Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson kutangaza kujiuzulu mchana huu

Richard
Toka Tony Blair aresign siasa za UK zimebadilika sana na Boris miaka ya karibuni ndio amechochea kuni. Kuna makundi hasa Tory.

-Tony Blair aliondolewa na Gordon Brown.
-Gordon Brown akaondolewa kwenye Kura baada ya kipindi kifupi.
- Cameron akaondolewa na referendum ya Brexit iliyochangiwa na Boris.
-Theresa akaondolewa na Brexit na Boris
-Boris naye kaondolewa

Sasa hivi Conservative wanaitaji mtu ambaye hayupo kwenye makundi kupokea kijiti. La sivyo watamchomoa tena.
Afadhali Labour lakini bado awajapa mtu anayekubalika kwa wananchi
 
Nato weusi mpo??[emoji16][emoji16]
20220707_104313.jpg
 
Kufuatia Ongezeko la gharama za Maisha nchini humo hususani Mafuta na Gas kitu kilichopelekea Bidhaa na Maisha Kwa ujumla Kupanda .

Kushindwa kwake kuongoza na kufanya maamuzi ya kiuongozi .

Hatimaye kufuatia Ongezeko la Mawaziri wake zaidi ya 50 kujiuzulu Toka juzi .

Jamaa kabwaga Manyanga !!!

Wale WAMAGHARIBI wa Yombo , Buza na Kwa mtogole !!

URUSI NI TAIFA KUBWA , KUJARIBU KULITENGA NA DUNIA HAIWEZEKANI, HAIWEZEKANI !!

Sasa kimbunga ndo kimeanza, Rais Macron kapoteza Bunge Kwa wapinzani , Ujeruman Kansela naye anaanza kupumulia mashine !!
Uholanzi wameanza kuandamana kwa matrekta
 
embu ficha ujinga wako bana .

Au ni Leo baada ya hili ukaona nawee ujaribu kufatilia upate A,B,C ,D ?. Sasa tayari unazijua Siasa za Huko .
Shida humu unaona kila mtu ni kama wewe, tunagawa muda kujifunza na kufatilia vitu mbalimbali. Ila mimi ningependa Priti Patel ndio awe next PM ngona tuone
 
Jamaa kakomaa imeshindikana,ila wenzetu wako mbali sana kwenye masuala ya uongozi na uwajibikaji.

Huku kwetu PM anadanganya kila siku bila hata aibu
 
.... hiyo ndio tofauti ya democratic leadership's as compared to dictatorships ambapo maamuzi yote huwa ya sadist mmoja anayehisi ni mungu wa taifa.
Tulia dawa ikuingie vizuri, nadhani hamumjui Russia Federation nyinyi watoto wajuzi, lile ni taifa lililojaaliwa kila kitu, mlikua mkimezeshwa matango pori kuwa Marekani ndio anategemewa, sasa huko Ulaya wanalia na kusaga meno, Picha inajionyesha wazi nani Super Power kmmke, huu ni mwanzo tu
 
Shida humu unaona kila mtu ni kama wewe, tunagawa muda kujifunza na kufatilia vitu mbalimbali. Ila mimi ningependa Priti Patel ndio awe next PM ngona tuone

Priti ana kashfa nyingi hawezi kuwa PM
Basi arudi Theresa May
 
Acha apumzike tu aje mwingine. Pole zao, interval ndogo tu uchaguzi, hongera kwa ukomavu wa Demokrasia.
 
Boris Johnson waziri mkuu wa Uingereza baada ya kukalia kuti kavu kwa masaa 24 yalopita hatimae leo mchana atatangaza kujiuzulu baada ya mawaziri 55 kujiuzulu nafasi zao na serikali kushindwa kujiendesha.
===
Serikali ya Waziri mkuu wa Uingereza amezama katika mzozo ambao athari zake hazijajulikana ambazo zimepelekea kujiuzulu kwa mawaziri na maafisa wengine wa ngazi ya juu waliodai kuwa wamekosa imani na uongozi wa nchi wa Johnson.

Msukosuko huo ulianza Jumanne wake, kufuatia kashfa ya unyanyasaji wa kingono inayomuhusisha Chris Pincher – mbunge wa Conservative ambaye yuko karibu na Johnson, akiwa Waziri wa uchumi , Rishi Sunak , na Waziri wa afya. Sajid Javid, viongozi wakuu katika serikali, walijiuzuru.

