Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,710
- 9,063
Ina maana magari ya Serikali hayana Bima? Siamini hicho kitu.Tumerudi utawala uliopita? Makampuni binafsi yanataratibu za kuwalipa wanaopata ajali, hao wahusika hawakupanda gari za makampuni yao na hili liwe fundisho kwa waandishi wa habari kwa kupenda chee!
Waandishi hawa wamepata ajali kwenye gari ya serikali, sidhani kama ina bima. Kutokana na gari kuwa si ya mwajiri sijui hapo mwajiri anahusikaje! Mheshimiwa waziri chukua jukumu la kuubeba msiba na malipo majeruhi na waliofariki na si kuonesha ubabe.
Huyu nape hajui taratibu za mirathi,haya ni masuala ya kisheria.atulize munkari Safari bado ndefu.Mfanyakaz wa serikal akifa Leo Una jua mpaka familia Yake ilipwe mafao yake ni baada ya siku ngapi? Sasa yeye ana kurupuka tu
Watu wanahoji uhalali wa tamko lake, wewe unajibia kwa hisia zako, na Hauna ushahidi wa kuthibitishia!Sawa sawia...hadi anaongea hivyo ina maana kuna malalamiko keshapata either kutoka kwa ndugu or co-workers kuwa baadhi ya waliofariki wanamalimbikizo ya mishahara ambayo hawajalipwa.
STL hainaga bima.... serikali inataka kujitoa kimtindo wakati walikuwa wanaenda kuandika habari za serikali na walikuwa wamebebwa na serikali (STL) na sio waajiri! Kwa mfano, suala la bima (ya ajali) hapo inakuwaje? Chombo kilichosababisha ajali ni cha waajiri?
Hiyo ni mihemuko tu. Sheria inasemaje kuhusu malipo kwa marehemu? Anayepata malipo haya huwa ni msimamizi wa mirathi. Tartibu za kumpata huchukua si chini ya mwezi. Kuanzia vikao vya familia, kumteua, kumthibitisha mahakamani n.k. Baada ya hapo msimamizi hufuatilia malipo haya ambayo nayo huchukua muda. Tuwaombee viongozi wetu waweze kuwa na busara katika hayo wanayoyasema kwani mengine hayatekelezeki kiurahisi namna hiyo.Umeanza kukurupuka. Serikali inasaidiaje familia za hao marehemu?