Waziri Ummy: Bima ya Afya (NHIF) inakaribia kufa

Ila mashirika ya umma kwanini kila shirika ni hasara tu ninachojua ni usimamizi mbovu ona TTCL nayo suala la mda
 
Tatizo kubwa litakuwa kwenye manejimenti ya NHIF.
Watumishi wa umma wawe huru kuchagua mifuko ya kujiunga nayo.
Hii itafanya mfuko wa NHIF kushindana na mifuko mingine. Na watakuwa makini.
 
NHIF inaelemewa na wafanyakazi wa Serikali.

Ili mfuko usielemewe wategemezi waondolewe au mtu atibiwe kutokana na anavyochangia
Msitudanganye sababu ni CCM kuchota fedha za uchaguzi 2020.
 
Waziri hana aibu na uwezo wake wa kufikiri una walikini, hayo mashirika yanakusanya pesa nyingi sana na hadi kufikia uwezo wa kutumia hii michango kufanya biashara na majengo makubwa yanayopangishwa, huko kufa kunakujaje?
 
NHIF ilianzishwa na Mkapa pia, 1999
 
Uwekezaji mbovu, ufisadi kutoka baadhi ya watumishi, utawala mbovu ni baadhi ya vyanzo vitavyomaliza mashirika mengi ya Serikali
 
Viwango viko sawa kwa waajiriwa tu. Wanaojilipia wametungiwa vifurushi ambavyo hata ukichaguwa cha juu kabisa huduma utapata chini ya muajiriwa.
 
Swali ni kwa nini kuna ubaguzi wa kuwafanya wasiojiriwa wapate huduma ndogo kwa malipo makubwa zaidi.
 
Ila mashirika ya umma kwanini kila shirika ni hasara tu ninachojua ni usimamizi mbovu ona TTCL nayo suala la mda
Hivi kama sikosei, mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Bima ya Afya ni Mama Anna Makinda ..... kaazi kwelikweli.
 
NHIF ina tatizo.... Moja la tatizo ni kutoa huduma sawa kwa kila mtu..

Waweke viwango vya huduma kutokana na mtu achangiavyo
Nani kakwambia hakuna viwango
 
Matatizo yanachangiwa na ujinga na ulimbukeni wa jamii kwa ujumla.
Kuna watu wanapewa huduma za afya na dawa zisizohitajika kwa sababu tu ya ujinga na ulimbukeni wa bima, pia hospitali kujaribu kuongeza mapato kwa sababu hizo hizo.
Haiwezekani wagonjwa na gharama ziwe kubwa hivyo.
Kuna shida ya utawala, utaalamu na wadau kwa ujumla.
 
Waziri anakosea anapokiri bima ya afya NHIF inakaribia kufa, kwanini wasitafute njia mbadala itakayowawezesha kumudu hayo mazingira ya kuongezeka gharama za matibabu?
Sasa ajira tu, si wapoteze mfuko unakata hela zetu wengine miaka miwili hatujatibiwa, je tukisema hela zetu zirudishwe ?
 
Mfuko unakusanya kiasi gani jumla kwa mwezi, mwaka toka kwa watumishi?

Kwa hiyo idadi iliyotajwa × 15,000 × Miezi 12 = Takribani Trilioni moja kwa mwaka. Hapo ni kama watumishi wote wanachangia sh 15,000

Sasa kulipa hiyo 100bn kwa mwaka ndo shirika life?
 
Phd za mchongo haziwez leta mafanikio kwenye jamii
Mkapa hakuwa na phd lkn check tra na tanroad

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ummy kazidi lopolopo, siasa nyingiii,
 
Mwananchi apewe ruhusa kuchagua bima ya afya. Ataingia makubaliano yeye binafsi ie makato, coverage. NHIF inaendeshwa kisiasa zaidi. Bunge plus wizara are to blame. This was pointed out by the CAG. What action was taken???
Tulia kimya tulambe asali wewe

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…