Wewe ndiye unatakiwa ujiongeze/toka hicho chumba cha giza uone nje. Hivi unafikiri kuna System ya nchi yoyote ya NATO itakubali kuitangazia Dunia kuwa Shida zao za ndani zimesababishwa na vita ya Ukraine.
Unataka watangaze ili Dunia iwadharau na Putin apate Credit.
Unajua ni kwanini juzi hapa Russia alisema ikitokea WW3 target yake ya kwanza ni Uingereza, jiulize kwanini hakuitaja Ufaransa au Ujerumani.
Boris amekuwa ndiye kiherehere mkubwa kutoa kauli dhidi ya Russia tena zisizohusiana na Matamko ya NATO, Amekuwa akitoa vitisho kama Uingereza na sio NATO, HALI HII IMESABABISHA RUSSIA imuone kama ni adui namba 1 kwake ktk Ulaya. kiusalama, Approach ya Johnson kwa Russia inaweza kuleta shida .
Kinachoendelea Uingereza ni Usanii tu kuihadaa dunia kuwa shinikizo la kujiuzulu ni kwa sababu ya Maadili/Ethics .