani, na je, nini hatma ya elimu yao ya degree.
Huko VETA wakasome kozi za mda gani? Kwa lengo gani? Nani atagharamia ada na mahitaji mengine na nini hatma ya elimu yao ya VETA ikiwa hatma ya degree zao haijapatikana?
Mh. Samia usiogope gharama ya kuvunja bunge kwa kumtimua huyo Mh. Majaliwa.
Majaliwa ni jirani yangu huko Lindi ila kwenye mambo ya kitaifa Mimi sina jirani. Timua kabisa ili kuwepo na funzo kwa viongozi wengine waache kuongea kwa misisimko.

NJE YA MADA
Kama kuna mtoto wa Kiongozi mteule wa Rais anasoma VETA mje mnipige ngumi 4 za puani niko hapa TAZARA Dar es salaam nawasubiri.
Achana na watoto wa vichochoroni, nazungumzia mtoto aliyekulia nyumba za bure za viongozi.

Na wewe una digirii?
 
Back
Top Bottom