Waziri Nape: Natoa siku 7 waajiri kuwalipa Waandishi wa Habari waliofariki kwenye ajali. Tambueni tu leseni zenu ziko kwangu

Waziri Nape: Natoa siku 7 waajiri kuwalipa Waandishi wa Habari waliofariki kwenye ajali. Tambueni tu leseni zenu ziko kwangu

Malipo yoyote ya mtu aliyefariki ufanywa kwa kufuata sheria. Kwa mfano inatakiwa kwanza uteuzi wa msimamizi wa mirathi ambo ufanywa na mahakama baada ya mapendekezo ya kikao cha wana familia. Kwa kawaida ni mchakato wa muda usiopungua miezi 3 kwa wale walio fasta. Kama mh. waziri alikua na nia ya malipo kwa marehemu, basi bila shaka alizidiwa na emotions. Pole sana mh. Nape. It is understandable!
 
Kuwalipa malipo gani? Malimbikizo ya mishahara au mshahara wa mwezi January?
Any outstanding and legal arrears....

Sidhani kama ni jambo baya ili ziwasaidie ndugu katika wakati huu mgumu basi ni vema kuhakikisha haki inatendeka (Unajua Tanzania Haki huwa inacheleweshwa au inapotea kabisa)
 
Ameyatafuta kwa tabu sana, kushinda twitter everyday, day and night.
... na kujiliza mbele ya screen; "oooh kama baba yangu angekuwepo"; baada ya kuyapata ghafla keshalewa!
 
Waziri wa Habari na Mawasiliano ya teknolojia ya Habari Nape Nnauye ni miongoni mwa waliofika uwanja wa Nyamagana kungana na RC Mwanza Injinia Robert Gabriel na Waombolezaji wengine kuaga miili ya Waandishi 6 waliofariki kwenye ajali jana

Natoa siku saba kuanzia leo kwa waajiri wote, kama kuna mwanahabari aliyefariki dunia kwenye ajali hii uwe umemlipa na taarifa za malipo yake yafikishe kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza. Tambueni tu leseni zenu ziko kwangu.

Ni siku ngumu kidogo kwangu, ni shughuli yangu ya kwanza hadharani baada ya kuaminiwa kwenye dhamana hii, ni shughuli ngumu kwa sababu tumekuja kwenye jambo gumu ambalo ni pigo kwa tasnia yetu ya habari, kwa kanda ya Ziwa na nchi yetu

Tupitie ajali zote zilizohusisha wanahabari kwenye misafara, viongozi wangu wameniagiza tuwaombe wenzetu wa jeshi la polisi watuletee ripoti za ajali hizi tuone kwanini zinagusa wanahabari na tuchukue hatua ya kuwalinda

Pia soma > Simiyu: Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali katika msafara wa Mkuu wa Mkoa Mwanza

Waandishi wamekufa wakiwa ndani ya gari la serikali ambalo lilikuwa likiendeshwa kizembe kwa hiyo ndio inawajibu wa kwanza kulipa familia zao haraka sana iwezekanavyo. Mwajiri atawajibika tu kwa masuala yanayohusu ajira yake

Nape aache vitisho mbuzi
 
Ingekuwa ajali kama ile ya Azam media sawa, gari la mwajiri na wametumwa na majiri.

Lakini waandishi watumiwe na serikali kwenye propaganda zao, gari la serikali halafu lawama uwape makampuni.

Kama makubaliano ya kazi hayana limited liability; serikali ianze kwanza kulipa fidia hizo taasisi husika kwa kuwapotezea wafanyakazi na familia za marehemu.

Mengine ya kitaasisi yatafanyika kwa mujibu wa sheria za kazi; sio amri ya waziri.
 
.... serikali inataka kujitoa kimtindo wakati walikuwa wanaenda kuandika habari za serikali na walikuwa wamebebwa na serikali (STL) na sio waajiri! Kwa mfano, suala la bima (ya ajali) hapo inakuwaje? Chombo kilichosababisha ajali ni cha waajiri?
STL hazina Bima
 
Waandishi wamekufa wakiwa ndani ya gari la serikali ambalo lilikuwa likiendeshwa kizembe kwa hiyo ndio inawajibu wa kwanza kulipa familia zao haraka sana iwezekanavyo. Mwajiri atawajibika tu kwa masuala yanayohusu ajira yake

Nape aache vitisho mbuzi
Kabisa

Hiyo ndio commonsense

Sasa sikiliza mawazo ya hawa vijana ambao CCM imewandaa kwa uongozi.
 
Waziri wa Habari na Mawasiliano ya teknolojia ya Habari Nape Nnauye ni miongoni mwa waliofika uwanja wa Nyamagana kungana na RC Mwanza Injinia Robert Gabriel na Waombolezaji wengine kuaga miili ya Waandishi 6 waliofariki kwenye ajali jana

Natoa siku saba kuanzia leo kwa waajiri wote, kama kuna mwanahabari aliyefariki dunia kwenye ajali hii uwe umemlipa na taarifa za malipo yake yafikishe kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza. Tambueni tu leseni zenu ziko kwangu.

Ni siku ngumu kidogo kwangu, ni shughuli yangu ya kwanza hadharani baada ya kuaminiwa kwenye dhamana hii, ni shughuli ngumu kwa sababu tumekuja kwenye jambo gumu ambalo ni pigo kwa tasnia yetu ya habari, kwa kanda ya Ziwa na nchi yetu

Tupitie ajali zote zilizohusisha wanahabari kwenye misafara, viongozi wangu wameniagiza tuwaombe wenzetu wa jeshi la polisi watuletee ripoti za ajali hizi tuone kwanini zinagusa wanahabari na tuchukue hatua ya kuwalinda

Pia soma > Simiyu: Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali katika msafara wa Mkuu wa Mkoa Mwanza

Hii Wizara kuwekewa Habari inameza lengo kuu la kuwa na Wizara ya TEHAMA.... inshu hapa zitakuwa kufungia magazeti, tv...waandishi wa habari. Na mwisho wa siku pia itakosa Waziri sahihi kwenye hii Wizara watawekwa wa tantalila ...
 
Aaah nape ungeanza na waliovamia cloud na aliyekutolea bastola.
Mfuga mbwa zimezagaa mfuga mbwa hayupo tena
 
Ana kurupuka sijui bado haja jifunza kwakilicho mpata kwenye awam ya 5 yakukurupuka kumuundia tume mteule wa Rais na kutoa hukumu
Alikuwa sahihi sema shida ni wakati
 
Alikuwa sahihi sema shida ni wakati
Hakuwa sahii kuna wateule wa Raisi wana wajibika kwa Rais mfano mkuu wa majeshi hawezi kumuundia tume ya kumchunguza mkuu wa Uhamiaji, mkuu wa magereza , ndiyo maana kuna matukio mengine raisi ana unda tume ya kuchunguza, we waziri una muundia tume mkuu wa mkoa kwa kifupi aliingilia majukumu ya Rais mkuu wa mkoa ni mteule wa Raisi na ana wajibika kwa Raisi .
 
Back
Top Bottom