Waziri Mkuu: Wanaolalama kupata ongezeko la 20,000 ni wale wenye mishahara mikubwa

Hivi hawa Mawaziri wote kwenye hii press Wameshindwa akili na Dr Mwinyi?Mbona kama hili genge linamhujumu Rais halafu na yeye hastukii huu mchezo??
Nataka nikuhakikishie Rais alitaka iwe kama ilivyotamkwa ili kina Majaliwa walidhani watadharaulika na Watumishi wakipata hela nzuri. Hili genge lina roho mbaya hata chatu ana afadhali
 
Formula ipi mkuu hembu iweke hapa Kuna kitu kinaitwa increment waachane na hilo ongezeko la rais..
Increment ya mwka ni kubwa mara dufu ya hilo ongezo la rais la 23 perc..ni Bora wangeweka increment wakaachana na hilo ongezeko..
Magu ndio alizuia increment miaka yake yote mtu ungekuta umepanda parefu tu..
Na increment ipo kisheria ila hakuna Sheria inamlazimisha rais kuongeza mshahara.
Ujinga sitaki,hukuona mchanganuo?
 
Hivi naomba kuuliza wale wa kima cha chini TGS. A ni kweli wameongezewa hiyo asilimia 23 anayosema katelephone [emoji849][emoji849]
 
Tulivyo wajinga kama nyumbu, tutaendelea kuvumilia huu ujinga. Muda wa kuikimbia nchi umefika.
 
Huyu Mtu Kila kukicha anazidi kua Muongo muongo.

Ninapendezwa na Usimamizi wake ila Uongo wake unakera

Angakaa kimya ili alotangaza iyo 23% ndo aje alitolee ufafanuzi.

Hivi hao wa Kima Cha chini, wanaishi nchi gani hiyo ? . Na hao wa Kima Cha chini Kuna aloongezewa walau hata laki Moja??.

Mbona anajichoresha na ujuha !.
 
Ndani ya hiyo miezi 12 Kuna matukio ya hatar kwenye uchumi. Rais aliidhinisha bil 100 zende kwenye mafuta zilimsaidia nini mtumishi, vitu vimepanda bei, Hapo bado hajakutana na tozo za miamala,VAT ya 18% kwa kila manunuzi,kupanda kwa bei za bidhaa na huduma kwa karibia 60% miaka 5
Wewe unata Rais afanye nini katika kuondoa mfumuko wa bei nchini ikiwa asimilia 50% ya vitu vinatoka nje ya nchi na wakati huo gharama ya usafirishaji wa mizingo kwa njia ya bahari imepanda kwa zaidi ya Mara 2?.
Ulitaka Rais afanyeje katika kushusha bei ya vyakula nchi ikiwa nchi ilikumbwa na ukame na kusababisha mazao kufia shambani?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri Mkuu, Kasimu Majaliwa amesema wengi wanaolalamika kupata ongezeko dogo la mishahara ni wale ambao wana mishahara mikubwa. Ametolea mfano wa mawaziri kuwa wako baadhi ambao ongezeko lao ni 0.02%

Amewaomba watumishi kuwaamini viongozi wa vyama vya wafanyakazi. Amesema wengi waliopata ongezeko kubwa ni wale watumishi waliokuwa wanapata mishahara midogo.

Pia amesema wananchi wanapaswa kushukuru kwa ongezeko hilo ambalo miaka kadhaa iliyopita haikuwepo
Rubbish!!!!

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mshahara wa milioni moja na point kwa mwezi ndiyo kwake anauita mshahara mkubwa! Na hapo bado huyo mfanyakazi hajakopa ili ajenge kibanda cha kumuhifadhi! Maana hakai kwenye nyumba ya serikali kama yeye Waziri mkuu! Hana deni Bodi ya mikopo!

Kweli alieyeshiba hamjui mwenye njaa. Ifikie wakati Wagombea binafsi waruhusiwe ili tupate watu wenye mawazo ya kitajiri, na hivyo kuachana kabisa na hawa watu wenye mawazo ya kimaskini na kibinafsi miaka nenda.
Majaliwa kavimbiwa. Hizi ni kauli za mtu aliyevimbiwa.
 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, amesema serikali inapopandisha mishahara inaangalia zaidi kima cha chini na kwamba asilimia 23 iliyosemwa na Rais Samia Suluhu siku ya Mei Mosi iliwalenga zaidi wenye kipato cha chini.

“Asilimia 23 iliyotamkwa haijalipwa kwa watumishi wote, fomula iliyotamkwa si wote mpaka wenye mishahara mikubwa, walionufaika ni wenye mishahara midogo.-Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ufafanuzi nyongeza ya mishahara.”

“Hao wanaosema tumeongeza sh 20 ni wenye mishahara mikubwa, wako kwenye asilimia 22, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mameneja, Wakurugenzi na Wakuu wa Mikoa ambao kidogo wana mshahara unaotosha” Mhe. Majaliwa, akifafanua nyongeza ya mishahara.
Bora JPM alikuwa akiupasua ukweli. Uongo uongo haufai. Wanajichanganya changaya kama vile ndio mara ya kwanza kima cha chini kimepandishwa nchi hii.
Hata yeye mwenyewe alikuwa akionyesha uso usiokuwa wa ukweli.
Waseme haiwezekani, waache kutudanganya kama watoto.
Sasa imagine serikali hiyo hiyo ijenge Makao Makuu Dodoma, Ijenge SGR, hata kama ni kwa mkopo, Ijenge JNHPP, ituhahakishie usalama, iweke akiba ya fedha za kigeni, iweke akiba ya fedha za ndani, iajiri ajira mpya, ilipe posho mpya halafu iongeze mishahara kiwango cha kuridhisha?
Haiwezekani, ila tatizo wanapenda uongo uongo na kupaka rangi kwingi.
JPM yeye angetuambia ukweli.
Mungu amlaze Mahali Pema! Aamen.
 
