Ahyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2019
- 2,310
- 5,482
mindset ya degree holders wengi ni kuajiriwa, hapo anawaza aajiriwe awe injinia wa serikaliKwa mfano mwenye degree ya Electrical Engineering kutoka pale CoET -UDSM, kwani hawezi kufanya wiring mpaka aende VETA? Labda kauli ya PM ililenga baadhi ya kozi za degree..!
Tuishi katika uhalisia, mazingira ya kazi kuna wafanyakazi wengi waliongia muda mrefu ambao pengine wana elimu ndogo kuliko huyo injinia, tatizo linakuja wengi walio makazini wanaogopa kuwapa nafasi wenye elimu ya juu wakiona huenda nafasi zao zitapotea (si wote wanawaza hivi), hii hupelekea kuweka kauzibe, so huyu injia anauwezo mzuri lakini anasota kupata nafasi kwasababu ndogo kama hizi.
Ukiona unakwama tumia njia nyinginezo kufika hapo unapotaka, ukiona karatasi ya degree inazuia, tumia karatasi ya veta kufika hapo, na ndio hoja yangu ilipo, suala hapa ni kujenga profile, ni bahati tu ndio itakuingiza kazini ikiwa huna profile (direct from school), vinginevyo kujishusha ni muhimu.
Ingia veta soma kozi ya umeme, rudi kwenye kuomba ajira, hatoogopa kukupa nafasi kwakuwa ataamini huna elimu ya kumtoa, as a time goes on unajenga profile ambayo ukija ambatanisha na hiyo degree yako hakuna wa kukuzuia tena. Mwajiri anataka ujuzi.
Degree holders acheni kukariri na majivuni ya elimu, yanawafelisha, acheni mambo "nimesota sana kuipata hii degree" be intelligent.
Ipuuzieni kauli ya Majaliwa muendelee kusota kitaa.