Sunak alidai kuwa raia wanaitarajia serikali iendeshwe kwa njia "inayofaa, uwezo na kwa umakini "; huku Javid akidai kuwa utawala wa Johnson "haufanyi kazi kwa maslahi ya taifa".

Tangu wakati ule, katika kipindi cha saa 24, zaidi ya maibu mawaziri 40 na maafisa wengine wa ngazi ya juu wamewasilisha barua zao za kujiuzuru.

Jumatano Michael Gove, mjumbe wa muda mrefu wa baraza la mawaziri, alimuomba Waziri mkuu ajiuzuru. Ombi hili baadaye liliungwa mkono naa maafisa kadhaa wa ngazi ya juu, akiwemo Waziri wa mambo ya ndani Priti Patel.

Mawaziri kadhaa muhimu wa nchi hiyo pia walihudhuria makao makuu ya serikali ya Uingereza katika ofisi ya Waziri mkuu 10 Downing Street, ambao waliidhinisha uungaji mkono wao wa kumtaka Jonson aendelee kuwa mamlakani. Hawa ni pamoja na Waziri wa utamaduni,Nadine Dorries, na Waziri wa fursa za Brexit Opportunities, Jacob Rees-Mogg.

Kwa upande wake, Boris Johnson anaonekana kupinga uwezekano wa kung’atuka madarakani na badala yake alimuondoa mamlakani Gove, mtu ambaye amekuwa muhimu katika chama cha Conservative Party kwa muongo uliopita.

''Boris Johnson wants tanataka kuendelea kupambamba .Anaamini ana watu wa kutosha wanaomzingira wanaoweza kumuwezesha kusonga mbele ,"Waziri Dorries salielezea kwa kifupi alipokuwa akiondoka katika makao makuu ya serikali Jumatano usiku.

Boris amekuwa ni kiongozi Uingereza ambaye amepokea barua za kujiuzuru nyingi zaidi tangu mwaka 1932, alikabiliwa na maswali ya wabunge Jumatano kuhusu utawala wake, ambako alieleza wazi utashi wake wa kuendelea kubakia mamlakani.

Miito inayomtaka ajiuzuru inakuja mwezi mmoja baada ya Waziri huyo mkuu kukabiliwa na hoja ya kutokuwa na imani naye ambapo 41% ya wabunge kutoka chama chake walipiga kura dhidi yake.

BBC Swahili
Atajiuzulu kwenye chama chake lakini atabaki kuwa Waziri Mkuu wa nchi
 
Wewe Jamaa muongo unadhani humu wote wajinga sio. Kwanza anajiuzulu uongozi wa Chama, Uwaziri Mkuu ataendelea nao kidogo mpaka chama kipatw kiongozi wa kusimama kwenye uchaguzi.

Kilichomuondoa ni suala la ethics waingereza maadili wameyaweke mbele kabisa, hata kura ya kutokuwa na imani naye ni kwa sababu ya maadili. kawadanganye vijiweni
Wewe ndiye unatakiwa ujiongeze/toka hicho chumba cha giza uone nje. Hivi unafikiri kuna System ya nchi yoyote ya NATO itakubali kuitangazia Dunia kuwa Shida zao za ndani zimesababishwa na vita ya Ukraine.
Unataka watangaze ili Dunia iwadharau na Putin apate Credit.

Unajua ni kwanini juzi hapa Russia alisema ikitokea WW3 target yake ya kwanza ni Uingereza, jiulize kwanini hakuitaja Ufaransa au Ujerumani.

Boris amekuwa ndiye kiherehere mkubwa kutoa kauli dhidi ya Russia tena zisizohusiana na Matamko ya NATO, Amekuwa akitoa vitisho kama Uingereza na sio NATO, HALI HII IMESABABISHA RUSSIA imuone kama ni adui namba 1 kwake ktk Ulaya. kiusalama, Approach ya Johnson kwa Russia inaweza kuleta shida .

Kinachoendelea Uingereza ni Usanii tu kuihadaa dunia kuwa shinikizo la kujiuzulu ni kwa sababu ya Maadili/Ethics .
 