Hivi naomba kuuliza wale wa kima cha chini TGS. A ni kweli wameongezewa hiyo asilimia 23 anayosema katelephone [emoji849][emoji849]
Ndio hao wameongezewa hiyo asilimia 23.3 katika mishahara yao wanaolalamika wengi ni kuanzia TGS E. Pia imekuwa kinyume wakati mwendazake anapunguza kodi hao wenye mshahara wa TGS F walikutana na ongezeko la 40k ila mwenye kima cha chini alikutana na elfu 10 sasa wao kipindi hichi wamekutana na TGS F wamekutana na ongezeko la elfu 10 wakati wakima cha chini kakutana na ongezeko la zaidi ya elfu 70 imekuwa nongwa kila mwamba ngoma uvutia kwake
 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, amesema serikali inapopandisha mishahara inaangalia zaidi kima cha chini na kwamba asilimia 23 iliyosemwa na Rais Samia Suluhu siku ya Mei Mosi iliwalenga zaidi wenye kipato cha chini.

“Asilimia 23 iliyotamkwa haijalipwa kwa watumishi wote, fomula iliyotamkwa si wote mpaka wenye mishahara mikubwa, walionufaika ni wenye mishahara midogo.-Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ufafanuzi nyongeza ya mishahara.”

“Hao wanaosema tumeongeza sh 20 ni wenye mishahara mikubwa, wako kwenye asilimia 22, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mameneja, Wakurugenzi na Wakuu wa Mikoa ambao kidogo wana mshahara unaotosha” Mhe. Majaliwa, akifafanua nyongeza ya mishahara.
Kuna walimu maskini wa Mungu wameongezwa asilimia 2 hadi tatu wamekuwa makatibu wakuu au mawaziri tangu lini mh katelephone?
 
"Asilimia 23 iliyotamkwa haijalipwa kwa watumishi wote, fomula iliyotamkwa si wote mpaka wenye mishahara mikubwa, walionufaika ni wenye mishahara midogo.-Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ufafanuzi nyongeza ya mishahara.”
Nyongeza ya 23 % ililenga kima cha chini tu, hili ndilo halikueleweka na wengi.
 
Mshahara wa milioni moja na point kwa mwezi ndiyo kwake anauita mshahara mkubwa! Na hapo bado huyo mfanyakazi hajakopa ili ajenge kibanda cha kumuhifadhi! Maana hakai kwenye nyumba ya serikali kama yeye Waziri mkuu! Hana deni Bodi ya mikopo!

Kweli alieyeshiba hamjui mwenye njaa. Ifikie wakati Wagombea binafsi waruhusiwe ili tupate watu wenye mawazo ya kitajiri, na hivyo kuachana kabisa na hawa watu wenye mawazo ya kimaskini na kibinafsi miaka nenda.
Anachoweza ni kupaka kiwi nyeusi kichwani mwake tu. Ameshasahau alikotoka
IMG-20220610-WA0004.jpg

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Waziri Mkuu, Kasimu Majaliwa amesema wengi wanaolalamika kupata ongezeko dogo la mishahara ni wale ambao wana mishahara mikubwa. Ametolea mfano wa mawaziri kuwa wako baadhi ambao ongezeko lao ni 0.02%

Amewaomba watumishi kuwaamini viongozi wa vyama vya wafanyakazi. Amesema wengi waliopata ongezeko kubwa ni wale watumishi waliokuwa wanapata mishahara midogo.

Pia amesema wananchi wanapaswa kushukuru kwa ongezeko hilo ambalo miaka kadhaa iliyopita haikuwepo
Kochaa
 
Bora JPM alikuwa akiupasua ukweli. Uongo uongo haufai. Wanajichanganya changaya kama vile ndio mara ya kwanza kima cha chini kimepandishwa nchi hii.
Hata yeye mwenyewe alikuwa akionyesha uso usiokuwa wa ukweli.
Waseme haiwezekani, waache kutudanganya kama watoto.
Sasa imagine serikali hiyo hiyo ijenge Makao Makuu Dodoma, Ijenge SGR, hata kama ni kwa mkopo, Ijenge JNHPP, ituhahakishie usalama, iweke akiba ya fedha za kigeni, iweke akiba ya fedha za ndani, iajiri ajira mpya, ilipe posho mpya halafu iongeze mishahara kiwango cha kuridhisha?
Haiwezekani, ila tatizo wanapenda uongo uongo na kupaka rangi kwingi.
JPM yeye angetuambia ukweli.
Mungu amlaze Mahali Pema! Aamen.
Ukweli ndio huo kwamba 23% iliwahusu kima cha chini tu na sio kwa wote ila hawakueleweka.
 
Back
Top Bottom