Waziri Nape: Natoa siku 7 waajiri kuwalipa Waandishi wa Habari waliofariki kwenye ajali. Tambueni tu leseni zenu ziko kwangu

Waziri Nape: Natoa siku 7 waajiri kuwalipa Waandishi wa Habari waliofariki kwenye ajali. Tambueni tu leseni zenu ziko kwangu

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Waziri wa Habari na Mawasiliano ya teknolojia ya Habari Nape Nnauye ni miongoni mwa waliofika uwanja wa Nyamagana kuungana na RC Mwanza, Injinia Robert Gabriel na Waombolezaji wengine kuaga miili ya Waandishi 6 waliofariki kwenye ajali jana.

Natoa siku saba kuanzia leo kwa waajiri wote, kama kuna mwanahabari aliyefariki dunia kwenye ajali hii uwe umemlipa na taarifa za malipo yake yafikishe kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza. Tambueni tu leseni zenu ziko kwangu.

Ni siku ngumu kidogo kwangu, ni shughuli yangu ya kwanza hadharani baada ya kuaminiwa kwenye dhamana hii, ni shughuli ngumu kwa sababu tumekuja kwenye jambo gumu ambalo ni pigo kwa tasnia yetu ya habari, kwa kanda ya Ziwa na nchi yetu

Tupitie ajali zote zilizohusisha wanahabari kwenye misafara, viongozi wangu wameniagiza tuwaombe wenzetu wa jeshi la polisi watuletee ripoti za ajali hizi tuone kwanini zinagusa wanahabari na tuchukue hatua ya kuwalinda

Pia soma > Simiyu: Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali katika msafara wa Mkuu wa Mkoa Mwanza


N1.jpg
N2.jpg

N3.jpg
 
Umeanza kukurupuka. Serikali inasaidiaje familia za hao marehemu?
.... serikali inataka kujitoa kimtindo wakati walikuwa wanaenda kuandika habari za serikali na walikuwa wamebebwa na serikali (STL) na sio waajiri! Kwa mfano, suala la bima (ya ajali) hapo inakuwaje? Chombo kilichosababisha ajali ni cha waajiri?
 
Huko kukumbushia kwamba leseni zao unazimiliki ni udiktekta na uhuni🐒
... mara hii ameshasahau "mistakes" alizofanya awamu iliyopita! Madaraka hulevya zaidi ya kilevi kikali!
 
Natoa siku saba kuanzia leo kwa waajiri wote, kama kuna mwanahabari aliyefariki dunia kwenye ajali hii uwe umemlipa na taarifa za malipo yake yafikishe kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Wawalipe nini? ni vema kueleza wazi walipwe nini?

Wizara ije na sera ambayo itawasaidia wanahabari pindi wanapopata Chamamoto kama hizi, mfano Chombo husika kutoa mkono wa pole kwa familia kiasi cha TZS Kadhaa etc...
 
Sawa sawia...hadi anaongea hivyo ina maana kuna malalamiko keshapata either kutoka kwa ndugu or co-workers kuwa baadhi ya waliofariki wanamalimbikizo ya mishahara ambayo hawajalipwa.
.... sawa ila hakutakiwa kuwakaripia waajiri kwa namna alivyofanya na kujenga image kwa jamii kama wakosefu! Mbona hataji wajibu wa serikali kwenye suala hilo? Bado ana elements za udikteta fulani wa enzi iliyopita!
 
Vipi kuhusu wale raia wengine waliofariki kwenye ajali hiyo mbona habari zao sijaziona? ingependeza kama nao wangeagwa hapo pia.
 
"Tambueni leseni zenu ziko kwangu"

Huyu mfungia magazeti anaonekana bado hajaiacha ile tabia yake, more to come.
 
Huyu kwa kukurupuka.

Ilitakiwa serikali ilipe fidia kwa familia za wafiwa.
 
Back
Top Bottom