Heshima mbele mkuu, hakuna noma nilitumiwa na jamaa private, aliyekuwepo kwenye ajali, anyway Mungu amlaze pema marehemu peponi, hii inatisha sana,
Wiki hii nilipata bahati ya kuzngumza na baadhi ya wabunge wetu, walioshirki kwenye mjadala ule wa kumfukuza Zitto,
1. Mundhihir, aliandikiwa kipande cha ujumbe na Lowassa, kuipeleka hoja ya kumfukuza Zitto, yaani alishinikizwa na Lowassa,
2. Alipomaliza kutoa hoja, ikawa zamu ya Zitto, kuzungumza, vyombo vyote vya mawasiliano ndani ya bunge vikazimwa, matokeo yakawa wananchi kutokupata exactly what Zitto, said!
3. Baada ya Zitto, kumaliza ilibidi kupigwe kura kuhusu kumfukuza, kuna wabunge wa CCM, waliokasirishwa, na uamuzi huo wa wabunge wa CCM, kuipitisha hiyo hoja wakaamua kuondoka ili wasipige kura, hakuna gazeti waloa media zetu, ambako wananchi walifahamishwa haya,
4. Naomba ninukuuu machache aliyoyasema Zitto, kama nilivyofahamishwa huku mawasiliano yote bungeni yakiwa yamezimwa,
"....Mheshimiwa Mundhihir, sisi wabunge wote hapa tumechaguliwa na Mungu, ili tuje tuwakilishe masilahi ya taifa na wananchi kwa ujumla, wewe unawakilisha masilahi yako na wenzako, mimi ninawakilisha masilahi ya wananchi na taifa. Ninacho omba ni kamati iundwe kuchunguza kama madai yangu yana ukweli, yasipokuwa na ukweli basi sio tu nifukuzwe bunge, bali ninyongwe,....Mungu hatawasamehe wewe na wale wote unaowawakilisha...."
Wakuu wangu nimejaribu tu kufupisha na kuchambua kwa kifupi yale yaliyojiri, ambayo binafsi nayaona yanakaribiana sana na yanayojiri,
Namuomba Mwenyezi Mungu ayapitishie Mbali, na mkuu Zitto, I do not care unatoka chama gani, lakini Bravo mkuu na heshima mbele mkuu,
na Mungu akujalie mkuu! na Mungu amlaze mahali pema peponi marehemu Mbatia!