Boris Johnson waziri mkuu wa Uingereza baada ya kukalia kuti kavu kwa masaa 24 yalopita hatimae leo mchana atatangaza kujiuzulu baada ya mawaziri 55 kujiuzulu nafasi zao na serikali kushindwa kujiendesha.
===
Serikali ya Waziri mkuu wa Uingereza amezama katika mzozo ambao athari zake hazijajulikana ambazo zimepelekea kujiuzulu kwa mawaziri na maafisa wengine wa ngazi ya juu waliodai kuwa wamekosa imani na uongozi wa nchi wa Johnson.

Msukosuko huo ulianza Jumanne wake, kufuatia kashfa ya unyanyasaji wa kingono inayomuhusisha Chris Pincher – mbunge wa Conservative ambaye yuko karibu na Johnson, akiwa Waziri wa uchumi , Rishi Sunak , na Waziri wa afya. Sajid Javid, viongozi wakuu katika serikali, walijiuzuru.

Sunak alidai kuwa raia wanaitarajia serikali iendeshwe kwa njia "inayofaa, uwezo na kwa umakini "; huku Javid akidai kuwa utawala wa Johnson "haufanyi kazi kwa maslahi ya taifa".

Tangu wakati ule, katika kipindi cha saa 24, zaidi ya maibu mawaziri 40 na maafisa wengine wa ngazi ya juu wamewasilisha barua zao za kujiuzuru.

Jumatano Michael Gove, mjumbe wa muda mrefu wa baraza la mawaziri, alimuomba Waziri mkuu ajiuzuru. Ombi hili baadaye liliungwa mkono naa maafisa kadhaa wa ngazi ya juu, akiwemo Waziri wa mambo ya ndani Priti Patel.

Mawaziri kadhaa muhimu wa nchi hiyo pia walihudhuria makao makuu ya serikali ya Uingereza katika ofisi ya Waziri mkuu 10 Downing Street, ambao waliidhinisha uungaji mkono wao wa kumtaka Jonson aendelee kuwa mamlakani. Hawa ni pamoja na Waziri wa utamaduni,Nadine Dorries, na Waziri wa fursa za Brexit Opportunities, Jacob Rees-Mogg.

Kwa upande wake, Boris Johnson anaonekana kupinga uwezekano wa kung’atuka madarakani na badala yake alimuondoa mamlakani Gove, mtu ambaye amekuwa muhimu katika chama cha Conservative Party kwa muongo uliopita.

''Boris Johnson wants tanataka kuendelea kupambamba .Anaamini ana watu wa kutosha wanaomzingira wanaoweza kumuwezesha kusonga mbele ,"Waziri Dorries salielezea kwa kifupi alipokuwa akiondoka katika makao makuu ya serikali Jumatano usiku.

Boris amekuwa ni kiongozi Uingereza ambaye amepokea barua za kujiuzuru nyingi zaidi tangu mwaka 1932, alikabiliwa na maswali ya wabunge Jumatano kuhusu utawala wake, ambako alieleza wazi utashi wake wa kuendelea kubakia mamlakani.

Miito inayomtaka ajiuzuru inakuja mwezi mmoja baada ya Waziri huyo mkuu kukabiliwa na hoja ya kutokuwa na imani naye ambapo 41% ya wabunge kutoka chama chake walipiga kura dhidi yake.

BBC Swahili
Sasa sa100 anangoja nini kujiuzulu
 
Tulia dawa ikuingie vizuri, nadhani hamumjui Russia Federation nyinyi watoto wajuzi, lile ni taifa lililojaaliwa kila kitu, mlikua mkimezeshwa matango pori kuwa Marekani ndio anategemewa, sasa huko Ulaya wanalia na kusaga meno, Picha inajionyesha wazi nani Super Power kmmke, huu ni mwanzo tu
... umaenza kushabikia mataifa ya kikafiri nowadays?
 
Bongo tukifikia kuwa kama hawa jamaa,tutakuwa mbali sana

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
Umasikini ndio unaosababisha sisi Bongo tusifike huko. Tena hapa simzungumzii level ya PM nk. Nazungumzia levels za mawaziri, wabunge kushuka chini ambapo wengi kupata nafasi hizo wanasema EHUUUUU! Mungu kaniona niondokane na umasikini huu.
Ndio maana hawawezi kukosoa lolote linalogusa mamlaka. Kwasababu akijiuzulu au kufukuzwa anafikiria ataishije.

UNAFIKIRI NI KWANINI KINA MDEE WANANG'ANG'ANA NA UBUNGE.
 
Back
Top Bottom