Tatizo la nchi hii ni katiba mbovu alioiacha Mwalimu huku akijua ikipata kiongozi asiye na hekima yeye ndie atakuwa executive, judiciary na parliamentary. Na si hivyo tu, bsli atakuwa mungu mtu na asihojiwe na yeyote. Katiba hii inaruhusu yeye awe kila kitu. Hata wanaotakiwa kumshughulikia kiongozi anayeharibu nchi (mavipenyo) yeye ndie anawachagua na wanamuogopa. Fikiria nchi kama Marekani ingekuwa na katiba bomu kama hii, nakuhakikishia Trump angewatesa sana na asingetoka madarakani. Maskini wee, Mwalimu alifikiri wote huwa wana hekima, hakujua hata wasio na hekima (wapumbafu) huwa wana fluke na kupata vyeo vikubwa!