KING KIGODA
JF-Expert Member
- Dec 28, 2018
- 3,893
- 3,145
2016 hadi 2020 hakuna mtumishi aliyepandishwa daraka ndugu,kilichofanyika ni kupunguza kodi tu.Mimi naongelea miezi 12 tangu Rais Samia alipotoa ruhusa ya watumishi kupandishwa madaraja na mwezi huu wa 7 wa nyongeza.Sasa wewe hukuelewa wapi?.Huelewi hata miaka 5 ni sawa na miezi mingapi?Huyo mfanyakazi alipanda cheo chake cha mwisho 2016 akaahirishiwa akapewa 2017.Je,hiyo ni sawa na miezi 12?
Tuache dhihaka dhidi ya wafanyakazi na wajenzi wa nchi hii.
Hoja niliyoleta ina vipengele vingi;
i:Asilimia ya nyongeza =2.4%.
ii:Makato 37% ya nyongeza.
iii:Huyu mfanyakazi amekaribia kustaafu na wakati huo ukiwadia unamlipa kwa mkupuo 33.3%.
iv:Anakutana na Tozo afanyapo miamala Benki.
v:Akinunua bidhaa anakuta VAT 18%.
vi:Akisafiri nauli zimepanda na akienda kununua chochote bei=>60% ya zile za 2017.
Hapo na penyewe ashukuru?Je,kufanya kazi za ajira ni tofauti na utumwa hapa Tanzania ya Tanganyika na Zanzibar?
Unategemea huyu mfanyakazi ataacha kupokea Rushwa?
Sent using Jamii Forums mobile app