Biashara yoyote yenye mauzo ghafi 14m na kuendelea.jamani naombeni elimu. Efd machine hata kwenye Duka la mangi? au
Unashauri zoezi lingechukua muda gani?Mashine zimeuzwa miaka 7 halafu unataka zote ziwekewe software mpya ndani ya siku 30 , inawezekana kweli ?
Mashine yangu ilikubali upgrade,sikununua na ilifanywa bure na supplier.Kingine ni kwamba kuna gharama ya marekebisho hayo zinazolipwa na Mfanyabiashara binafsi , na kuna baadhi ya mashine hazikubali hiyo software , hivyo ni lazima huyo mfanyabiashara anunue mashine mpya , jambo kama hili katika biashara hizi za sasa unawezaje kuweka muda wa siku 30 ?
Unajua kwanini wameweka hio system ya barcode?Kuna siku nililalamika kuhusu ili jambo kuna kichaa mmoja akaona ni suala dogo. Magufuli ajaribu kuangalia sana hawa TRA hawana nia njema kbs na kama ndio anawatuma kuna jambo analitafuta. Kulikuwa na uharaka gani? EFD zina serial number zina TIN namba hili janga la BARCODE linakuja kuharibu kbs biashara za watu. TRA wajiangalie biashara haifanywi kwa sifa za kijinga unatoa mwezi mmoja ili iweje.
Swali lako lielekezwe kwa mawakala , angalau kila wakala anajua idadi ya mashine alizosambaza na bila shaka anajua kwa siku 1 angeweza kurekebisha mashine ngapi , baada ya hapo ingekuwa rahisi sana kwa TRA kujua zoezi hilo laweza kwisha kwa muda ganiUnashauri zoezi lingechukua muda gani?
hii unamaanisha Kwa mwaka mkuu sio?Biashara yoyote yenye mauzo ghafi 14m na kuendelea.
Kwa mwaka.hii unamaanisha Kwa mwaka mkuu sio?
mauzo ghafi Kwa ngeli ni nini?
je yakiwa chini ya 14m unataka nini mtu akinunua kitu? Au najitengezea za kwangu stationery?
Yes huu ujinga mawakala wanapiga watu sanaOn upgrading of EFD:Kuna tatizo upande wa Wakala wa Permagon Mwanza Nyerere Road wanalazimisha wafanya biashara kununua betri mpya kwa ajili ya EFD ili hali zilizokuwepo zinafanya kazi. Hoja eti mfumo mpya ili ufanye kazi vizuri lazima uweke betri mpya. This technicality is nonsense Mamlaka ziangazie hili. Ni usumbufu na inaongeza gharama
Ndugu umewahi kufanya biashara yoyote hata ya genge lakuuza pilipili maana ulichoongea hapa inadhihirisha ni mtumwa wa ajiraWacha kamba wewe, mwezi moja unatosha sana nyinyi mmezoea kazi ndogo kama hizi kufanywa kwa miezi sita. Hakuna huo mpango hivi sasa. Baada ya mwezi lazima wamalize wafanye kazi usiku na mchana.
Yangu mpaka sasa inafanyakazi na bado sijaUpgradAnzia tar 3 Dec mashine yako ilikuwa inafanya kazi??
Unaongea usichokijua nadhani wee ni muajiriwa huwezi kuelewa kituKwanza nikupongeze kwa kujua kudiscuss. Kitu kistaarabu sio Kama hawa wengine kitu hakijui anakurupuka tu kuongea
Mimi nachojua mkuu kwanza tra walitoa waraka
Pili waliblock mashine zote.kama unavojua efd yako ikiwa na shida immediately unatakiwa ureport.sasa Kama mashine umezimiwa tuassume huna taarifa ya kuupgrade mashine then umefanyeje biashara mwezi mzima bila mashine??
Ndugu nikisoma comments za huyo anaejiita natafuta naona Nchi bado ina wajinga wengi sanaKingine ni kwamba kuna gharama ya marekebisho hayo zinazolipwa na Mfanyabiashara binafsi , na kuna baadhi ya mashine hazikubali hiyo software , hivyo ni lazima huyo mfanyabiashara anunue mashine mpya , jambo kama hili katika biashara hizi za sasa unawezaje kuweka muda wa siku 30 ?
Acha uongo gharama ya kuUpgrade ni elf 80Mashine yangu ilikubali upgrade,sikununua na ilifanywa bure na supplier.
asante mkuu. hayo mengine hujanijibu lkn. kwamba Mimi ni below 14m he natengeneza risiti stationary au si lazimaKwa mwaka.
Gross ndio ghafi
Yeah unatoa risiti ya kawaida. Ya kutengeneza ila unaweka jina na TIN yakoasante mkuu. hayo mengine hujanijibu lkn. kwamba Mimi ni below 14m he natengeneza risiti stationary au si lazima
Hili jambo wanaliona labda ni dogo lakini kuna manung'uniko makubwa ndani ya mioyo ya wafanya biashara kwa sababu jambo hili lingepewa muda lifanyike vizuri. Nenda pale ' web technologies ' pale Fire, Kariakoo kuna msongamano mkubwa sana usio wa lazima ambao hata unaweza kuleta madhara mengine na hasa kutokana na hali ilivyo huko duniani kwa sababu hatuwezi kujua nani kaja jana au juzi na huko alikutana na watu gani.
Kwa sababu kodi inalipwa na imekuwa ikilipwa ni swala la kufanya 'upgrading' tu,basi lipewe muda lifanyike kwa ufasaha bila madhara au manung'uniko na kuanza kuisema vibaya serikali kwa sababu tunajua lengo ni zuri kutokana na hili zoezi. Tunaomba hata ikibidi Rais alisikie hili na kulitolea tamko ili muda wa zoezi hili uongezwe.