Si mnajenga SGR yenu na itafika, Rwanda, Burundi na bandari yetu inategemea mizigo ya Rwanda, Burundi, Congo na Uganda. Nyie mnataka mfanye biashara nyie tu? Hii ni two way traffic lazima sisi wenyewe waafrika tuungishane. Hapo kibaha Kuna malori ya kichina yanaundwa/ kuunganishwa mnadhani soko litapatikana wapi? Mazao yenu mnauza wapi, Azania, Mo na Bakhresa huko Rwanda, Burundi na Congo ndiyo masoko yao makubwa. Lazima na sisi tununua toka kwao ili tuwe na biashara endelevu.
Wakati wa Magu huyu kagame alinunua advance Radar kabla ya sisi akaifunga kwao halafu akaomba kibali kwenye mamlaka ya anga ya Africa acontrol anga letu lote kwa kuongoza ndege kwa niaba yetu, zile radar zinasoma mpaka Dodoma. Magu akaona ujinga huu akanunua za kwetu na kuzifunga, bila hivyo tungekula tunawalipa Rwanda kutuongozea ndege. Kingine amejenga mtambo mkubwa wa kuchenjua Madini wakati sisi bado hatuna, Magu akahimiza wawekezaji mpaka wamejenga. Kagame alitegemea kupata Madini yetu yakasafisbwe huko. Ndiyo maana uhusiano wao haikuwa mzuri Sana hapa mwishoni.