Waziri wa Elimu kataza wanafunzi kulazimishwa kwenda na madaftari yote shule

Waziri wa Elimu kataza wanafunzi kulazimishwa kwenda na madaftari yote shule

Unawezaje kulifanya jambo kama hili liwe na matokeo chanya kitaifa bila ya Waziri wa Elimu kulitolea agizo??

Mbona wakati ule ulikuwa hushangai Rais wa nchi kuzungumzia migogoro ya Ardhi na ndoa za watu?
Kama unakumbuka tuli kuwa tunalaani kwamba ni one man show au umesahau mkuu?

Kwanini tunakuwa vigeu geu, kwani maafisa elimu au walimu wakuu wasifanye hadi waziri?
 
Ndio, mtoto wa shule ya msingi akiwa nyumbani hatakiwi kusoma mambo ya shuleni tena. Ulimbukeni wa elimu unawatesa sana watoto.
Naonba Nikuulize Swali…Na Akiwa nyumbani hasomi? Sababu vitabu na Madaftari ameweka Shuleni kwenye Locker[emoji2368]
Pili Huu Mzigo Anapotoka Tuu Shule anabeba Na Anapoenda Shule mgongo Itauma sana Baadae
 
Huwezi kuelewa mzigo wanaobebeshwa wanafunzi wa shule za kutwa mpaka pale utakapojaribu kuubeba mfuko wa madaftari wanaobeba wakienda shuleni. Kitendo cha watoto kulazimishwa kwenda na Vitabu vya kiada na Madaftari ya Masomo yote shuleni kila siku kinawaletea wanafunzi hao matatizo kwenye uti wa mgongo.

Hivi kila shule si ina ratiba ya Masomo. Kwa nini watoto wabebeshwe mzigo wa madaftari na vitabu kwa masomo yasiyohusika kwa siku hiyo.

Kama Ratiba inaonesha kutakuwa na masomo manne ni kwa nini mtoto asibebe madaftari ya masomo hayo tu?

Miaka ijayo jamii itaingia gharama ya kutibu watu wazima chungu nzima watakaokuwa wanaumwa uti wa mgongo, chanzo kikiwa ni uzembe tu wa walimu kulazimisha watoto kubeba mzigo wa madaftari na vitabu bila ya sababu.
Wazazi ongeeni na walimu, sio kila kitu kigeuzwe siasa.
 
Hili ni tatizo !
Na linachangiwa pia na teknolojia kutotumika ipasavyo katika ufundishaji tangu awali.
 
Kama unakumbuka tuli kuwa tunalaani kwamba ni one man show au umesahau mkuu?

Kwanini tunakuwa vigeu geu, kwani maafisa elimu au walimu wakuu wasifanye hadi waziri?
Kwa mfumo wa Elimu Tanzania ni Waziri wa Elimu peke yake ndiyo mwenye mamlaka hayo. Jamaa yenu tulimlaumu kwa kuwa alipora madaraka ya wengine na taasisi zao kinyume cha sheria.

Katika hili Waziri wa Elimu kapewa madaraka hayo.
 
Wazazi ongeeni na walimu, sio kila kitu kigeuzwe siasa.
Kwa ivo siasa kazi yake nini sasa. Yaani watu wanalipwa mamilioni ya shilingi na marupu rupu mengi tu mnataka wafanye kazi gani sasa??
 
Kwa mfumo wa Elimu Tanzania ni Waziri wa Elimu peke yake ndiyo mwenye mamlaka hayo. Jamaa yenu tulimlaumu kwa kuwa alipora madaraka ya wengine na taasisi zao kinyume cha sheria.

Katika hili Waziri wa Elimu kapewa madaraka hayo.
Je maafisa elimu majukumu yao nini?
 
Back
Top Bottom