Waziri Nape: Natoa siku 7 waajiri kuwalipa Waandishi wa Habari waliofariki kwenye ajali. Tambueni tu leseni zenu ziko kwangu

Waziri Nape: Natoa siku 7 waajiri kuwalipa Waandishi wa Habari waliofariki kwenye ajali. Tambueni tu leseni zenu ziko kwangu

Tumerudi utawala uliopita? Makampuni binafsi yanataratibu za kuwalipa wanaopata ajali, hao wahusika hawakupanda gari za makampuni yao na hili liwe fundisho kwa waandishi wa habari kwa kupenda chee!

Waandishi hawa wamepata ajali kwenye gari ya serikali, sidhani kama ina bima. Kutokana na gari kuwa si ya mwajiri sijui hapo mwajiri anahusikaje! Mheshimiwa waziri chukua jukumu la kuubeba msiba na malipo majeruhi na waliofariki na si kuonesha ubabe.
Ina maana magari ya Serikali hayana Bima? Siamini hicho kitu.
Serikali inatakiwa kusimamia sheria na kuwa mfano kwa raia.
 
This guy is an empty brain really. Leseni za waajiri (media houses) zinahusianaje na vifyo vya waandishi wa habari vilivyosababishwa na ajali ya gari/barabarani wakiwa wamepakiwa kwenye gari la serikali lisilokuwa na bima?
Useless statement kabisa.
 
Mfanyakaz wa serikal akifa Leo Una jua mpaka familia Yake ilipwe mafao yake ni baada ya siku ngapi? Sasa yeye ana kurupuka tu
Huyu nape hajui taratibu za mirathi,haya ni masuala ya kisheria.atulize munkari Safari bado ndefu.
 
Sawa sawia...hadi anaongea hivyo ina maana kuna malalamiko keshapata either kutoka kwa ndugu or co-workers kuwa baadhi ya waliofariki wanamalimbikizo ya mishahara ambayo hawajalipwa.
Watu wanahoji uhalali wa tamko lake, wewe unajibia kwa hisia zako, na Hauna ushahidi wa kuthibitishia!
Acha mwenyewe atoe ufafanuzi wa kauli yake

Uchawa, uchawa, uchawa kila Kona!!!
 
wamefia kwenye gari ya serikali, iko wazi insurance inweza kuhusika.
wamekufa wakiwa kazini, mwajiri anawajibika.
 
Eti leseni zipo kwangu? huyu kumbe boga tuu, acha vitisho fanya kazi
 
Semina elekezi hakuna.

Ngurdoto ndio imeshakua Hostel.

Waziri anarukia rukia tu Wizara Nyingine.
 
.... serikali inataka kujitoa kimtindo wakati walikuwa wanaenda kuandika habari za serikali na walikuwa wamebebwa na serikali (STL) na sio waajiri! Kwa mfano, suala la bima (ya ajali) hapo inakuwaje? Chombo kilichosababisha ajali ni cha waajiri?
STL hainaga bima
 
Umeanza kukurupuka. Serikali inasaidiaje familia za hao marehemu?
Hiyo ni mihemuko tu. Sheria inasemaje kuhusu malipo kwa marehemu? Anayepata malipo haya huwa ni msimamizi wa mirathi. Tartibu za kumpata huchukua si chini ya mwezi. Kuanzia vikao vya familia, kumteua, kumthibitisha mahakamani n.k. Baada ya hapo msimamizi hufuatilia malipo haya ambayo nayo huchukua muda. Tuwaombee viongozi wetu waweze kuwa na busara katika hayo wanayoyasema kwani mengine hayatekelezeki kiurahisi namna hiyo.
 
Back
Top Bottom