Waziri Mkuu: Wanaolalama kupata ongezeko la 20,000 ni wale wenye mishahara mikubwa

Waziri Mkuu: Wanaolalama kupata ongezeko la 20,000 ni wale wenye mishahara mikubwa

Huelewi hata miaka 5 ni sawa na miezi mingapi?Huyo mfanyakazi alipanda cheo chake cha mwisho 2016 akaahirishiwa akapewa 2017.Je,hiyo ni sawa na miezi 12?
Tuache dhihaka dhidi ya wafanyakazi na wajenzi wa nchi hii.
Hoja niliyoleta ina vipengele vingi;
i:Asilimia ya nyongeza =2.4%.
ii:Makato 37% ya nyongeza.
iii:Huyu mfanyakazi amekaribia kustaafu na wakati huo ukiwadia unamlipa kwa mkupuo 33.3%.
iv:Anakutana na Tozo afanyapo miamala Benki.
v:Akinunua bidhaa anakuta VAT 18%.
vi:Akisafiri nauli zimepanda na akienda kununua chochote bei=>60% ya zile za 2017.
Hapo na penyewe ashukuru?Je,kufanya kazi za ajira ni tofauti na utumwa hapa Tanzania ya Tanganyika na Zanzibar?
Unategemea huyu mfanyakazi ataacha kupokea Rushwa?
2016 hadi 2020 hakuna mtumishi aliyepandishwa daraka ndugu,kilichofanyika ni kupunguza kodi tu.Mimi naongelea miezi 12 tangu Rais Samia alipotoa ruhusa ya watumishi kupandishwa madaraja na mwezi huu wa 7 wa nyongeza.Sasa wewe hukuelewa wapi?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huelewi hata miaka 5 ni sawa na miezi mingapi?Huyo mfanyakazi alipanda cheo chake cha mwisho 2016 akaahirishiwa akapewa 2017.Je,hiyo ni sawa na miezi 12?
Tuache dhihaka dhidi ya wafanyakazi na wajenzi wa nchi hii.
Hoja niliyoleta ina vipengele vingi;
i:Asilimia ya nyongeza =2.4%.
ii:Makato 37% ya nyongeza.
iii:Huyu mfanyakazi amekaribia kustaafu na wakati huo ukiwadia unamlipa kwa mkupuo 33.3%.
iv:Anakutana na Tozo afanyapo miamala Benki.
v:Akinunua bidhaa anakuta VAT 18%.
vi:Akisafiri nauli zimepanda na akienda kununua chochote bei=>60% ya zile za 2017.
Hapo na penyewe ashukuru?Je,kufanya kazi za ajira ni tofauti na utumwa hapa Tanzania ya Tanganyika na Zanzibar?
Unategemea huyu mfanyakazi ataacha kupokea Rushwa?
Serikali ya Tanzania haihudumii watumishi tu,inahudumia watanzania wengine pia.Sasa ukitaka tujaliwe sisi watumishi tu,hapo mimi sioni kama ipo sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana nawasihi Wapiga kura wa Tanzania epukeni kuwapa madaraka ya uongozi kwenye ngazi za siasa Walimu.
 
BInafsi sijaelewa mishahara ya mawaziri imeingiaje ingiaje kwenye ishu ya mishahara ya watumishi wa umma, katelephone ni changamoto sana
Kuna kipindi wateule wa rais tuliambiwa si watumishi wa umma. Ule wakati wa kumtetea Bashite.
 
Sasa hii hoja Yako Ina mahusiano Gani na kauli ya waziri mkuu?sometimes kuweka siasa kwenye Kila jambo ni too harmful.
huyo jamaa nahisi ni mwehu au kichaa manake kwenye karibia kila thread anapaste hiyo comment hata kama hazinamahusiano
 
Mbwembwe zote na kupongezwa Mama kuupiga mwingi ndiyo hiyo Tsh 90,000 kwa kima cha chini Tshs 270,000?.
Majaliwa anaweza kutumia hicho kiasi kwa saa ngapi/siku nga za mwezi?
Tuache dhihaka kwa wafanyakazi wetu.
Ongezeko la mishahara lazima liendane na hali halisi ya uchumi wa nchi, tusije kuishia kujilipa mishahara huku tukishindwa kutekeleza majukumu mengine ya kimaendeleo.
 
Siku ile Rais ametamka asilimia 23.3% watu walirukaruka sana,! Kwani hakuelewa ongezeko lilikuwa kwa watu wa kima cha chini?
 
Waziri Mkuu, Kasimu Majaliwa amesema wengi wanaolalamika kupata ongezeko dogo la mishahara ni wale ambao wana mishahara mikubwa. Ametolea mfano wa mawaziri kuwa wako baadhi ambao ongezeko lao ni 0.02%

Amewaomba watumishi kuwaamini viongozi wa vyama vya wafanyakazi. Amesema wengi waliopata ongezeko kubwa ni wale watumishi waliokuwa wanapata mishahara midogo.

Pia amesema wananchi wanapaswa kushukuru kwa ongezeko hilo ambalo miaka kadhaa iliyopita haikuwepo
Lakini pia kodi ya ATM haikuwepo.
 
Ndio hao wameongezewa hiyo asilimia 23.3 katika mishahara yao wanaolalamika wengi ni kuanzia TGS E. Pia imekuwa kinyume wakati mwendazake anapunguza kodi hao wenye mshahara wa TGS F walikutana na ongezeko la 40k ila mwenye kima cha chini alikutana na elfu 10 sasa wao kipindi hichi wamekutana na TGS F wamekutana na ongezeko la elfu 10 wakati wakima cha chini kakutana na ongezeko la zaidi ya elfu 70 imekuwa nongwa kila mwamba ngoma uvutia kwake
Samaki kula mtu ni habari ila mtu kula samaki sio habari....
 
Huyu naye ni mwananchi. Kitendo Cha kudharau maoni ya wananchi kitawafikisha pabaya. Serikali ipo kuwahudumia wananchi na sio kujifanyia maamuzi.
😬😬😬😬 Pabaya wapi? Hutaki acha Kazi kama una hiyo jeuri..

Na likitambi lako wewe sio mwananchi mlemgwa.
 
"Asilimia 75 - 78 ya watumishi wote wa Umma ndiyo wanaofaidika na hii asilimia 23 ya nyongeza ya mshahara, hata Mawaziri wetu na wao wanaongezewa asilimia 0.7" - Kassim Majaliwa - Waziri Mkuu""

mkuuu hapo umetishaaaaa
Lengo la Rais Samia ni kuwainua wale wenye mishahara midogo
 
Back
Top Bottom