Waziri wa fedha ingilia kati sakata la uboreshaji wa mashine za EFD, kamishna wa TRA ataleta balaa kubwa

Waziri wa fedha ingilia kati sakata la uboreshaji wa mashine za EFD, kamishna wa TRA ataleta balaa kubwa

Muda uliotolewa wa kuboresha Mashine za EFD wa mwezi mmoja (kuanzia desemba 7 hadi Januari 7) hautoshi, kwa sababu mawakala wanaofanya kazi hiyo wamezidiwa na kazi hiyo kutokana na wingi wa mashine hizo na tayari wameomba kuongezewa muda wa kufanya marekebisho hayo ya ghafla yaliyosababishwa na TRA wenyewe kutokana na sababu zisizofahamika.

Tayari Kamishna wa TRA amekataa kuongeza muda na ameahidi kuwaadhibu wafanyabiashara walioshindwa kuboresha machine zao za EFD kwa muda uliopangwa , hapa analenga kuwakamua pesa wafanyabiashara ambao tayari wana hali mbaya kutokana na kuzorota kwa biashara nchini.

Sasa kwa hali hii kamishna haondoi Tatizo bali anaharibu zaidi, ikumbukwe kwamba wafanyabiashara wenye EFD hawajakataa kuboresha mashine zao bali mawakala wenye dhamana hiyo wameshindwa kumaliza kazi kwa wakati, wako ambao mashine zao ziko kwa mawakala mpaka sasa zikisubiri foleni ya kuboreshwa, sasa kamishna anapokataa kuongeza muda halisaidii Taifa bali ataleta mkanganyiko zaidi.

Namuomba Waziri wa fedha aingilie kati jambo hili ili kuokoa biashara za watu kwa Manufaa ya Taifa.
Wacha kamba wewe, mwezi moja unatosha sana nyinyi mmezoea kazi ndogo kama hizi kufanywa kwa miezi sita. Hakuna huo mpango hivi sasa. Baada ya mwezi lazima wamalize wafanye kazi usiku na mchana.
 
ITV waliweka hiyo clip ya malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara kwenye YouTube channel yao naona imefutwa kwa sababu wazijuazo wao.

Ilikuwa inaonyesha hadi tarehe 6 January kuna wafanyabiashara wengi walikuwa hawajui wanatakiwa kubadili system za mashine zao wamepokea txt tarehe sita ikiwaonya tarehe 7 mwisho, yaani wana masaa 24 ya ku update mashine ama fines.

In short ni chaos ukiangalia ile clip kuanzia communication za TRA kwa wafanyabiashara hadi kwenye uratibu wa zoezi zima kutokana na uwezo wa mdogo wa makampuni yanayotakiwa kufanya update given demand and their daily capacity.
Walitoa mwezi mzima.kwanza waliblock mashine zote toka tar moja Dec .Sasa hao wafanyabiashara muda wote mashine zilivoblokiwa walikuwa wapi??
 
Muda uliotolewa wa kuboresha Mashine za EFD wa mwezi mmoja (kuanzia desemba 7 hadi Januari 7) hautoshi, kwa sababu mawakala wanaofanya kazi hiyo wamezidiwa na kazi hiyo kutokana na wingi wa mashine hizo na tayari wameomba kuongezewa muda wa kufanya marekebisho hayo ya ghafla yaliyosababishwa na TRA wenyewe kutokana na sababu zisizofahamika.

Tayari Kamishna wa TRA amekataa kuongeza muda na ameahidi kuwaadhibu wafanyabiashara walioshindwa kuboresha machine zao za EFD kwa muda uliopangwa , hapa analenga kuwakamua pesa wafanyabiashara ambao tayari wana hali mbaya kutokana na kuzorota kwa biashara nchini.

Sasa kwa hali hii kamishna haondoi Tatizo bali anaharibu zaidi, ikumbukwe kwamba wafanyabiashara wenye EFD hawajakataa kuboresha mashine zao bali mawakala wenye dhamana hiyo wameshindwa kumaliza kazi kwa wakati, wako ambao mashine zao ziko kwa mawakala mpaka sasa zikisubiri foleni ya kuboreshwa, sasa kamishna anapokataa kuongeza muda halisaidii Taifa bali ataleta mkanganyiko zaidi.

Namuomba Waziri wa fedha aingilie kati jambo hili ili kuokoa biashara za watu kwa Manufaa ya Taifa.
Walitoa mwezi mzima ulikuwa wapi??
 
Wewe unaandika usichokijua , nakupuuza rasmi , halafu usione tunaandika humu basi ukadhani haya ni mambo yetu binafsi , sisi ni watetezi tu
Mtetezi wa Nani? Wamekutuma? Ungewauliza mashine zao walipeleka lini?
Tatizo watanzania ni watu wasiojali.unamuona kamishna hata akili sio??
 
Wacha kamba wewe, mwezi moja unatosha sana nyinyi mmezoea kazi ndogo kama hizi kufanywa kwa miezi sita. Hakuna huo mpango hivi sasa. Baada ya mwezi lazima wamalize wafanye kazi usiku na mchana.
Achana nao mkuu .muulize alipeleka mashine yake lini??
 
Walitoa mwezi mzima.kwanza waliblock mashine zote toka tar moja Dec .Sasa hao wafanyabiashara muda wote mashine zilivoblokiwa walikuwa wapi??
Hiyo ndio hoja ya TRA walitoa hizo info in advance ila kwenye mkutano wao na wafanyabiashara Kagera kupitia ITV asilimia kubwa ya wafanyabiashara wanadai hawakuwa na hizo taarifa.

Sina shaka TRA wanasema ukweli walitoa notice a month in advance ila issue how did they communicate that message kwa wafanyabiashara wote nchini. Kwa ivyo sina shaka pia kuna wafanyabiashara wengi hawakua na taarifa maana wengi kilichowaogopesha fines, kwa maana hiyo wangejua wangetii.

Mbona walituma text kwa wengi siku ya mwisho kwanini awakufanya ivyo siku ya kwanza.

Changes kubwa kama hizo zinataka using various communication channels to reach your audience na sidhani kama mwezi unatosha kuanzia tangazo mpaka mabadiliko. TRA wenyewe wanakiri capacity ya kampuni zinazofanya upgrade ya hizo machine ni ndogo to meet the deadline wameruhusu watu watoe paper receipts.

Kwa kifupi zoezi alikuandalia vizuri awajajifunza tu jinsi ya kufanya mabadiliko kupitia kwa Makamba wakati anatoa zuio la mifuko ya plastic. Mbona Ummy Mwalimu somo kalielewa vitu vingine vinahitaji kuwapa watu habari na reasonable time.
 
Back
Top Bottom