Waziri Ndalichako better late than never; Mikopo ya elimu ya juu hailipiki sababu ya Value Retention fee ya 6%

Na CCM ndio hawataki kubadilisha katiba
 
Haulipiki, unacholipa ni kidogo kuliko riba inayoongezeka
 
Hii ya
Madeni ya HESLB ni noma sana, plus ukosefu wa ajira na kuzuiwa kwa mafao.

Nihatari kwa Usalama wa nchi yetu. Nivema wahusika wakawajibika.

Ikitokea mtu mmoja akawaunganisha wahanga hawa nchi inaweza ingia matatani

Mh! Raisi wangu naomba uliangalie hili ili lisije chafua kazi nzuri unayofanya.
 
Mimi sijasoma LAW ila najua kuwa kabla kutunga sheria yeyote lazima uangalie impact yake mahala itakapotumika kinagaubaga. Na kama itaacha loophole yeyote basi lazima ibadilishwe ili kukidhi vigezo. Sasa walipotunga hii sheria sijui kama walifikiria kama kuna siku graduate atakosa ajira rasmi na kujiari kama bodaboda.
 
Wabunge wa upinzani walionya mapema bungeni. Ndugai na viherehere wa Ccm wakaoitisha kwa wingi wao. Walidhani ina wahusu Chadema na Act wazalendo. Sasa wako wenyewe wana hadaa motion wameianzisha wao.
Bado records zipo. Hata Ndugai aki rest leo, bado historia ita mhukumu.
 
Kwahiyo hili hawalioni? Hebu fikiria kijana ambae hajaajiriwa tangia 2015 retention fee yake inasoma tu na hajui ataajiriwa lini
Huyo bora asiajiriwe tu, maana deni lake now ni karibia mara 10 ya alichokopa
 
Profesa anayesikia tu tamko la mkulu kuwa lianzishwe somo la Historia ya Afrika Kusini haipiti hata saa 24 tayari ashatangaza kuanzakwa somo hilo kuanzia la kwanza mpaka kidato cha Sita tena kwa Kiswahili ili mradi mkuu afurahi yaani
 
Msamehe bure... Pengine hata haelewi alichoandika... Inawezekana hajui hata kinachoongelewa hapa... Si unaona hata mwandiko wake ulivo mbovu!!
 
Kuna siku kama sijakosea alisema serikali kwenye makato ya heslb ina haki ya kukata ata mpka robo tatu ya mshahara.😫😫
 
Profesa anayesikia tu tamko la mkulu kuwa lianzishwe somo la Historia ya Afrika Kusini haipiti hata saa 24 tayari ashatangaza kuanzakwa somo hilo kuanzia la kwanza mpaka kidato cha Sita tena kwa Kiswahili ili mradi mkuu afurahi yaani
Yani wanafanya kazi ya kulinda vibarua siyo masilahi ya wananchi
 
Ajakataa kulipa tatizo lipo unalipa unategemea deni linapungua kumbe bado lipo pale pale
 
Uzalendo ni kusoma historia? Yaani usome historia mpaka chuo kikuu halafu unyimwe ajira huku watoto wa vigogo wakiajiriwa kimyakimya . Ili uitwe mzalendo eti usilalamike?
 
Inashangaza sana.Halafu anaibuka mtu anasema et yeye ni mtetezi wa wanyonge!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…